Dkt. Mwigulu: Kabla ya Samia kuingia madarakani mabenki yetu yaliishiwa pumzi

Dkt. Mwigulu: Kabla ya Samia kuingia madarakani mabenki yetu yaliishiwa pumzi

Kuna ukweli/uongo ulikuwa hausemwi enzi za JPM Sasa unasemwa wakati wa Samia
Na Samia akitoka madarakani nae atasemwa tu kwa ubaya.
Hapana mimi ni mmoja niliongea humu kwenye hili hasa ila kipindi kile kuna watu waliziba masikio hata kwa vitu obvious .Anyway cha msingi mambo yanaenda vizuri kwa sasa .Let us forget the past

. Kuna mazuri sana past yalifanyika lakini kuna maeneo past walichemka mno ok hawakuwa Miungu .Tusamehe tu tusonge mbele Mungu tu ndie hakosei
 
Ni kweli alichosema lkn beans Madelu huna credibility ya kuongea haya ww ndo ulikuwa unapiga mikasi hoja za wapinzani kwny social media hatimae ukakumbukwa ni vyema ukakaa kimya pambana hapo wizara ya fedha watu watakuelewa tu sio lzm umchafue mtu ili uonekane msafi
 
"Ilikuwa haisemwi kwa sauti kubwa lakini ni ukweli usiofichika kwamba mabenki yetu mengi yalikuwa yameishiwa pumzi. Ulikuwa ukienda kwenye counter zao unahesabu wateja wawili watatu na wateja wengi walikuwa wanadefault," Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba.

Ameyasema hayo leo 05/03/2022 wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la makao makuu ya CRDB, jijini Dar es Salaam.
Huyu ndio alichora mawe, madaraja, makaravati na milima yote nchi nzima?
 
Arudi nyuma mwaka ajiulize je siku kama ya leo mwaka jana angesema kauli kama hii??
 
Jamaa hawaachi kudanganya tu.

Tozo za kwenye miamala ya simu ndio zimerejesha wateja kwenye mabenki na sio porojo za huyu jamaa.

Hali ya uchumi sasa ni mbaya kuliko awamu iliyopita.
 
Kuna siku, kutatolewa kitabu kuelezea jinsi utawala wa Magufuli ulivyokuwa mbaya kuliko utawala mwingine wowote nchini mwetu. Na kitabu kitapata mauzo makubwa sana. Na ndipo itaamliwa, pivha yake kutoonekana ofisi yoyote ya umma.
kuna ofisi yoyote ya Umma yenye picha ya Magufuli? Sisi tuliambiwa tuzishushe piacha zote na kupelekwa store siku moja baada ya kuapishwa Rais Samia.
 
"Ilikuwa haisemwi kwa sauti kubwa lakini ni ukweli usiofichika kwamba mabenki yetu mengi yalikuwa yameishiwa pumzi. Ulikuwa ukienda kwenye counter zao unahesabu wateja wawili watatu na wateja wengi walikuwa wanadefault," Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba.

Ameyasema hayo leo 05/03/2022 wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la makao makuu ya CRDB, jijini Dar es Salaam.
Duuuh, haya yalitokea Tanzania hii hii?
Sijawahi kukosa foleni Benki, hata nikiwahi Saa tatu na nusu, ntakuta watu wanasubiri.
Anyways kwa Kua ni vita dhidi ya marehemu, yatasemwa mengi.
 
Aanze kujiandaa kiti kinapwaya
Akili za kuungaunga shida sana
 
Kuna swala la PayPal watanzania kuruhusiwa kupokea PayPal bado .Hili tumepiga yowe muda mrefu mno kipindi cha Magufuli chote muda wote hakuna aliyejali

Kuwa watanzania hatuwezi tu kuruhusiwa kuwa walipaji tu kupitia PayPal ,turuhusiwe pia kuwa wapokeaji sio walipaji tu. Hakuna wa kusikiliza na kufanyia kazi.Labda Mama Samia atalifanyia kazi tuombe Mungu
 
HAWA NDIO WANASIASA WETU JAMANI TUSIWASHANGAE KABISA...............................................
 
Nimeamini Mwanasiasa akikuambia Toka Nje Kumekucha, Toka Kweli Nje
Screenshot_20220305-202446.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
CRDB ilijenga Jengo hilo katika awamu ya 5, Mwingulu ni muongo Jengo alilo lifungua lilianza kujengwa awamu ya 5, na awamu ya 6 imekuja kufungua Jengo.
 
Back
Top Bottom