Mungu amjalie uponyaji huyu ndugu yetu. Hata tuwe na tofauti za namna gani, tusifurahie kifo cha binadaamu mwenzetu.
Tukiamini mtu ametukosea tumwombee maisha marefu ya kujutia ubaya wake, na kisha amgeukie Mungu wa haki.
Tufurahie mdhulumaji wa haki mmoja anapodilika na kuwa mtu wa haki kuliko wenye haki wa wakati wote 100.
Najua wengi wamejenga chuki dhidi ya watawala kutokana na ushetani uliofanyika kwenye uchaguzi wa 2020. Ni kweli ulikuwa ni ushetani wa hali ya juu, waliiba kura, waliwatesa wapinzani, waliwaengua na sehemu nyingine mpaka waliua. Ulikuwa ni ushetani wa hali ya juu. Na bado wanaendelea kujivunia ushindi wa shetani. Tusiwachukie bali tuwakumbushe uovu wao, wapatwe na hekima ya Mungu, wajutie, na siku moja wakawe mbele katika kutafuta na kuilinda haki.