Tunaangamia kwakukosa maharifa..!!
MUNGU NI NGUVU YA AJABU SANA.
Sifa zote za Mungu (hiyo Nguvu) anazo/yo Mwanadamu mwenye JInsia Yeyote ile, hivyo kila mtu anaweza kutumia taswira ya Nguvu ya Kimungu na kuipa Jinsia kwa kadri aiaminivyo katika kuamini kwake..
Mfano panapokua na hatari au magumu Tutamuomba Mungu atuvushe< hapo tunamtazama kama mwenye nguvu ambapo tutamfananisha na mwanaume, na inapotokea kuna tatizo lihitajilo ffaraja na msamaaha tutaipata taswira ya Mungu kama mama mwenye huruma ya kweli..
hivyo basi mazingira na hali ndizo zitatupa taswira ya kijinsia ya Nguvu Ya Mungu kutokana na lipi linahitajika kushinda majaribu vikwazo na matatizo.
Sifa Ya Mungu amabayo mwanadamu hana ni ile NGUVU tu inayoweza kubadilisha hali fulani kuwa nyingine bila kujua ni kivipi inatokea, lakini Sifa nyingine zooote alizonazo Mungu, tunazishuhudia kwa sisis wanadamu wenyewe, na hapo ndipo naipata maana ya kusema TUMEUMBWA KWA MFANO WAKE na sio KWA MFANANO WAKE.
Kwa mfano.. Ni nani anaweza kutoa ushuhuda wa kumkosea mwanadamu mwenzake na akamuomba Mungu faragha na akabaki na Amani?
Mungu ni mwenye;
Hasira
Huruma
Upendo
Haki
Kusamehe
kuhukumu
Tukimuomba yeye anatupa, tukibisha hodi anafungua, tukitafuta tunapata.
Binafsi naona sifa zote zinapatikana katika sisi wanadamu, hivyo tukichukuliana kama wawakilishi wa sifa za Nguvu za Mungu maisha yetu yatakua ni bora na yenye kumpendeza kila mmoja alie hai maana Nguvu za Mungu zitakua ndani ya nguvu zetu za kibinaadamu na tutaweza kutendeana yote tunayoamini ni Mungu tusiyeweza kuja kumjua kua ndie mtendaji wakati huo huo tukiwa na ushahidi wa matendo yote tutendeanayo tunafurahishana, tunachukizana, tunasameheana ama tunahukumiana sisi kwa sisi wanadamu na Mungu hausiki kabisa maana sifa alizonazo mwanadamu anazo.
So yeyote atumiaye jinsia yeyote kuwakilisha nguvu ya Mungu yupo sahihi.
Asante!