Dkt. Mwigulu: Kabla ya Samia kuingia madarakani mabenki yetu yaliishiwa pumzi

Moja ya sifa ya kuwa mwana siasa ni akili kukaa tenge, hata kama utakuwa umesoma vitabu vyote vya dunia hii.
 
Anaongea kana kwamba hakuwahi kuitumikia awamu ya tano. Mwigulu ni hatari sana. Ni wa kuogopa kama Covid-19.
 
Si uongozi, ni sheria tulizo nazi ndio tatizo. Nafuu ya mtanzania inatokana na huruma ya mtawala, si sheria.
 
Mzilankende Mnyago
Dikteta aliumiza wengi sana, aliua ndoto za watu wengi, Madelu naye alikuwa ni muhanga wa Uchwara, sidhani kama hii 5 mingine angemaliza naye! Umeona wapi mchumi anapewa wizara ya sheria aiongoze??
 
Si uongozi, ni sheria tulizo nazi ndio tatizo. Nafuu ya mtanzania inatokana na huruma ya mtawala, si sheria.
Sheria ya TRA ambayo inawapa mamlaka ya kufreez account ilitumika vibaya ..tena ilitumika kulipa visasi
Nakubaliana na wewe sheria zetu ni tatizo
 
Kabla ya Samia Nchi ilikuwa inaongozwa na chama gani? Nae alikuwa katika nafasi gani
 
Kaongea ukweli lakini
Sasa ukweli ni upi, kati ya huu na ule alisema Magufuli anastahili kuwa Rais wa Afrika kwa kupandisha uchumi wa nchi?
Maana kauli zote zimetoka kwa mtu mmoja
 

Kwa sasa wananchi wa kawaida ndio wanapumulia mashine. Kila kitu bei juu. Gharama za maisha zimepanda mara dufu. Kila bidhaa bei ghali. Umeme, maji, mafuta, nafaka, usafiri vyote viko juu!

Jua nalo linakausha mazao kabla ya wakati wake, baadhi ya maeneo mifugo inakufa kwa ukame. Kila kukicha, afadhali ya jana. Wananchi wa kawaida wasio na mtetezi kwa sasa ndio wanaopumulia mashine!
 
Hakuna mtu asiye na mtetezi nchi hii, acha propaganda mfu! And wananchi wapi ni wa kawaida na wapi siyo wa kawaida?
 
Hakuna mtu asiye na mtetezi nchi hii, acha propaganda mfu! And wananchi wapi ni wa kawaida na wapi siyo wa kawaida?
Wananchi wa kawaida ni wale wasiokuwa kwenye mfumo wa uongozi na sio viongozi. Wasio wa kawaida ni viongozi na watawala. Hili halihitaji nguvu nyingi kuelezea. Hata wao kwenye hotuba zao, husema 'kwa mwananchi wa kawaida...'

Kuhusu utetezi, wale wanaotetea wengi wao hulinda zaidi maslahi yao. Je, imeshindikana kabisa kudhibiti mfumuko wa bei? Kabla ya march 2021, bei za bidhaa zikikuwa nafuu. Lakini baada ya hapo, kila bidhaa inazidi kupanda. Nani anazungumzia hili?
 
Unafiki tu ni vile ulipitiwa. Serikali dharimu hazifai.

Tuombe Mungu atupatie viongozi weledi na kuwafyekelea mbali mabaradhuli wote.
 
Hata hao CRDB wameanza ujenzi wa jengo lao kwenye utawala wa Magufuli! Halafu kuna mjinga anasema benki zilikuwa zinapumulia mashine! Ndo maana analeta matozo kana kwamba hakuwahi kusoma uchumi! Mjinga sana huyu bwana!
Kabla ya Samia Nchi ilikuwa inaongozwa na chama gani? Nae alikuwa katika nafasi gani
 
Wapunguze tozo za mihamala ya kwenye simu waone kama tutaenda tena kwenye mabenk yao.
 
Reactions: Ame
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…