Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Dkt. Philip Mpango: Narudi kuchapa kazi, Mungu amenivusha. Leo siku ya 3 sijatumia mtungi wa Oxygen

Hongera ...haya njoo sasa utangaze kwamba Corona ipo nchini na ni tishio!!
 
Kuna ulazima gani wa kujitangazia afya yako Kama hakulazomishwa kuutangazia umma Basi kafanya kosa kubwa sana
 
Huyu jamaa bado anaonekana mdhaifu asijikaze kisabuni yakatokea ya kutokea, badala ya kufanya press conference angetumia muda huo kupumzika ili aimarike zaidi
 
Pole yake sana...

Asifanye kazi ngumu ngumu kwa kipindi kirefu kidogo...
 
Hivi ukiwa kwenye oxygen unaweza kuandika na kutuma meseji? Maana kama leo ni siku ya tatu ndio hajatumia oxygen, ile meseji tulisomewa wiki iliyopita ilitoka wapi?
 
Waziri wa fedha na mipango Dkt. Philp Mpango amesema anarudi kuchapa kazi baada ya mkono wa Mungu kumvusha na ugonjwa uliomkumba mpaka akalazwa.

Waziri Mpango amesema haya (Nukuu) - Narudi kazini na kazi ndogondogo nimekwishaanza za kulitumikia Taifa. Watanzania tuendelee kumwomba Mungu kwa kila mmoja na imani yake na atatuvusha. Amenivusha mimi na wengine ninaowaacha hapa atawavusha.

Nilikuwa nafungua mitandao, ni mambo ya ajabu sana. Nimeonja upendo mkubwa sana kwa wananchi wa Tanzania na wananchi wenzangu wa Buhigwe, wawe na amani na muda si mrefu nitakwenda kuwatembelea

Madaktari, manesi, wataalamu wa viungo, mpaka wahudumu nawashukuru sana kwa huduma nzuri mlizonipa katika kipindi chote. Ni vijana lakini wanafanya kazi kubwa sana"

Natoa pole sana kwa familia zilizopoteza wapendwa kwa wiki mbili nilizokuwa hapa na nyumbani. Ningeshiriki msiba wa Maalim Seif, Balozi John Kijazi na jana nimempoteza mwalimu wangu wa pekee, Profesa Benno Ndulu na mdogo wangu Atashasta Nditiye"

Kulikuwa na vishawishi, hamia Dar es Salaam, hamia huku nikasema hapana, hospitali ni nzuri kabisa na wataalamu walioiva. Sababu ya kukimbilia Ulaya, haipo. Tuboreshe vya kwetu na kwa nafasi aliyonipa Rais, nitamshauri kuboresha zaidi



Ikumbukwe watu wasio wema walizua taarifa za uongo kuwa amefariki baada ya kulazwa. Na tarifa hizo za uongo zilidai amefariki kwa ugonjwa wa Covid 19.

Dkt. Mpango alituma sms kwa mkuu wa nchi yetu kuwa amewasamehe waliomzushia uongo kuwa amekufa.Sasa wakimuona sijui watajisikia vipi. Aibu kubwa kwa wanafiki. Zaidi soma Dkt. Philip Mpango: Mimi ni mzima, walionizushia kifo nimewasamehe
Kama leo ni siku yake ya tatu tangu atoke kwenye oxygen machine hii maana yake ni nini? Maana yake ni either rais alitudanganya kwamba ali chat naye au alikua akichat naye akiwa under intensive care huku akiwa kwenye oxygen machine
 
Kwani lazima avae?
..kama anajijua ameugua corona ni busara na uungwana kuvaa barakoa.

..pia inashauriwa kuziba kinywa kila anapokohoa au kupiga chafya ili asisambaze maambukizi.

..bahati mbaya sikuona Dr.Mpango akizingatia hayo wakati wa press conference.

..kibaya zaidi Dr.Mpango alikwenda kushikana mikono na wauguzi na madaktari baada ya press conference.
 
Back
Top Bottom