Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Amevuka hizi wiki mbili mlizomzushia kifo.

Ni kweli, japo alishuhudia wapinzani wakiuliwa na kupewa vilema ili ccm ikae madarakani kwa shuruti. Bora yeye kazuishiwa vifo, wapinzani wameuwawa kabisa ili ccm itangazwe washindi.
 
Mbona bado mgonjwa?? Tens sana tu! Iko wazi kwamba hao walioko pembeni yake wako hatarini, maana anakohoa tu uncontrollably!! hivi sisi huwa tunatumia nini kufirikiri?? hata tu mask ,, kama act of kindness (kulinda wengine)?? politics, na uchoyo!
 
Hawa ndio PhD holder tulio nao Tanzania.

Sishangai Msukuma anavyo watukana bungeni na wao kushangilia wakati wana tukanwa...
Hivi wengi inawezekana hamjui hiyo hapo mkononi mwake ni IV line ya kuwekewa dawa. Sasa kama mtu ana IV line maana yake ni kwamba bado anapata matibabu na Mpango bado ana IV line mkononi.
 
Amerudi KUCHAPA KAZI Kama alivodai
Back to ICU
Sijui kwanini hakujionea huruma! Alikuwa anaongea huku anahema juu juu ili TU kumfurahisha mkuu. Too bad

Mungu amsimamie apone.

Haikupaswa kutusuta walimwengu kabla hajapona vizuri.
 
Ni kweli, japo alishuhudia wapinzani wakiuliwa na kupewa vilema ili ccm ikae madarakani kwa shuruti. Bora yeye kazuishiwa vifo, wapinzani wameuwawa kabisa ili ccm itangazwe washindi.
Hii imekaa sawa? Inaingia vipi?
 
Mkuu umeongea NENO...
 
Sijui nini kinaendelea katika dunia hii ya Tanzania? Kuna ulazima gani huyu mzee wa watu kuzungumzishwa katika vyombo vya habari. Kuna jambo linatafutwa. Bado mgonjwa huyu saa 48 ni chache sana.
 
Kama tumefika huku, basi tumepoteza muelekeo kama nchi. Maana hii ni hatari sana, huyu mh bado anaumwa haikuwa sahihi kabisa kumleta kwenye vyombo vya habari. Hata kama tunataka kuwaonyesha "mabeberu" kwamba maombi yamejibiwa lakini huyu mh bado anahitaji muda.
Daktari anae simamia matibabu yake ilitakiwa awajibike kwa kuhatarisha maisha ya mgonjwa anae mtibu.
Kwa sababu anafahamu kwamba mh alikuwa anatumia mtungi (oxygen) kumsaidia kupumua, hii maana yake ni kwamba wasiojulikana wameharibu mapafu hali inayopelekea mtu kupata tatizo la changamoto ya upumuaji.
Ikifikia mtu akiwekewa mtungi (oxygen) ina maana kati ya asilimia 1 adi 30 ya mapafu yake imeathirika, na hata kama wasiojulikana wametoka/wamedhibitiwa lakini ile athari/uharibifu waliofanya haindoki nao pamoja. Hivyo mgonjwa bado anahitaji uangalizi wa hali ya juu badala yakumuhangaisha kwenye vyombo vya habari.
Ndio maana mabeberu baada ya kugundua athari zinazo achwa na wasiojulikana hasa kwa wale waliofikia kutumia mtungi (oxygen) wameamua kuanza kinga kwa wazee, lengo lao sio kwamba wakipata maambukizi watakufa, bali lengo nikuwahi kuwalinda wasihathirike. Maana hata wakipona kwa wasiojulikana lakini athari zake mtu anaweza kuhitaji huduma ya mapafu katika uhai wake wote ulio baki, na athari zinazoachwa na wasiojulikana hazimo kwenye mifumo ya bima, ni jukumu la serikali kupitia mpango wa dharura na kwa kuwa gharama yakumtibu mtu mmoja kwa mwaka mzima ni kubwa kuliko gharama inayotokana na vifo vya watu 10 kwa mwaka mzima ndio maana wanamuangalia mtu kwa ukaribu zaidi adi afya yake kuimarika badala ya kumkimbiza kwenye vyombo vya habari.
Hivyo waliofanya ama kushirikiana na mh kufanya maamuzi yakuzungumza na vyombo vya habari na daktari wake kuruhusu hilo, wote kwa pamoja wamefanya jambo ambalo ni hatari sana kwa afya yake na ni hatari pia kwa taifa kutokana na nafasi yake.
 
sasa hao walio hapo pembeni ... duuuuuh Mungu awasaidie. Pole mzee wetu Mpango. Mungu aendelee kukupigania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…