Dkt. Mwigulu asema Nchi haiwezi kupigwa Tsh. 30 Trilioni wakati Bajeti yetu haivuki Tsh. Trilioni 50, Mpina asema Waziri hajui lolote

Dkt. Mwigulu asema Nchi haiwezi kupigwa Tsh. 30 Trilioni wakati Bajeti yetu haivuki Tsh. Trilioni 50, Mpina asema Waziri hajui lolote

Wote wezi tu ndio maana hawamchukulii serious. Ni sisi wananchi tusiokua na akili ndio tunamuona Mpina ni mzalendo!! Huyu Mpina anayetaka ripoti ya CAG iheshimike huko nyuma aliwahi sema inatumika kumchafua JPM na alikua mmojawao waliotaka CAG Assad achukuliwe hatua na bunge!! Cha ajabu leo hana uwaziri ndio anaamini ripoti za CAG?

To hell
Mpina mhuni mhuni anapiga kelele kwa sababu hajapewa uwaziri tu
 
hivi huyu mjamaa hua ana uchungu kweli na rushwa nchini au ana uchungu wa kutemwa na kuachwa kunako baraza la mawaziri serikalini?
Maana hayo yanafanyika, yumo serikalini anayaona na amekaa kimya tuli analamba Asali tu......
jamaa zingine dezi sana....
Kwanini Mpina akiikosoa serikali mnasema ana uchungu na kuachwa kwenye Baraza?mbona Mawaziri wengi tu awamu ya tano waliachwa na Huwa wanachangia hoja Bungeni, kwanini Mpina?
Kwani ukiondolewa kwenye Uwaziri ndiyo huruhusiwi kuwatetea Wananchi?
Acheni siasa za kishamba!
 
thumbs_b_c_46a028195dc2d0cfaff584795528ec97.jpg

African-Hospital.jpg

Athari za UPIGAJI ziko Dhahiri👆
 
Mpina ana ujumbe mzuri ila yeye ni mjumbe haramu ambaye hana sifa za kuongea anayoongea. Ni mtu aliyewatia umaskini wavuvi wa nchi hii. Au mmesahau alivyokuwa anapima samaki kwa rula? Mpina ni jitu la hovyo linalopaswa kupuuzwa. Ni mnufaika mkubwa wa udhalimu wa awamu ya 5
 
Mbunge Mpina asema hii nchi inapigwa kila kona na zaidi ya Tsh. 30 Trilioni zimepigwa na nyingine zimesafirishwa/ kutoroshwa nje ya nchi.

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba PhD amesema anachosema Mpina hakiwezekani kwa sababu Bajeti ya nchi haizidi tsh 50 trilioni.

Mpina ameomba Waziri Dr Mwigullu PhD na Prof. Mbarawa Wakamatwe na kufungwa kwa Uhujumu Uchumi.

----
Hivi ndivyo ilivyokuwa ndani ya Bunge, leo Novemba 3, 2023 wakati Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina alipokuwa akichangia hoja kisha kujibiwa na Mbunge na Waziri wa Fedha, Mwigulu Lameck Nchemba kuhusu upigaji wa zaidi ya Tsh. Trilioni 30.
Mungu mbariki Mpina
 
Mwigulu amekuwa akihenyeshwa na Mpina karibia miezi sita mfululizo, hana hamu kabisa na huyo jamaa.

Huyo Mbarawa ni sawa na mdoli tu wa Samia, hata yeye binafsi naamini anajua kabisa hastahili kuendelea kuwepo kwenye hiyo nafasi, amshukuru dada yake anayemlinda.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Denoo, upo!
 
Ok. Tukubaliane na Mwigulu kuwa nchi haiajapigwa trilioni 30, basi Mwigulu aseme, yeye na wenzake wameipiga nchi kwa trilioni ngapi?

Maana hajakanusha kuwa nchi haijapigwa bali anachokataa ni kiasi walichokipiga.
Changamoto kubwa ni watu wengi kushindwa Kutofautisha nchi na serikali.
Utoroshaji wa pesa za sekta binafsi nao ni sehemu ya upigaji dhidi ya nchi.
Bajeti ya serikali yaweza kuwa tofauti na hali halisi ya uchumi wa nchi kwa ujumla, hasa pale sehemu kubwa ya uchumi inaposhikiliwa na wageni.
 
Kwanini Mpina akiikosoa serikali mnasema ana uchungu na kuachwa kwenye Baraza?mbona Mawaziri wengi tu awamu ya tano waliachwa na Huwa wanachangia hoja Bungeni, kwanini Mpina?
Kwani ukiondolewa kwenye Uwaziri ndiyo huruhusiwi kuwatetea Wananchi?
Acheni siasa za kishamba!
check namna wanavyochangia utaona tofauti kuuubwaaaa baina yao......

angalia michango ya mpina tangu atemweeee ni deconstractive criticism ambazo hakuna ataezifanyia kazi hata nukta....
 
Mwigulu anajibu huku anakigugumizi cha hofu
 
Huyu mpina si nasikia anaenda chadema sasa yote ya nini si aende tu bila kuleta umbea na majungu?
 
Hakuna jitu jinga kama Mpina, lenyewe ndio halijui kitu. Namfahamu tangia kaiwa Mzumbe huwezi kwa namna yoyte kumlimganisha hata kwa tone na Mwigulu.

Huwa linaongeaga kwa jazba kukosa uwaziri, shida ni kwamba halina impact ktk nchi hii. Amesharudisha yale mashamba alowadhulumu wananchi kule Morogoro?
Bungeni hawatumii akili za darasani,; kibajaji na msukuma wasingekuwa bungeni.
 
Ok. Tukubaliane na Mwigulu kuwa nchi haiajapigwa trilioni 30, basi Mwigulu aseme, yeye na wenzake wameipiga nchi kwa trilioni ngapi?

Maana hajakanusha kuwa nchi haijapigwa bali anachokataa ni kiasi walichokipiga.
ni udhaifu wa speaker- ama mwenyekiti wa Bunge, angewaambia tu kila mtu athubitishe madai yake tuone mbivu na nchi
 
Hivi ile Ripoti ya CAG Ndiyo imeanza kujadiliwa Tuache Bunge lifanye kazi yake..Tutaona Mwisho wake
 
Back
Top Bottom