Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Kauli ya kiongozi mkubwa wa serikali kuwa "PAMBANENI MPATE KATIBA MPYA" inazua mjadala mzito wa kisera na kisiasa kwa sababu inaweza kutafsiriwa kuwa jukumu la kuleta Katiba Mpya limehamishiwa kwa wananchi, vyama vya siasa, asasi za kiraia na watetezi wa haki za binadamu, ilhali mamlaka ya kuanzisha na kusimamia mchakato huo yapo mikononi mwa serikali na taasisi zake. Kauli ya namna hiyo inaleta taswira kwamba serikali inatambua umuhimu wa Katiba Mpya, lakini haitaki kubeba wajibu wa kuiongoza hadi mwisho bila kushinikizwa. Hilo linaibua swali la msingi, ikiwa viongozi waliopo madarakani wanakubali kuwa Katiba Mpya ni hitaji la taifa, kwa nini wananchi tuambiwe tupambane kuipata badala ya kupewa ratiba, mwelekeo na dhamira ya wazi ya kuifikisha?
 
Tatizo hammjui! Kila siku nasema hapa JF kuhusu yeye, watu wanapinga. Ana msimamo na anaumia kwa haya yanayotendeka. Kuiba raslimali za Tanganyika na kuijenga Zanzibar. Ndiyo maana aliitwa Yuda na yule Mzanzibari.
Angekuwa anaumia asingekuwepo kwenye hicho cheo.
Kwa sababu hicho cheo kimepatikana kwa damu za watanzania na mpaka sasa watu wanazidi kutekwa na kufunguliwa kesi za ugaidi na yeye kama makamu haramu hawezi kumshauri boss wake haramu kwamba haya yanayofanyika siyo?
 
Angekuwa anaumia asingekuwepo kwenye hicho cheo.
Kwa sababu hicho cheo kimepatikana kwa damu za watanzania na mpaka sasa watu wanazidi kutekwa na kufunguliwa kesi za ugaidi na yeye kama makamu haramu hawezi kumshauri boss wake haramu kwamba haya yanayofanyika siyo?
Sina tofauti na wewe katika haya uliyosema hapa...

ILA; kama ameamua kwa dhamira yake mwenyewe, kwamba hawezi kuendelea na kuvumilia anayoyaona yakitendeka; na sasa anayazungumzia waziwazi; kuna sababu gani ya kutosikiliza anayosema na sisi tuamue kuyaamini au kutoyaamini?
 
Sina tofauti na wewe katika haya uliyosema hapa...

ILA; kama ameamua kwa dhamira yake mwenyewe, kwamba hawezi kuendelea na kuvumilia anayoyaona yakitendeka; na sasa anayazungumzia waziwazi; kuna sababu gani ya kutosikiliza anayosema na sisi tuamue kuyaamini au kutoyaamini?
Sawa mkuu 🙏
 
Kauli ya kiongozi mkubwa wa serikali kuwa "PAMBANENI MPATE KATIBA MPYA" inazua mjadala mzito wa kisera na kisiasa
Umeandika mambo hapa chini kana kwamba wewe ni mgeni hapa nchini asiyejuwa lolote kuhusu hilo swala la katiba linavyotumiwa na hao hao viongozi na serikali wanayoiongoza.

Yaani wewe hujui danadana zote zinazofanyika kuhusu swala hilo hilo toka enzi za Kikwete hadi sasa?

Kwamba hata hukumbuki ahadi ya Samia ya siku 100 akiwa madarakani katika serikali haramu kuwa mchakato utakuwa umeanzishwa; leo hii ni siku ngapi tokea Oktoba 2025?
 
Maswali mengineyo
Tupambane kwa kutumia nini?
Kwa nini tupambane?
Tupambanie wapi?
Kwa nini wakati huu tupambane?
Tukipambana tutakuwa na nani?
Kwa nini......kwa nini....
Swali la nyongeza,...wataua tena kama walivyo ua Oct.29 wakati tunapambana?
 
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, akizungumza leo Julai 23, 2026 katika Mkutano wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam, amesisitiza Watanzania kupambana kupata Katiba Mpya na kwamba taifa linahitaji Katiba yenye mwafaka na makubaliano ya wadau wote itakayolinda haki za raia na kulipeleka taifa mbele kwa miaka ijayo.

Dkt. Nchimbi amesema kuwa kati ya madai mengi yanayopiganiwa katika jamii, Katiba ndicho chombo pekee kinachoweza kubeba mengine yote na kubatilisha sheria yoyote inayokinzana nayo

Kwanza wajiuzulu iwepo serikali ya mpito ambayo itatayarisha katiba mpya. Yeye mwizi ana uhalali gani wa kuongoza nchi?
 
Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, akizungumza leo Julai 23, 2026 katika Mkutano wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC)

25 July 2026
GODIGODI : NGOs ZICHUNGUZWE ZINATUMIKA KUPITISHA FEDHA ZA WAHALIFU WANATUMWA NA MABEBERU KUCHAFUA

View: https://m.youtube.com/watch?v=NkBqqSM-IvU
Mwenyekiti wa Tanzania Peace Foundation Taifa Bw. Godigodi Sadick amewataka Watanzania kuwa makini .

Mjadala kuhusu uchunguzi wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) unahusisha mitazamo tofauti ya kisiasa, kiusalama, na haki za binadamu nchini Tanzania.

Mtazamo wa Serikali na Wakosoaji wa NGOs
  • Usimamizi wa Fedha: Kuna hofu kuwa baadhi ya mashirika yasiyo ya kibiashara NGOs yanapokea fedha kutoka ndani na nje bila uwazi wa kutosha wa matumizi yake.
  • Ulinzi wa Kitaifa: Wakosoaji wanadai kuwa baadhi ya wafadhili wa kigeni ("mabeberu") wanaweza kutumia NGOs kupenyeza ajenda zinazovuruga amani au misingi ya kitamaduni ya nchi.
  • Utiifu wa Sheria: Serikali inasisitiza kuwa mashirika yote lazima yafuate Sheria ya NGOs na kutoa taarifa sahihi za mapato na matumizi.

Mtazamo wa Mashirika ya Kiraia na Watetezi wa Haki
  • Uhuru wa Kiraia: Watetezi wa haki za binadamu wanaona madai haya kama mkakati wa kubana nafasi ya mashirika yanayokosoa serikali.
  • Mchango wa Maendeleo: NGOs zinasisitiza kuwa zinatoa huduma muhimu za kijamii kama afya, elimu, na msaada wa kisheria pale ambapo serikali haijafika.
  • Ukaguzi wa Kisheria: Mashirika mengi yanasema tayari yanakaguliwa na mamlaka za kodi (TRA) na Msajili wa NGOs, hivyo hakuna haja ya kuyapakaza matope kwa jumla
 
Back
Top Bottom