Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Umesema watanzania wapambanie katiba mpya, na ukaenda mbali zaidi kwa kusema Rais pia anaitaka katiba mpya...lakini mbona watu walio onyesha nia ya kuiipambania hiyo katiba mmewapa kesi za ugaidi na uhaini?
 

Attachments

  • downloadfile(36).jpg
    downloadfile(36).jpg
    71.6 KB · Views: 11
CCM Ina akili sana.Niliwaambia watu kwamba mwaka 2030 CCM wanaumiza kichwa wapate mtu ambae atakuwa anaongea Lugha ya Wapinzani Ili wasalie Madarakani.

Sasa ukifuatilia stori za Nchimbi utasikia ooh sijui anamsema SSH mara ooh wanamba hahusiki na Mo29. Hii ni michezo ya kuwachezea wajinga Ili waendelee kubakia Madarakani.

Akishakuwa Rais 2030 ndio mtajua ni Katiba Mpya au sio Katiba Mpya 😂😂😂😂😂

So Kwa Sasa Nchimbi ndio karata ya CCM Uchaguzi Mkuu wa 2030 chini ya Katiba Mpya.
Ndio ninachokifikiria hiki.
 
Wapi..
Nchimbi yupo tofauti na Samuya.. nitamuamini Polepole si wewe...

Ni kawaida ndani ya chama kutofautiana mawazo...

Ccm sio ya kuiamini lakini hata wao wanatofautiana...
Utajua mwenyewe nyie si ni watu wa kutumikishwa na Wanasiasa.

Kwani Magufuli hukumuamini? Hakuna anaongea Lugha za Wapinzani?

Ruto yukoje? Mtapata majibu kadiri ya mda unavyoenda.
 
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, akizungumza leo Julai 23, 2026 katika Mkutano wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam, amesisitiza Watanzania kupambana kupata Katiba Mpya na kwamba taifa linahitaji Katiba yenye mwafaka na makubaliano ya wadau wote itakayolinda haki za raia na kulipeleka taifa mbele kwa miaka ijayo.

Dkt. Nchimbi amesema kuwa kati ya madai mengi yanayopiganiwa katika jamii, Katiba ndicho chombo pekee kinachoweza kubeba mengine yote na kubatilisha sheria yoyote inayokinzana nayo

Kuna kitu, ngoja twendelee kuwa rada
 
Utajua mwenyewe nyie si ni watu wa kutumikishwa na Wanasiasa.

Kwani Magufuli hukumuamini? Hakuna anaongea Lugha za Wapinzani?

Ruto yukoje? Mtapata majibu kadiri ya mda unavyoenda.
Wewe umeumia sana kwa hio kauli ya Nchimbi... hio si lugha ya wapinzani.. ni lugha ya Watanganyika...

Na bado hadi wewe utazungumza lugha moja..
 
Back
Top Bottom