Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Jambo la kheri ni kwamba anapata nafuu, nafurahi kuona na kusikia hivyo japo ningefurahi zaidi kama angetahadharisha kuhusu COVID ili wengine nao wachukue tahadhari, angalau ushuhuda wake ingesaidia wengi.

Suala ninaloliona hapa ni kwamba ukimsikiliza sana Dr. Mpango ni kama anasisitiza zaidi tiba ya (Kisayansi) hospitalini japo anagusia gusia mambo ya vyungu, all in all ndugu zangu, tuchukue tahadhari, hatujui mpango kaawacha wangapi bado wapo kwenye mitungi hapo hospitalini, tuwaombee wapone maisha yaendelee.
 
Kwani kuna Corona au anataka tu kumuumbua boss wake. anyway i just wish him a very quick recovery.! Tunaamini atakuwa balozi mzuri kwa wanaobeza kuwa tatizo la corona halipo nchini
 
Kumbe alikuwa anaumwa kweli? Nilijua mijamaa ilikuwa inazusha tu.

Mshukuru sana Mungu, usije ukakufuru ukamshukuru yule jamaa yetu kama walivyofanya wale vigogo wa Pentekoste.
Aisee!
 
Bado anaongea kwa taabu, sijui kwanini wamemruhusu kuongea na waandishi.

Ameongea kwa huzuni sana kuhusu waliofariki, nimeona kama machozi yamemlenga lenga.
Tatizo lilikukuta ndiyo utajua ugumu wake lakini bila hivyo watabakia kushabikia tu
 
Kwani alipatwa na nini? Mbona mafumbo mafumbo?
 
Hayo yote ni bure bila msaada wa Mungu.

Nae amesisitiza Mungu kamponya, wangapi kwan wanafia mhimbili au India!!?
 
Waafrica hawajaizingatia corona
In short Corona Africa imepotea njia
 
ukiumwa usiiingie mitandao ya kijamii kuna mapepo kazi yao kukuombea kifo.
 
Hizi siasa hatari sana mtu ulikuwa ICU kwenye koma situation siku unachomolewa oxygen unatoka mkuku kwenda kuongea na media bila hata kupumzisha misuli ili tu ku prove mtu wrong.
Mpango anawapenda watanzania,anataka kyshare nanyi exprience,,that is why?
 
Nimefurahi hapo kwenye"Nitamshauri mh.Rais tuboreshe vya kwetu"
 
Duu! Kwa hiyo kila mtu anatakiwa anunue mtungi wake wa oxygen kwa kujihami?
Hivi hiyo mitungi inauzwa pesa ngapi mkubwa,halafu kumbe asingekuwa na mtungi wake wa oxygen sasa hivi angekuwa anacheza karata na akina Kijazi huko kuzimu kwa waiba kura
 
Hivi hiyo mitungi inauzwa pesa ngapi mkubwa,halafu kumbe asingekuwa na mtungi wake wa oxygen sasa hivi angekuwa anacheza karata na akina Kijazi huko kuzimu kwa waiba kura
Una roho ya kichawi.
 
Baada ya kushindwa kuficha korona sasa wagonjwa wanaandaliwa press conference. Ila watanzania.wenye utimamu wameshajielewa, hata viongozi wa dini hawapo upande wa waficha maradhi. Failed leadership
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…