Mimi sikatai madhara ya Chanjo iliyoharakishwa kama ilivyofanyika na inavyoendelea kufanyika hata sasa kwa ugonjwa wa Corona. Hata hivyo, siwezi kukubaliana kuwa kwa kuwa majaribio yamefanyika nchi za baridi ndiyo iwe sababau ya msingi ya kukataa chanjo. Viongozi wetu watumieni Wataalamu wa Sayansi za Afya katika kutoa hoja zinazogusana na sayansi. Chanjo zote katika nchi yetu tangu uhuru zimetoka na zimefanyiwa utafiti huko huko katika nchi za baraidi na bado zilitufaa na zimeendeleea kutufaa hata sasa, Chanjo ya surua, pepopunda na kadhalika. Hazikutafitiwa Dar es Salaam hata mojawapo! Hatukuzikataa kwa sababu tafiti zake zilifanyika nchi za baridi. Zipo sababu za msingi na maana zaidi ya kukataa au kuchelewa kuzikubali chanjo za Corona kwa sababu nyingi za kisayansi, lakini si kwa sababu dhaifu ya mahali zilipofanyika tafiti zake. TUKUMBUKE, miaka ya 1980's kulikuwa na mradi mkubwa sana wa chanjo chini ya Wizara ya Afya ambao uliitwa "Cold Supply Chain" ambao ulitulazimu sehemu zisizokuwa na umeme yalinunuliwa MAJOKOVU YA MAFUTA YA TAA ili kuhakikisha Chango zinakuwa kwenye ubaridi unatakiwa muda wote. Kisayansi, hata chanjo ikitafitiwa na kutengenezwa Dar es Salaam, BADO ITAHITAJI KUTUNZWA KWENYE UBADIRI UNAOTAKIWA KWA AINA YAKE YA CHANJO. Ninaomba kuwasilsha,