Dkt. Philip Mpango: Mimi ni mzima, walionizushia kifo nimewasamehe

Dkt. Philip Mpango: Mimi ni mzima, walionizushia kifo nimewasamehe

Katika kuuaga mwili wa Balozi John Kijazi Karemjee, Rais Magufuli amesoma hadharani ujumbe mfupi wa simu aliyotumiwa na Waziri Mpango akimjulisha Rais juu ya Afya yake.

Nukuu

''Mheshimiwa Rais asante nimepata ujumbe wako kupitia kwa mke wangu, kwa Neema ya Mungu naendelea vizuri, nakula na ninafanya mazoezi ya kifua, wanaonizushia kifo niliwaombea msamaha kwa Yesu wakati wa sala ya jioni jana

Mheshimiwa Rais, Mungu akubariki na akupe Neema ya ujasiri zaidi katika kuliongoza Taifa letu katika wimbi hili, naungana na wewe na familia katika maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu Balozi kijazi''. - Mwisho wa nukuu


Rais Magufuli amewaonya "walioniua Mpango" huko tweeter.

My Take: Tumuombee Mpango na wagonjwa wengine wote.
Covid -19 bado inatesa Utawala wa Jiwe kwasababu ya kibri chake!!!!
Bado Jiwe halitaki kukiri kuwa Covid-19 ipo na inaua badala yake Jiwe(no feelings) linaendelea kuwalaghai Watz ati ni MATATIZO YA MFUMO KUPUMUA TU....!!!Very shameful.
Hakika Wahenga walisema MFICHA MARADHI MSIBA UTAMWUMBUA...!!
That's what is happening in Tanzania Bara& Visiwani now!!Just call a spade is a spade not a big spoon...!!!
God bless Tanzania n' her people.
 
Mungu ni mwema!
Kumbe ukiwa ICU na very Critical Madaktari wanaweza Kukuruhusu Uchati mpaka hata utume na Viimoji? Kuna Mtu Kachati na House Boy wa Mr. Plan anatutambia Watanzania kuwa ni Yeye. Walikuwa wanatuficha kuwa Mr. Plan haugui Sasa mbona leo Wamekiri Kwetu kuwa anaumwa kweli? Wanafiki Wakubwa nyie ( wao )
 
Hata kama corona ipo , rais hakisema haipo yuko sawa, msiwape wananchi taharuki mpaka wanaogopa kutoka nje
Mbona magonjwa mengine huko nyuma yalitangazwa na watu waliendelea na shughuli zao bila taharuki? Ni kwamba kwa sasa watanzania wekuwa watoto hivyo watapata taharuki? Wasipate taharuki kwa ccm kuiba kura wapate taharuki kwa ugonjwa ulioko dunia nzima?
 
Ukiwa na akili timamu unatakiwa ujiulize, kwanini watanzania tumeanza kuombea vifo na mabaya mengine ilihali haikuwa utamaduni wetu? nani amefufikisha kwenye hii hali mbaya ya chuki na visasi? jibu ni moja tu kuna kundi la wachache wanajiona wao ndiyo wenye hati miliki na nchi hiii na wengine ni waimbiki, mtawala unapokuwa mbaguzi matokeo yake ndiyo haya ya chuki na visasi. Kiongozi ni kuonyesha njia na siyo kuwa mbaguzi wa namna yoyote ile.
Usiseme watz, sema chadema
 
Katika kuuaga mwili wa Balozi John Kijazi Karemjee, Rais Magufuli amesoma hadharani ujumbe mfupi wa simu aliyotumiwa na Waziri Mpango akimjulisha Rais juu ya Afya yake.

Nukuu

''Mheshimiwa Rais asante nimepata ujumbe wako kupitia kwa mke wangu, kwa Neema ya Mungu naendelea vizuri, nakula na ninafanya mazoezi ya kifua, wanaonizushia kifo niliwaombea msamaha kwa Yesu wakati wa sala ya jioni jana

Mheshimiwa Rais, Mungu akubariki na akupe Neema ya ujasiri zaidi katika kuliongoza Taifa letu katika wimbi hili, naungana na wewe na familia katika maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu Balozi kijazi''. - Mwisho wa nukuu


Rais Magufuli amewaonya "walioniua Mpango" huko tweeter.

My Take: Tumuombee Mpango na wagonjwa wengine wote.


Lakini kakubali kuwa anaumwa tatizo la kupumua na anafanya mazoezi! tatizo ni uwazi. Hivyo anaumwa Corona huo ndiyo ukweli
 
Acha wacheze huyu mdudu atabeba mtu mkubwa hapo juu.
 
Unajua hata mtu akikaribia kufa huwa anatiaga matumaini!!yaani unaweza kuta kalazwa alafu unaenda kumtembelea unapigia ndugu wengine simu mgonjwa anazungumza nao mwanzo mwisho na kicheko juu lakini baada ya mda mnakuja ambiwa kashapoteza ramani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..Dr.Mpango ni mzima kwa maana hajafa.

..lakini ni mgonjwa na ndio maana ili kuwasiliana naye inabidi utume ujumbe kwa mke wake.
 
Back
Top Bottom