Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Makamu wa Rais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewasihi Watanzania wapambane kupata katiba mpya ambayo itaipeleka nchi mbele na kuleta maendeleo.
Your browser is not able to display this video.

​
 
Kuna kitu kinapikwa hapa, tunachezewa akili mtakuja kuniambia.

Hii kauli imenifikirisha hata mimi!.

Nchimbi Dr, ni kama anaendelea kujiweka pembeni hivi..

Sasa sijui kama ametumwa au ndio dhamira yake..
Hawezi kufanya jambo bila kutumwa.
Ina maana hapo ni kutuchezea akili raia.
 
Kama haya ya kweli na ameyatoa moyoni bila kulazimishwa au kutega watanzania;-
1. Kuna kitu ameona hakipo sawa huko ameona wanachokifanya wenzake sio.
2. Anaamua kujisafisha kutoka huko ili 2030 aingie akiwa msafi.
3. Anajielewa tatizo kipingamizi kipo mbele yake ambacho ni...
SIMAMIA HAPO HAPO MZEE LAKINI KAMA UNATUCHORA TUTAJUA TU.
 
Alikuwa RPc,Mbeya na huyu jamaa aliesoma Sangu secondary school ulikuwa na walimu wazuri Sana ila vijana wahuni walijaa pale,wahindi,Waburushi,Wasomali! Nk
Sikufuatilia hili..
Nimesoma hapa jf mzee wake kumbe kafariki hapo 2022. Alikuwa rpc wa Mtwara kabla hajastaafu.

Kweli ni mtoto wa Njagu.
 
Asije akatekwa na lile genge la sa.... ambalo lilimteka hamphrey polepole.
Atekwe vipi na huu ni mkakati wao? Hivi unaamini kabisa Nchimbi kama anataka tuwe na katiba mpya atashindwa kushawishi CCM wengine? Anawaambia watanzania wanapigania katiba huku wananchi wanaohoji makosa ya serikali sasa hivi wanatekwa na kubambikiwa kesi za uhaini?
 
Hawa si ndo waliahidi wataanza mchakato ndani ya siku 100 tu baada ya uchaguzi. Sahizi tena wanatuambia tudai, washasahau waliahidi wenyewe!😁😁😁😁Tunachezewa hapa si bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…