i hope atakuwa amefariki huku akiwa amepatana na le mutuz, ni muhimu sana ukiwa hapa duniani kuelewa kwamba kama hutasamehe wengine Mungu hawezi kukusamehe pia. watu walishangilia kifo cha mafu lakini leo hii watakuwa wamekutana huko. jueni kwamba hapa duniani si mahali pa milele, unapoishi hapa duniani unatakiwa kuiandaa milele yako utaishi wapi. kuna njia mbili tu, motoni na uzima wa milele na vyote viwili vinaandaliwa ukiwa bado mzima hapa duniani. uwe na pesa uwe na chochote hautaenda navyo, ukifa utaviacha ila kule kama hukufanya maandalizi utajuta heri usingelizaliwa.
le mutuz alikuwa na ugomvi na uyu dada kwasababu lemutuz ni mtoto wa kambo na amehangaika sana akitengwa, na hata kurudi kwake hapa bongo waliamini amerudi kuja kusubiri amiliki mali/mirathi ya dingi yao. nakumbuka kwenye kitabu chake aliongea mengi sana na namna alivyokimbia hadi nchi kwasababu kuna watu walimtakia mabaya kwasababu tu yeeye ni mtoto wa kambo. inauma sana wakati mwingine, imagine unazaliwa mtoto wa kambo huna hatia yeyote na hukuwepo wakati wazazi wanapambana kukutafuta pale kitandani, ukiwa huku duniani unaanza kulipa makosa ya wazazi wako, just kwasababu unafikiriwa usije kumiliki mali za baba. mali na vitu vyote vinapita lakini Neno la Mungu ladumu milele. Neno la Mungu linasema tupendane na pia samehe, usiposamehe hata Mungu hatakusamehe.
sifurahii kifo, kifo ni kichungu, najua kufiwa kunavyouma, nimefiwa na baba, mama na ndugu zangu wa tumbo moja, naelewa uchungu wake, nawaombea wanafamilia wapate faraja wao kama wao kusonga mbele wakimkumbuka Mungu wangali hai kwasababu kila mtu atabeba furushi lake mwenyewe na atatoa hesabu ya maisha yake binafsi. watu wengi wanakebehi wokovu, Yesu Kristo ametoa uhai wake ili iwe kafara ya dhambi zao na maisha yao lakini wao wanachagua dunia kuliko Mungu,
Damu ya thamani kuliko vitu vyoote imemwagwa, damu isiyo na hatia yeyote, a plan which God had for years, kwamba kwa Damu /kafara la Yesu wanadamu wapate access ya kuingia katika ufalme wake, lakini wanadamu wanachagua mauti badala ya uzima, wanaangalia kwa macho ya mwilini kuthamini mali na vitu vinavyopita ambavyo pia hata ukiwa kwa Mungu unaweza kuvipata. watu wanaabudu pesa na kazi za dunia/ajira. watu wanaabudu nafasi zao za kazi n.k, wanasahau kwamba kuna siku vyote hivyo vitapita na watasimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya kila jambo walilolifanya. Mungu atusaidie.