Upuuzi tupu.
1. Ikiwa Watanzania tuliwasaidia watu wa ANC ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Makaburu kule nchini Afrika Kusini.
2. Ikiwa Watanzania pia tuliwasaidia watu wa ZANU ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wazungu (Waingereza) kule nchini Zimbabwe.
3. Aidha, ikiwa Watanzania vile vile pia tuliwasaidia watu wa FRELIMO ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wareno kule nchini Msumbiji.
Je, ni kwa nini basi majirani zetu wa Kenya au Uganda nao wasiwe na Haki ya kuwasaidia Wananchi wa Tanzania ili waweze kuondokana na Utawala dhalimu na usiitenda Haki wa CCM hapa nchini sawa sawa kabisa na vile ambavyo waTanzania walifanya kwa majirani zao wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji?
Remember:
"Injustice somewhere is a threat of justice everywhere."
By Martin Luther King Jr.
HAKI haina mipaka, wala Haki haijali mipaka ya nchi.
Good for the Jews is good for the gunners, and bad for the Jews is also bad for the gunners.
Niungane na wewe kusema sababu zilizotolewa hazina mashiko
1. Swala la leseni ya uwakili halihojiwi na watu wa uhamiaji airport
2. Si kila wakili anayekuja Tz anakuja kwa ajili ya kesi
3. Utetezi wao kama wangeanza kuufanya wangezuiwa mahakamani maana hawana leseni hiyo.
3. Wanaosikiliza kesi pale mahakamani wapo mawakili lkn sio sehemu ya watetezi wake. Madai hayo ni ya kutupa
Lakini nipingane na wewe pia kwa sabau zote ulizotoa ambazo zinafanana ila utofauti wamaeneo
1. Utetezi wa Tz katika kupigania uhuru ulifanywa na nchi , hii maana yake sera ya serkali iliruhusu, kugharamia,kuweka kambi mafunzo kwa ajili ya ukombozi kusini mwa nchi hizo, jambo ambalo nchi ya Kenya haijawatuma kama sehemu ya wapigania Haki au Wanaharakati wanaokuja kwa ajili ya sera na lengo la serkali ya Kenya.
2. Wanasheriahao na wanaharakati walikujakama watu binafsi , kikundiau chama ambacho hakina serkali nchini mwao i.e chama cha upinzani kama msaada kwa chama cha upinzani Tz hapowalitakiwa kufuata taratibu zingine za kidiplomasia.
3. Kuzuiwa kuingia nchi yoyote ni haki ya nchi hiyo wala haiwajibiki kujieleza hata kama sababu zake hazina mashiko, watu hunyimwa Visa kwenda USA kwa sababu zisizo mashiko mf tuna wasiwasi unaweza ukaloea huko
Kwamjumuisho huo jambo hili kila upande unaeleza kwa mapungufu na kadri unavyoenda unaona nia ovu kwa makusudi yaliyolengwa
Mfano vikundi vya harakati Kenya a.k.a Gen Z kusema vitashughulika na serkali hususan Rais wa Tz huo ni upuuzi na ujinga. Mfano ni mtumizi ya nguvu kuliko hoja sioni umaana wa danadana kwa mtuhumiwa kama ushahidi haujakamilika kuendelea kushikiliwa awe huru hadi ushahidi wa serkali uwe tayari na mahakama iwe huru na wazi kwa raia kusikiliza