Ndalichako alikua best student enz zake huko sekondari...yaan Tanzania one...shaur yako.
Napata tabu sana na huyu mama ata bachelor yake ni hesabu watu wachache wenye uwezo wa kufanya hiyo degree, she is supposed to be very clever.

Lakini ukimsikiliza dah
 
Can you imagine anachokifanya ni kosa la jinai ...anawa insight wananchi dhidi ya viongozi wa serikali.. anawaambia wasiwatii mawaziri na maafisa wa serikali wanaokaa maofisini na kutembelea magari yenye AC ( tofauti na yeye anayetembelea Punda.) Last time I checked ata bosi wake wa Tamisemi, waziri mkuu na Rais wote Wana office na gari zao zina AC pia...Mtaka kakosea Sana no matter what people say.. sijawahi kuona kiongozi mkubwa wa serikali akiwahamasisha wananchi kuwadharau viongozi wa kitaifa Kwa kuwasema maisha Yao binafsi..if he stays then waziri wa elimu na Tamisemi should resign otherwise tabia hii itaendelea ambapo kila mkuu wa Mkoa ataamua kuwaambia wananchi wasiwasikilize mawaziri,and then waziri mkuu au Rais .. baadae wao ma RC ndio watakua Bosi kubwa wa mikoa.. mawaziri watakosa sehemu za kutawala na eventually anayewateua...kama angekua na wazo tofauti na Waziri angeshauri Kwa staha tofauti na alivyofanya ... implication ya alichosema ni kubwa Sana..Ila naona watu wanaichukulia poa... alichosema ni Sawa na mkuu wa JKT awaambie vijana wasimsikilize Mnadhimu au CDF Kwa sababu wao wanakaa tuu ofisini upanga wanakula kiyoyozi na watoto wao hawaendi Kambi za JKT na kukaa field kama wao.
 
Waziri anayo mamlaka ya kuamua utaratibu wa wanafunzi kuingia, kutoka, kula, uniform n.k katika shule za Kongwa, Kibaigwa na nyinginezo mkoani Dodoma?
Amejiharibia sana huyu, hajaweza kudhibiti ulimi wake, yawezekana nia yake ni njema lakini hajatumia diplomasia kumnanga kiongozi mwenzake jukwaanni
 
Yule mama wa kawaida sana
Ni mwalimu wangu mzuri mno amenifundisha Educational Statistics wakati nasoma undergraduate, na anaijua kuliko kawaida.

Wanawake wa Kigoma kwa ujumla hawana majivuno ni wakarimu, wana nidhamu ya hali ya juu mno tena ile natural. Nimekaa Kigoma mwaka mzima nawajua mno hawa watu. Nasikitika sana kwa kilichotokea. Huyu mama inabidi amsamehe tu Mh. Mkuu wa Mkoa ameteleza kidogo katika ule ubinadamu wa kawaida tu

Lakini na nyie mitandao sasa msiendelee kuweka kuni kwenye moto
 
safi sana
 
Hili Taifa letu vijana tunakwama wapi? Kwanini tunashindwa kuwaza mambo kwa mapana? Vijana mnababaishwa na hayo majina ya mwanzo yaani Proofesa...., Binafsi naendelea kumuomba mama yetu SAMIA apokee ombi la kusafisha wizara hii. Huyu mama ni nshida ...tizama kipindi kile alivyowadharirisha kina Msonde pamoja Mgaya.....Wizara haina mtendaji, Mama safisha wizara hii.
 
Mzee ..elimu ya darasani tofautisha kabisa na uhalisi ulipo kule nje..... uNAZUNGUMZA SIJUI UNAJUA HILO? AU NDIYO WALE MNAOITIKIA NDIYO MZEE!
 
Ndalichako ni waziri wa JF na sisi ndio tuliopiga kelele apewe wizara msisahau.
 
Syllabus ipo, Work plan ipo, huhitaji kukaa hadi saa 10.

Sheria inataka mwalimu asilazimishwe kukaa overtime na hata akikubali alipwe overtime.

Sasa umlipe overtime wakati mshahara tu mbinde.
Umemsikiliza RC lakini? Nini maana ya wazazi na waalimu wakubaliane?
 
