Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Hii kauli ni kweli au ni AI?
kama ni kweli basi anakosea
Kudai katiba mpya ni kosa ?

Kwanza umeshachangia mwenge mwalimu au zile $20 mnazokatwa kihuni ndio zinaenda huko?
HN6n_h0WMAARjN2.jpg
 
Sina tatizo na Makamu wa Rais, lakini ni kwanini hawa watu wanapo ongelea Katiba wana associate na uchaguzi?? Hawajui kwamba Katiba ni maisha yetu Watanzania ambao wengine hata sio wana siasa? Hawajui kuwa unapo ongelea Katiba unaongelea uchumi wa nchi, utamaduni wa wananchi, ustawi wa jamii kwa ujumla wake, etc? Wanasiasa ni wabinafsi sana, they tend to see Katiba ni kwa ajili yao tu😔
 
Yeye siyo mtanzani? Au ametumwa kutuchora tu
Mkuu 'Bush', umenifanya nicheke.
Umejipambanua kwa hivi vimaneno vyako vichache unavyoandika humu JF.
Naona hii ni staili yako ya kipekee inayofikisha ujumbe haraka.

Bwana Nchimbi, kama walivyo wengi wenzake ndani ya chama hicho, sasa ni kama mateka tu hawajui wafanye nini.
Hawawezi/hawana uthubutu wa kusimama na kuhesabiwa kwa wanachokiamini; kwa sababu wanaogopa kutupwa nje ya ulaji wanaopewa na waovu.

Kama kiongozi huna uthubutu wa kufanya/kusema na kusimamia unachokiamini, huo ni uongozi gani.
"Anatuchora".
 
Kwani ni jambo gani jipya alilolizungumzia Nchimbi katika hotuba yake hiyo; au hayo maneno aliyotumia ya "kupambania katiba mpya"?

Mbona Samia mwenyewe, hadi aliahidi siku 100 kuanza mchakato wa Katiba Mpya!

Hapa Nchimbi hajatoka kwenye mstari hata kidogo katika mambo yaliyoko huko kwenye genge.
 
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, akizungumza leo Julai 23, 2026 katika Mkutano wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam, amesisitiza Watanzania kupambana kupata Katiba Mpya na kwamba taifa linahitaji Katiba yenye mwafaka na makubaliano ya wadau wote itakayolinda haki za raia na kulipeleka taifa mbele kwa miaka ijayo.

Dkt. Nchimbi amesema kuwa kati ya madai mengi yanayopiganiwa katika jamii, Katiba ndicho chombo pekee kinachoweza kubeba mengine yote na kubatilisha sheria yoyote inayokinzana nayo

Sasa mbona Boss wake alisema katiba haina kitu ni kikaratasi tu.
 
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, akizungumza leo Julai 23, 2026 katika Mkutano wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam, amesisitiza Watanzania kupambana kupata Katiba Mpya na kwamba taifa linahitaji Katiba yenye mwafaka na makubaliano ya wadau wote itakayolinda haki za raia na kulipeleka taifa mbele kwa miaka ijayo.

Dkt. Nchimbi amesema kuwa kati ya madai mengi yanayopiganiwa katika jamii, Katiba ndicho chombo pekee kinachoweza kubeba mengine yote na kubatilisha sheria yoyote inayokinzana nayo

Yuko sahihi 100%
 
Hii kauli imenifikirisha hata mimi!.

Nchimbi Dr, ni kama anaendelea kujiweka pembeni hivi..

Sasa sijui kama ametumwa au ndio dhamira yake..
ni dhamira yake. hata kama ametumwa jambo la katiba mpya ndio habari ya muji. Shetani akikwambia "nenda kamwabudu Mungu," kwani utabaki kuuangalia ushetani wake?
 
Back
Top Bottom