Dkt. Slaa: Wapo viongozi walichaguliwa kwa uchaguzi unaopatikana Tanzania tu

Ndio mwisho wa kuwaza kwako? Kwa hio kila anaye toa maoni tofauti anataka asali? Watanzania milion 60 tunapaswa kuwaza sawa?
Kuna watanzania wajinga sana aisee. Sijui wapewe elimu gani wajitambue Slaa kasema ukweli.
 
Wewe na mfano wako ni vitu vya kupuuzwa
 
Nakumbuka kabla Devotha Minja wa Chadema hajachachamaa Wagombea wote wa CCM walipitishwa bila kupingwa mkoani Morogoro

Baadae ikaamuliwa Morogoro mjini Uchaguzi Ufanyike

Labda ndio sababu Wabunge wa Morogoro wamedoda bungeni tofauti na Enzi za akina Jay wa Mitulinga, Suzan Kiwanga, Devotha Minja, Lijualikali nk

Ila kuwawakilisha Watu kwa lazima ni Dhambi kubwa sana!
 
Naona mna attack mtoa mada na kuacha mada
Tukubali kuwa kwenye siasa, au masuala ya kimkakati vyote vinaweza kuwa “suala”. Tena ukiwa maarufu kama Dr Slaa, unakuwa sehemu “context” - mazingira - ya unachosema. Lazima vyote vipimwe kwa pamoja ili uzito wake uthaminiwe. Jus’ for the sake of credibility.

Alichosema ni sahihi kabisa kwa mujibu wa katiba tena ni “obvious” kabisa kwa mtu mwenye kusimama kwenye ukweli. Huyu Dr. alikuwa upande wa waliodai kuwa uchaguzi wa 2020 ulikuwa safi na serikali ile ilikuwa njema sana - Majaliwa akiwemo. Hiyo inampotezea hadhi ya kuwa “quoted” kuhusu ubatili wa kina Majaliwa. Mada inaweza kujisimamia bila jina lake. Ndio maana anakuwa sehemu ya mjadala.

Ni kama kumnukuu Kim Jong Un akipigia chapuo faida za utawala wa kidemokrasia na haki za binadamu! Hapo, yeye ndiye atageuka kuwa hoja 100% badala ya anachokisema - ambacho ni obvious! Haitashangaza wadau wakihisi kawehuka au katekwa na CIA au hata karogwa!
 
Yapo mengi batili nchi hii.
 
hilo halina ubishi, na tunaamini halitakiwi kujirudia tena. though najua waarabu sasaivi watamwaga sana pesa za uchaguzi manake sisiemu ndio kinga yao kwenye huo mkataba wa ajabu. tuna safari ndefu sana.
 
Dkt Slaa anataka uteuzi akipewa anatulia, basi apewe uenyekiti wa bodi katika moja ya taasis za serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…