Dkt. Mwigulu: Kabla ya Samia kuingia madarakani mabenki yetu yaliishiwa pumzi

Dkt. Mwigulu: Kabla ya Samia kuingia madarakani mabenki yetu yaliishiwa pumzi

Utawala wa jiwe ulikuwa na shida nyingi sana
Yuko sahihi Kilicholeta shida hiyo ni kitengo cha Anti money laundering na TRA
Mfano wewe Dalali wa mteja anakuwekea Milioni 20 kwenye Akaunti umnunulie mzigo mfanyabiashara wa kongo au Zambia au Malawi au mtu wa mikoani TRA walikuwa wanatreat zote kama mauzo yako ndio maana Kariakoo images business.Walitreate ni income wakiona tu pesa zimeingia kwenye akaunti hiyo wanachululia income! Wakati ni pesa iko held on trust huanza chochote .Waligeuza Akaunti za kampuni kama income akaunti na income statement kwa kila kilichoingia

Au mteja anakuachia mazao umuuzie umpe chake huwezi kaa na mipesa yote nyumbani ukienda ku deposit bank maswali Mia moja unatoa wapi kelele kibao kuwa wewe mtakatisha pesa zinazulumiwa watu wakaacha ku deposit kwenye mabenki anti money laundering walihamia na mifumo yao counter za benki watu wakaona isiwe shida tutakaa na pesa zetu nyumbani yaani hata ku deposit tu shida taabu ya nini?

Mimi ni mmoja nilipiga kelele sana humu kuwa Kitengo cha Anti money laundering kitaua mabenki nobody cared.
 
Haikuwa sahihi kabisa kwa serikali kuwa na blanket access na akaunti za wateja benki. It was inexcusable.

Credible banking industry inaruhusu access kwenye akaunti za wateja kwa kibali cha mahakama kinachopatikana kwa mchakato unaokubalika kisheria kwa kusudio maalum. Na kuna masharti yanayolinda taarifa na usalama wa akaunti hizo katika hatua hiyo.
Hili ni suala la Katiba Mpya pia
 
Hapana mimi ni mmoja niliongea humu kwenye hili hasa ila kipindi kile kuna watu waliziba masikio hata kwa vitu obvious .Anyway cha msingi mambo yanaenda vizuri kwa sasa .Let us forget the past
. Kuna mazuri sana past yalifanyika lakini kuna maeneo past walichemka mno ok hawakuwa Miungu .Tusamehe tu tusonge mbele Mungu tu ndie hakosei
Walioumizwa na matendo ya utawala wa jiwe wanapaswa kutambuliwa na kulipwa fidia, waliohusika kuumiza watu wanapaswa kuwajibishwa pia. Lazima tuwe na utaratibu wa kuwajibishana
 
Kuna swala la PayPal watanzania kuruhusiwa kupokea PayPal bado .Hili tumepiga yowe muda mrefu mno kipindi cha Magufuli chote muda wote hakuna aliyejali

Kuwa watanzania hatuwezi tu kuruhusiwa kuwa walipaji tu kupitia PayPal ,turuhusiwe pia kuwa wapokeaji sio walipaji tu. Hakuna wa kusikiliza na kufanyia kazi.Labda Mama Samia atalifanyia kazi tuombe Mungu
Nchi ya watu waliokumbatia ujima kwa muda mrefu.
Poor us.
 
Wakati yupo haya yalikuwa hayasemwi, wakisema akina Lissu wanachapwa risasi akina Mbowe wanapewa kesi za ugaidi na hakuna aliyethubutu kuwatetea katika hawa wote ambao leo wamegeuka wema wenye huruma na wananchi wakati ni mashetani wanaovuma kwa kufuata mwelekeo wa upepo unavyovuma.
 
