Dodoma: Naibu Waziri wa TAMISEMI Festo Dugange apata ajali akiendesha gari
Huko UK, miaka ya zamani kidogo, Waziri mdogo, alikutwa na kashfa ya uzinzi, yaani kutembea na hawara zake, UK PM wa wakati huo, alimteua mtu mwingine right away, hata hajamjulisha na kazi yake ikawa ndio basi, Waziri mdogo akawa kajifukuzisha kazi kwa aibu kubwa.

Waziri mzima unakosa maadili au unashindwa kuficha siri zako tena nyeti kabisa, sasa siri za serikali si ndio hata hawezi kuficha hata kidogo, mimi ningekuwa Mh. Rais nachagua tu mtu mwingine paaap, ndio imeisha hiyo.
Magu au jk ndo angefanya hvo mama amejawa na huruma katu jawezi mpiga chini.
 
JESHI LA POLISI limetoa ufafanuzi kuhusu ajali ya iliyomhusisha Naibu Waziri wa TAMISEMI DR FESTO DUGANGE mnamo tarehe 26/04/2023 katika barabara ya lyumbu maeneo ya ST.PETER CLEVER wilaya na jiji la Dodoma iliyohusisha gari namba T454 DWV aina ya Toyota Land cruiser iliyokuwa ikiendeshwa na DKT DUGANGE.

Katika ajali hiyo DKT FESTO DUGANGE alikuwa peke yake na yeye ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo. Ajali ilitokea wakati akijaribu kumkwepa Bodaboba aliyevuka barabara ghafla bila ya kuchukua tahadhari. Kitendo ambacho kilipelekea gari hilo kugonga kingo ya barabara na kupinduka.

DKT DUGANGE alivunjika kidole gumba cha mkono wa kulia na kupata majeraha katika mkono huo na amelazwa katika Hospitali ya Benjamini Mkapa akiendelea kupatiwa matibabu na Afya yake inaendelea kuimarika.

Kumekuwa na taarifa za uzushi na upotoshaji katika mitandao ya kijamii kwamba katika ajali hiyo kulikuwa na Mwanamke ambaye majina yake hayafahamiki na kwamba alifariki katika ajali hiyo na pia kudai kwamba ajali hiyo ilihusisha gari ambalo ni mali ya Serikali.

Jeshi la Polisi limesema taarifa hizo zipuuzwe kwani ni za uongo na upotoshaji. Gari lililohusika katika ajali hiyo ni Mali ya Dkt Dugange na alikuwa peke yake katika gari hilo na yeye ndiye alikuwa dereva wa gari hilo.

Jeshi la Polisi linatoa rai kwa wananchi kuacha kusambaza taarifa za uongo na kuzua taharuki kwa watu bila ya kufanyia utafiti taarifa hizo kabla ya kuzisambaza katika mitandao ya kijamii na kubainisha kuwa lipo macho na makini kufuatilia na kutoa ufafanuzi wa taarifa zozote hivyo wananchi wasisite kufika Polisi na kupata ufafanuzi wa taarifa zozote mnazotilia mashaka.
 
Screenshot_20230430-081345.jpg
 
Hii issue ukiitazama kwa makini naona kuna kitu serikali inaficha, na sijui wanafanya hivyo kwa manufaa ya nani.

Kama mtu kakosea awajibishwe lakini kumuacha ni sawa na kulea uozo kwa watendaji wa serikali, au labda wanasubiri atoke hospitali ndio hatua nyingine zifuate..
 
Polisi wametoa taarifa kuwa Naibu Waziri mh Dugange alipata ajali akiwa Peke yake na alikuwa akiendesha gari binafsi siyo ya Serikal
Chanzo cha ajali ni Bodaboda iliyoingia ghafla barabarani

Aidha ajali nyingine ilitokea Kongwa ambayo ilihusisha gari la ofisi ya Makamu wa Rais lililogongana na lori na kuuwa Watu wawili na majeruhi mmoja

Chanzo: Jambo tv
 
Polisi wametoa taarifa kuwa Naibu Waziri mh Dugange alipata ajali akiwa Peke yake na alikuwa akiendesha gari binafsi siyo ya Serikal
Chanzo cha ajali ni Bodaboda iliyoingia ghafla barabarani

Aidha ajali nyingine ilitokea Kongwa ambayo ilihusisha gari la ofisi ya Makamu wa Rais lililogongana na lori na kuuwa Watu wawili na majeruhi mmoja

Chanzo: Jambo tv
Twisted ? ....basi sawa pona haraka mjomba
 
Mambosasa Kwenye Sakata La MO Wakati Wa Utawala Wa Mzilankende Alimwambia
Wamemrudisha MO Na Hawajakamatwa Nakwambia Tanzania Siyo Ya Wajinga




Kwenye Hiyo Ajali Najua Watanzania WanAujua Ukweli Wote Muda Sana Walikuwa Wanashindwa Kusema Chochote Mpaka Walipopika Data Ndiyo Wanakuja Hadharani
 
Back
Top Bottom