PreGE2025 Dkt. Ndumbaro ataja sababu kuzuiwa kwa Martha Karua kutoka Kenya, na wenzake

PreGE2025 Dkt. Ndumbaro ataja sababu kuzuiwa kwa Martha Karua kutoka Kenya, na wenzake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Leta ushahidi wako hapa kuhusu ilo...Hakuna nchi inayoweza kuruhusu ujinga wa hivyo.Nendeni mkamtetee na yeye kua alishinda uchaguzi dhidi ya Ruto
Wee kichaa kwenye orodha ya mawakili wa Lissu Kuna jina la Martha Karua?
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro amesema mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Mei 20, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.

Amesema walichokuwa wanakuja kukifanya hapa nchini ni uvunjifu wa sheria za Tanzania jambo ambalo halikubaliki.

"Kwa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania, kwa hiyo wanachokuja kukifanya ni uvunjifu wa sheria zetu lakini kwa nini waje kwetu wakati kwao yamewashinda, nyumba yako inawaka moto unataka kuuzima kwa jirani? huu ni unafiki. Na sisi Watanzania hatutaki unafiki, kwenye eneo la haki za binadamu tupo vizuri sana na naungana na Rais Samia kwenye kauli yake ya jana," amesema Ndumbaro.

Sana nimeamini kuwa mama amezungukwa na watu wenye uwezo mdogo sana wa kufikiri na kujenga hoja.
Nchi hii inapitia kipindi kigumu sana.
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Damas Ndumbaro amesema mawakili kutoka Kenya waliozuiwa kuingia nchini kumtetea Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania.

Ndumbaro ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Mei 20, 2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Jijini Dodoma.

Amesema walichokuwa wanakuja kukifanya hapa nchini ni uvunjifu wa sheria za Tanzania jambo ambalo halikubaliki.

"Kwa uelewa wangu wale hawana leseni ya kufanya shughuli za uwakili Tanzania, kwa hiyo wanachokuja kukifanya ni uvunjifu wa sheria zetu lakini kwa nini waje kwetu wakati kwao yamewashinda, nyumba yako inawaka moto unataka kuuzima kwa jirani? huu ni unafiki. Na sisi Watanzania hatutaki unafiki, kwenye eneo la haki za binadamu tupo vizuri sana na naungana na Rais Samia kwenye kauli yake ya jana," amesema Ndumbaro.

Kama ameyasema haya wazir atakua na shida!
Kosa ni kosa hata kama watatumika watu elfu kuhalalisha kilichofanyika.
Swali la kujiuliza alipokuja mara ya kwanza alifanya kazi ya uwakili? Na je kuna sheria ilivunjwa? Kwanini wabunge waliopo bungeni hawahoji? Au ni kwasababu bunge lao, spika wao, mawazir wao?
Waziri anasema watz hawapendi unafiki, unafiki gani anaozungumzia? Watz wanatekwa na kupotezwa? Wanaharakati wa haki za binadamu hawako salama? Ubadhirifu wa fedha za umma kupitia ripoti za CAG je, hatua gani zinachukuliwa? Serikali inasemaje kuhus usalama wa raia kutokana na matukio ya utekaji? Waziri anaposema tupo vizuri je, anakubaliana na kile kinachoendelea kuhusu kutekwa na kupotezwa na wanaharakati wa haki za binadamu, tupo vizuri katika angle gani? Je, CHRAGG wapo wapi? Je, unafiki Mh ametumia parameter zipi kusema sisi sio wanafiki?
 
Kutetea ujinga ni lazima ujizime ufahamu na uonekane mjinga pia.
 
Upuuzi tupu.

1. Ikiwa Watanzania tuliwasaidia watu wa ANC ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Makaburu kule nchini Afrika Kusini.
2. Ikiwa Watanzania pia tuliwasaidia watu wa ZANU ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wazungu (Waingereza) kule nchini Zimbabwe.
3. Aidha, ikiwa Watanzania vile vile pia tuliwasaidia watu wa FRELIMO ili waende kupindua Utawala wa kidhalimu na usiotenda Haki wa Wareno kule nchini Msumbiji.

Je, ni kwa nini basi majirani zetu wa Kenya au Uganda nao wasiwe na Haki ya kuwasaidia Wananchi wa Tanzania ili waweze kuondokana na Utawala dhalimu na usiitenda Haki wa CCM hapa nchini sawa sawa kabisa na vile ambavyo waTanzania walifanya kwa majirani zao wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji?

Remember:
"Injustice somewhere is a threat of justice everywhere."
By Martin Luther King Jr.

HAKI haina mipaka, wala Haki haijali mipaka ya nchi.

Good for the Jews is good for the gunners, and bad for the Jews is also bad for the gunners.
hayo uliyoandika yote yalifanyika hapa Tz na siyo katika nchi zao za Afrika Kusini, Mozambique, Angola na Zimbabwe.

Na wao wafanyie huko kwao Kenya
 
Halafu unashangaa ukiitwa mpumbavu kweli?
Halafu unachukua buku7 yako unafurahia kuwa nimewachamba kweli jamii forum.

Una tofauti gani na ling'ombe, masuala muhimu ya mustakabali wa nchi yetu mnaketa mizaha, PUMBAVU
Ndiyo maana tupo makini na Taifa letu kuliko nyie mnaotumiwa kuja kuharibu amani..WE SHALL DEAL WITH ANYONE
 
Upumbavu siyo tusi ni sifa yenu msiojitambua wazee wa buku7.

Hutaki kutambuliwa kwa sifa yako acha kutoa hoja za kipumbavu
Haya maneno siwezi kushangaa maana ata mama yako unamwambia
 
Kwa nini waziri wa sheria anajibu suala la kisheria kwa kusema "kwa uelewa wangu...".

Na kama hawana leseni ya kumtetea Tundu Lissu, kwa nini muwazuie kuingia nchini, kwa nini msiwaachie waingie nchini halafu muwakataze kumtetea Tundu Lissu?

Wapi kina Karua wamesema wanakuja kumtetea Tundu Lissu?

Are our ministers this dumb?
Kinachosikitisha zaidi ni waandishi wa habari kutokuwa na uwezo au kuhofia kumuuliza mhusika maswali kama haya..
 
Sema kuna baadh ya vitu wala sio ajend ila CCM ndo wanafany kuwa ajend Kwan kuwa Acha Tu kuja kusikiliza kesi kuna shida gan??
 
Back
Top Bottom