Sasa ni rasmi nakubaliana kabisa na woote wanakataa kiongozi yeyote kukaa akisifiwa sifiwa, iwe katika kutekeleza majukumu yake, ama katika kutoa mwelekeo wa jambo fulani, sifa zinalevya na kujikuta mtu akiharibu zaidi

Kwa mara ya kwanza, natofautiana na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu bwana Mtaka na sasa ni mkuu wa mkoa wa Doodoma kwa kauli yake aliyoitoa katika kikao chake ima na wazazi ama watoto wa shule huko Dodoma akimshutumu Waziri wa elimu

Mh Mtaka, ni ukweli usiopingika, amekuwa kiongozi anayevutia wengi kwa namna ya uongozi wake na usimamamizi wa mambo, mkuu huyo wa mkoa, amefahamika kwa kasi zaidi kwa namna ya maono makubwa ya kiuongozi aliyonayo, tokea tu alipochaguliwa kuwa mkuu wa mkoa Simiyu miaka mitano iliyopita

Mengi yamefanyika mkoani Simiyu hususani katika nyanja za ki Elimu, Pongezi kwake

Sasa basi, inaonekana dhahili kuwa, Sifa zinapokuwa nyingi, zinatuondolea maarifa na kuanza kujitukuza, na matokeo yake ni kuharibu kazi na sifa zetu njema kwa sababu ya kusifiwa sifiwa,

Sielewi ni kivipi, tunaposifiwa sana huwa inafika mahali tunaanza kuboronga zaidi, Nimesikitishwa na kitendo cha mkuu huyo wa mkoa wa Dodoma, kutoka hadharani kumponda Waziri wake wa Elimu, eti, wananchi wasimsikilize yeye, miongozo yake haufai kusikilizwa na yeyote, akisema angeoenda zaidi asikilizwe yeye kwa kuwa yeye ndiye anakaa nao huko

Kwa kuwasihi zaidi wananchi, alusema, haiwezekani kumsikiliza Waziri, ambapo watoto wake yeye hawasomi shule hizo za kayumba,

Ni sawa, Lakini, Je, wakwake naye wapo kwenye shule hizi za walala hoi?

Lakini unajiuliza, Hasa alikuwa na maana ipi anaposema waziri asisikilizwe? kwamba akionekana mbele za wazai na watoto azomewe kwa sababu watoto wake hawasomi hizo shule!!

Tukienda hivi, hatutafika, tunaondoleana heshima zetu, Je, waziri na mkuu wa mkoa wanaugomvi? kwani kulikuwa na ulazima mkuu wa mkoa kusema mbele ya halaiki kwamba, Waziri hafai kusikilizwa kwa chochote hususani katika suala la Elimu?

Lakini Je, Kama kulikuwa na nashida, kwa nini hawakuwasiliana ili kuondoa sintofahamu kati yao ili tu kusiwepo na mwingiliano kwenye utekerezajai wa majukumu yao,

Mtaka anataka kuwa Makonda? anafanya tu jambo lake bila kuwasiliana na viongozi wake kwa kushauriana?

Mtaka, hana kosa kwa mbinu anazozisuka katika mkoa wake kwa ajiri ya kuboresha Elimu,kosa lake ni kumponda mwingine ili yeye kubeba utukufu usiomstahili na kumfanya mwingine adharaulike
 
Msimsikilize mtoa maada ni BAWACHA/BAVICHA ... aneleta choko-choko 😀
 
Mtaka yupo sahihi kuhusu Kambi zake. Lakini approach ya kumjibu waziri, yaani mteule wa rais hivi kuna mushkeli kidogo. Labda yupo undercover ili kumexpose waziri kurahisisha uamuzi wa mamlaka
Kwa namna alivyoliongelea hilo suala ni kama ana clue fulani ya kutenguliwa kwa waziri ivyo anapigilia msumari.
Kamuaibisha sana waziri,nyumba moja lakini wanagombana hadharani
 
Hata mimi kila siku nawaambia hapa mbona Mtaka ni mtu mwenye maneno matamu naweza kusema ni kama watu wanaomotivate vijana kufanya biashara, huku akijitwika uzalendo ambao bado unamashaka ndani yake. Anamshutumu waziri Ndalichako kwamba watoto wake wanasoma shule international. Yeye Mtaka watoto wake wanasoma shule za day kaka sisi huku mtaani? kama ni kweli sawa, ila kama sio kweli Mtaka ni mnafiki mkubwa. Ajitahidi sana kuwa na weredi kwenye kauli zake maana hata JPM aliyembeba bado alitoa maneno ya shombo kwake. Asiwe mwongeaji sana ajifunze kusikiliza pia. Maana asili ya binadamu ni kujihesabia haki ila mwerevu huchunguza sana mwenendo wake ili asipotee kweye ile kweli.
 
Mkuu,mpango mkakati hata mtu mmoja. Mmoja anatakiwa kuwa nao
Kuweka kambi ni mbinu ya kumfanya mtoto a concentrate kujisomea
 
Mtaka yupo sahihi kuhusu Kambi zake. Lakini approach ya kumjibu waziri, yaani mteule wa rais hivi kuna mushkeli kidogo. Labda yupo undercover ili kumexpose waziri kurahisisha uamuzi wa mamlaka
anajengewa mazingira ya kuchomolewa katika wizara ni swala la muda tu ngoja tusubiri!
 
Hivi Mama Naomi Katunzi yuko wapi? Huyu mama ni hazina kubwa kwa Taifa. Huyu bali na wengine anafaaa kuwa Waziri wa Elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…