Na ni bora umeandika Allah anajua zaidi umetokea hapo. Vinginevyo unahitaji kujifunza dini zaidi na zaidi kuna vitu vingi hujui, japo alhamdulillah kwa iliyonayo ili kabla kupinga jifunze zaidi.
Huyo Sule huwezi kumpangua kwa hoja na kwambia wewe hapa umeonyesha kumdharau lakini kahifadhi Quran nzima moyoni na kichwani pia kahifadhi biblia nzima kichwani iweje umbeze jana kwamba hana kitu? Acha kabisa hilo
Kuhusu majini Dkt Sule yuko sahihi Kama muislam ana elimu kuhusu nayo pasi na kumshirikisha Allah basi anaweza kufanya nayo kazi kwani Nabii Suleiman majini na binadamu ndio waliojenga hekalu alikua akiwasimamia na alikua na akiwapangia kazi mbalimbali kwa jinsi anavyotaka na Allah ametwambia Nabii hakukufuru.
Aya nitakuwekea inshaallah
Hakuna sehemu nimemdharau kama ipo unaweza kuonesha kila neno langu nimeweka na dalili na ningependa uweke pia .
Kingine kuhifadhi quran anayepanga ni Allah (the almighty) kuna waarabu licha ya kuzaliwa wakiwa na uwepesi wa lugha ila hawajahifadhi quran lakini pia alhamdulillah kuna wasio waarabu lakini wameihifadhi quran aya kwa aya , herufi kwa herufi, qira'at kwa qira'at hivyo anayefanya wepesi wa mtu kuhifadhi ni Allah (the all knowing).
Kuhusu biblia ninaweza kukutajia waislamu waliohifadhi na wakahifadhi zaidi ya hayo na hakuna hata siku moja waliwahi kuongea kitu bila ya dalili maana wanajua bila ya dalili ni kupotea kama hadith ya sahih muslim 2673(niliyokuwekea comment uliyo quote) inavyotueleza .kwa kukutajia wachache.
1. Ahmed deedat ,da'ai (alihifadhi quran na biblia kwa version zote unazozijua wewe ) ni mwalimu wa zakir naik na mwaka 1984 aliwahi kumpa challenge pope john paul II waende mdahalo kuhusu dini ipi ni ya haki kupitia dalili za vitabu vya dini vyenywe pope alikataa challenge hiyo , huyu mtu Allah (the almighty) alimjalia kipaji kana kwamba aliwahi kwenda mdahalo na miamba wa dini ya kikristo enzi hizo watu wakubwa waliokuwa na mega churches na wana elimu ya ukristo pengine kuzidi hata viongozi wa miaka hii ya sasa mfano dr. Anis shorosh, josh mcdowell, eric bock na wengineo wengi tu na woote hao aliwashinda kwa hoja sahih (bi idhnillah).
2. Zakir naik ,da'ai (kwanza ni daktari wa magonjwa ya binadamu, amehifadhi quran, baghavad jita, bagavad purana, upanishad, biblia, na pia ana ufahamu kuhusiana na field kadhaa za kisayansi).
3. yusuf estes huyu kabla ya kuslimu alikuwa ni full fleged catholic student biblia haumwambii kitu na ni hafidh pia wa quran.
Sule unayemuongelea sidhani kama aliwahi hata kwenda mdahalo na Mwamposa , kakobe et al zaidi anao battle nao ni wakristo ambao hawana base kubwa ya wafuasi na hawatambuliki hoja zenyewe za biblia anazotoa ni very common hana uwezo wa kuichambua kwa level za hao wasomi hapo juu na ndiyo maana huwa midhalo mingi inaisha kwa sintofahamu and i doubt kama amehifadhi biblia yote anyway.
hoja yako ya nabii sulaiman (peace be upon him) unayoongelea haina mashiko laba uwe haujaelewa iyo aya uliyoiweka ya surat baqara aya ya 102 ukitaka kuielewa soma aya ya 101 sura hiyo hiyo al baqara .
Sulaiman alikuwa mtume na aliwahi kumuomba Allah (the almighty) ampe ufalme wa duniani ambao hatokuja kupewa yeyote baada yake na Allah( the almighty) akampa ufalme juu ya vilivyomo duniani watu, majini , wanyama , upepo n.k ushahidi ni sura ya 38 aya ya 35 hadi ya 37 (surat sad) nanukuu
Sad 38:35
قَالَ رَبِّ ٱغْفِرْ لِى وَهَبْ لِى مُلْكًا لَّا يَنۢبَغِى لِأَحَدٍ مِّنۢ بَعْدِىٓۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Akasema: Mola wangu Mlezi! Nisamehe na unipe ufalme usio mwelekea yeyote baada yangu. Hakika Wewe ndiye Mpaji.
Sad 38:36
فَسَخَّرْنَا لَهُ ٱلرِّيحَ تَجْرِى بِأَمْرِهِۦ رُخَآءً حَيْثُ أَصَابَ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Basi tukaufanya upepo umtumikie, ukenda kwa amri yake, popote alipo taka kufika.
English - Tafsir Ibn Kathir (Abridged)
Sad 38:37
وَٱلشَّيَٰطِينَ كُلَّ بَنَّآءٍ وَغَوَّاصٍ
Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani
Na tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi.
English - Tafsir Ibn Kathir (Abridged)
sidhani kama kunahitaji maelezi zaidi hapo , na kuhusu kuwepo na elimu ya kuyaamrisha majini kwenye uislamu hili napingana nalo kama una dalili tafadhal weka na isiwe nje ya quran na suna maana sitohangaika nayo na kama una muda hebu muulize huyo dr sule kama ana dalili pia kuhusiana na hayo aliyoyasema .
NA ALLAH(THE ALL KNOWING) ANAJUA ZAIDI