TANZIA Dkt. Mwele Ntuli Malecela afariki Dunia, aligombea Urais wa JMT 2015

TANZIA Dkt. Mwele Ntuli Malecela afariki Dunia, aligombea Urais wa JMT 2015

View attachment 2115127
Mwele Ntuli Malecela (alizaliwa tarehe 26 Machi 1963) alikuwa mkurugenzi wa taasisi ya tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI).

Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela amekua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa Afrika kama msimamizi wa maswala ya utawala, sera na ushauri wa kidiplomasia.

Pia, soma:

1) Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi NIMR Dr. Mwele Malecela

2) Rais Magufuli: Aliyetangaza ugonjwa wa ZIKA nchini alikuwa anatumika na ndiyo maana nilipomfukuza, waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi

3) Dr. Mwele Malecela aula WHO

4) Dr. Mwelecele (aka Mwele) Malecela pamoja na Dr. Kigwangala wamechukua fomu ya kugombea Urais wa JMT

Nimesikia ni cancer ingekuwa vizuri kama ni cancer waseme ili kusaidia watu kwenye hospitali mapema. Cancer ni kuiwahi🙏 RIP
 
View attachment 2115127
Mwele Ntuli Malecela (alizaliwa tarehe 26 Machi 1963) alikuwa mkurugenzi wa taasisi ya tafiti za kiafya Tanzania (NIMRI).

Aliwania nafasi ya mgombea wa uraisi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kuanzia Aprili 2017 Mwele Malecela amekua akifanya kazi na Shirika la Afya Duniani (WHO) upande wa Afrika kama msimamizi wa maswala ya utawala, sera na ushauri wa kidiplomasia.

Pia, soma:

1) Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mkurugenzi NIMR Dr. Mwele Malecela

2) Rais Magufuli: Aliyetangaza ugonjwa wa ZIKA nchini alikuwa anatumika na ndiyo maana nilipomfukuza, waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi

3) Dr. Mwele Malecela aula WHO

4) Dr. Mwelecele (aka Mwele) Malecela pamoja na Dr. Kigwangala wamechukua fomu ya kugombea Urais wa JMT

Apumzike kwa amani mzalendo Dr. Mwele Ntuli Malecela



From the archives:

4 December 2019

Keynote Address by From Dr. Mwele Malecela, Director, Department of Control of NTDs, WHO.

 
i hope atakuwa amefariki huku akiwa amepatana na le mutuz, ni muhimu sana ukiwa hapa duniani kuelewa kwamba kama hutasamehe wengine Mungu hawezi kukusamehe pia. watu walishangilia kifo cha mafu lakini leo hii watakuwa wamekutana huko. jueni kwamba hapa duniani si mahali pa milele, unapoishi hapa duniani unatakiwa kuiandaa milele yako utaishi wapi. kuna njia mbili tu, motoni na uzima wa milele na vyote viwili vinaandaliwa ukiwa bado mzima hapa duniani. uwe na pesa uwe na chochote hautaenda navyo, ukifa utaviacha ila kule kama hukufanya maandalizi utajuta heri usingelizaliwa.

le mutuz alikuwa na ugomvi na uyu dada kwasababu lemutuz ni mtoto wa kambo na amehangaika sana akitengwa, na hata kurudi kwake hapa bongo waliamini amerudi kuja kusubiri amiliki mali/mirathi ya dingi yao. nakumbuka kwenye kitabu chake aliongea mengi sana na namna alivyokimbia hadi nchi kwasababu kuna watu walimtakia mabaya kwasababu tu yeeye ni mtoto wa kambo. inauma sana wakati mwingine, imagine unazaliwa mtoto wa kambo huna hatia yeyote na hukuwepo wakati wazazi wanapambana kukutafuta pale kitandani, ukiwa huku duniani unaanza kulipa makosa ya wazazi wako, just kwasababu unafikiriwa usije kumiliki mali za baba. mali na vitu vyote vinapita lakini Neno la Mungu ladumu milele. Neno la Mungu linasema tupendane na pia samehe, usiposamehe hata Mungu hatakusamehe.

sifurahii kifo, kifo ni kichungu, najua kufiwa kunavyouma, nimefiwa na baba, mama na ndugu zangu wa tumbo moja, naelewa uchungu wake, nawaombea wanafamilia wapate faraja wao kama wao kusonga mbele wakimkumbuka Mungu wangali hai kwasababu kila mtu atabeba furushi lake mwenyewe na atatoa hesabu ya maisha yake binafsi. watu wengi wanakebehi wokovu, Yesu Kristo ametoa uhai wake ili iwe kafara ya dhambi zao na maisha yao lakini wao wanachagua dunia kuliko Mungu,

Damu ya thamani kuliko vitu vyoote imemwagwa, damu isiyo na hatia yeyote, a plan which God had for years, kwamba kwa Damu /kafara la Yesu wanadamu wapate access ya kuingia katika ufalme wake, lakini wanadamu wanachagua mauti badala ya uzima, wanaangalia kwa macho ya mwilini kuthamini mali na vitu vinavyopita ambavyo pia hata ukiwa kwa Mungu unaweza kuvipata. watu wanaabudu pesa na kazi za dunia/ajira. watu wanaabudu nafasi zao za kazi n.k, wanasahau kwamba kuna siku vyote hivyo vitapita na watasimama mbele za Mungu kutoa hesabu ya kila jambo walilolifanya. Mungu atusaidie.
 
[emoji871]Kwa wale mnaoshabikia vifo vya mahasimu wenu mnalo kubwa la kujifunza.

[emoji871]Hapo ndio muelewe kila mtu na tarehe yake Kiganjani.

[emoji871]Kubaki Duniani ukiwa hai huwa kuwategemea kudra za mwenyezi Mungu.

[emoji871]Kuna watu huwa wanapost kama vile wanao mkataba na Mungu.

Tumuombee marehemu pumziko jema la milele.
Yeye ameumaliza mwendo ila bado safari yetu. [emoji120]
 
Niki piga hesabu za haraka haraka huyu atakuwa ni mtoto wa5 ndani ya familia ya mzee malechela kufariki, sijui kunani japo kufa kupoo tuu
 
She is very beautiful woman🥰🥰🥰
View attachment 2115165
Rest well Mwele, Mwele Ntuli! You were one of the finest brain in Tanzania! You furthered research on NTDs! and surely matende and mabusha are a history in Tanzania!

I will always remember you as one of the pillars of research excellency in Tanzania! NIMR shone during your tenure! You were a rare gem! Pumzika kwa amani mwana mwema wa mama Tanganyika!
 
Back
Top Bottom