Ila katika maboko aliyowahi kupiga Mwigulu ni lile la kutokwenda kumuona ndugu yake Lissu, and hata kutompa pole hadharani! Ile itamtoa kwenye mbio zake za 2030
 
Kinachoniuma kuna wafanyabiashara hadi leo bado hawajasimama.. Wapo hoi
Kuna mmoja alikuwa anaagiza spare za pikipiki/ Bajaji.. Nje ya nchi.. Walimdaka akaonyesha anavyolipa kodi.. Task force ya Jiwe wakamwambia unalipa kidogo..
Wakamlamba zaidi ya M 110 benki..
Mpaka leo hana uwezo wa kuagiza.. Hana mtaji.. Watu walifilisiwa..
Tuombe tuu uongozi ule usije tena katika nchi hii
Oooooooh masikini Mungu amsaidie saba
 
"Ilikuwa haisemwi kwa sauti kubwa lakini ni ukweli usiofichika kwamba mabenki yetu mengi yalikuwa yameishiwa pumzi. Ulikuwa ukienda kwenye counter zao unahesabu wateja wawili watatu na wateja wengi walikuwa wanadefault," Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba.

Ameyasema hayo leo 05/03/2022 wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la makao makuu ya CRDB, jijini Dar es Salaam.
Kama huyu ndio mshauri wa Raisi atampoteza. Huyu ni mwanasiasa .

Huo mjengo umejengwa awamu ya Tano.
Angesema tu hongera kwa ujenzi
 
"Ilikuwa haisemwi kwa sauti kubwa lakini ni ukweli usiofichika kwamba mabenki yetu mengi yalikuwa yameishiwa pumzi. Ulikuwa ukienda kwenye counter zao unahesabu wateja wawili watatu na wateja wengi walikuwa wanadefault," Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba.

Ameyasema hayo leo 05/03/2022 wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la makao makuu ya CRDB, jijini Dar es Salaam.
Kipindi kile alikuwa wapi kuyasema alivoona hali ile?
 
Huyu na Nape wanaongoza kwa unafki Tanzania

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
Hauna akili wewe, ulitaka wa act kitoto wakati ule ili waondolewe roho zao. Walichokifanya wakati wa Jiwe ni kuheshimu mamlaka. Yule jamaa ilikuwa lazima kuenda naye atakavyo mpaka mauti yalipomfika. Sasa ni taifa huru lazima maovu yake yote tuyaseme. Tena imesaidia hata waliokuwa naye karibu wanasema. Huenda wengine walitusaidia kumuondoa kwa kukubari kuwa naye. We unadhani ingewezekana vipi kumuondoa kama wote wasiomkubali wangekaa naye mbali?
 
"Ilikuwa haisemwi kwa sauti kubwa lakini ni ukweli usiofichika kwamba mabenki yetu mengi yalikuwa yameishiwa pumzi. Ulikuwa ukienda kwenye counter zao unahesabu wateja wawili watatu na wateja wengi walikuwa wanadefault," Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba.

Ameyasema hayo leo 05/03/2022 wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la makao makuu ya CRDB, jijini Dar es Salaam.
Very true maana watu waliacha kuweka hela benk maana mwendazake akiziona tu anazichukua
 
302F4CCA-2EC1-4DA0-B4B5-F3113C9C5C98.png

Asset za CRDB ambayo ni mikopo historical data zake hizo hapo mpaka 2015.
F4F4DBB6-826E-45EB-B6C1-D5E7991562C1.png

Hizo mpaka kwenye financial statement yao ya mwisho kiwango cha mikopo kimekuwa mwaka hadi mwaka.

Huyo waziri yeye katumia data gani. Mtu anaeongea chochote mdomo uende kinywani unaweza muamini kweli siku mambo yakienda mrama.

Mtu asie na kifua kama huyu ipo siku atasema zama za mama kulipa mishahara ilibidi tuwe tunatumia hela za mikopo ya maendeleo.
 
4A813607-DF35-4D12-AB98-03D04BDBA404.jpeg

Net profit ya CRDB 2015

3EACC6E6-7675-4BE2-8911-56E549FD9C79.jpeg

Hiyo ni statement ya mwisho 2020 sidhani kama washawahi kuvuka kiwango icho cha faida katika historia yao. Hiyo faida ilitokana na nini kama siyo shughuli za kiuchumi.

Sometimes bora kukaa kimya kuliko kuendekeza njaa. Bila ya hawa watu kuacha kutuchukulia poa tuna safari ndefu, the other day nilisema vijana wa miaka 30 leo na wenyewe wakirubuniwa na huu mfumo wazee wa CCM leo ambao awataki kwenda na wakati atuchomoki; kwa sababu hii age group ya kina Mwigulu ishakuwa fouled tayari kuendeleza siasa zilezile za kishamba.
 
Back
Top Bottom