Dodoma: RC Antony Mtaka amchana Waziri wa Elimu kuhusu mwisho wa Watoto kusoma kuwa ni saa tisa
Amejiharibia sana huyu, hajaweza kudhibiti ulimi wake, yawezekana nia yake ni njema lakini hajatumia diplomasia kumnanga kiongozi mwenzake jukwaanni
Naamini anayo sababu ya msingi sana mpaka kufikia maamuzi ya kumlipua waziri hadharani.

Hawa mawaziri sometimes wanajikuta tu washakuwa wao ndio wanajua kila kitu
 
Mataka awaasa wananchi wampuuze Waziri wa Elimu kuhusu mambo ya elimu Kwenye mkoa wa Dodoma.

Mataka amesema wampuuze Waziri ambaye watoto wake wanasoma international school.

Sikiliza audio hapo.
Mama Ndali umezoea kuwaonea wakuu wa taasisi za elimu halafu system inakuangalia tu.

View attachment 1851200


Ndalichako ni Waziri wa kawaida sana. Tokea aingie Wizarani ni kufitinisha tu wenzake.

Wakuu wa taasisi wanamkoma huyu Mama. Wakuu wa idara Wizarani wanaipata habari yake.

Ndalichako badilika Mama Samia yupo tofauti na mwendazake.

Hakuna thamani uliyoongeza hapo Wizarani zaidi ya kufitinisha wakurugenzi na mamlaka za uteuzi.

Tabia ya kuwafitinisha wenzako waondolewe kwenye uteuzi acha mara 1.
Ndalichako alishindwa Baraza la Mitihani kwa ubishi wake ilikuwaje apewe Wizara.
Mama Samia tuondolee huyu Ndali
Mkuu wa Mkoa alichafukwa na nini, mbona katoa povu kubwa mbele ya Umma.

Alikosa kutumia lugha ya alama?? Anataja hadi cheo cha anayemkusudia tena mbele ya kadamnasi?

Ujumbe umefika in a hard way. Nlitegemea haya yasemwe na "wapinzani"

Ayway hii ndio inaitwa CALL A SPOON A SPOON
 
Mataka awaasa wananchi wampuuze Waziri wa Elimu kuhusu mambo ya elimu Kwenye mkoa wa Dodoma.

Mataka amesema wampuuze Waziri ambaye watoto wake wanasoma international school.

Sikiliza audio hapo.
Mama Ndali umezoea kuwaonea wakuu wa taasisi za elimu halafu system inakuangalia tu.

View attachment 1851200


Ndalichako ni Waziri wa kawaida sana. Tokea aingie Wizarani ni kufitinisha tu wenzake.

Wakuu wa taasisi wanamkoma huyu Mama. Wakuu wa idara Wizarani wanaipata habari yake.

Ndalichako badilika Mama Samia yupo tofauti na mwendazake.

Hakuna thamani uliyoongeza hapo Wizarani zaidi ya kufitinisha wakurugenzi na mamlaka za uteuzi.

Tabia ya kuwafitinisha wenzako waondolewe kwenye uteuzi acha mara 1.
Ndalichako alishindwa Baraza la Mitihani kwa ubishi wake ilikuwaje apewe Wizara.
Mama Samia tuondolee huyu Ndali
Huyu mtu yuko wazi sana and he is very strong, yaani hafichi hafichi ujumbe. Awe mwangalifu tu kwamba ujumbe wake usije ukamgeuka vibaya. Maana sasa kupingana waziwazi ndani ya Serikali nadhani siyo kitu ambacho hata mamlaka za uteuzi zinaweza kukivumilia
 
Anaweza akawa RC Bora but huwezi kumshambulia personally waziri ambaye ni cabinet member wa serikali ambayo unaiwakilisha hapo mkoani...analeta umbeya eti mtoto wa waziri anasoma international school,anatembelea mbuga za wanyama..vitu vya kuchonganisha tuu...SASA sijui anajua watoto wa PM au Katibu mkuu wanasoma wapi... nilikua namheshimu but Kwa attacks hizi kakosea Sana... waziri yeye anasimamia Sera ambazo nyingi zina Baraka za Baraza la mawaziri ambayo chairman ni Rais na Katibu mkuu ni secretary..Rais wa Zanzibar ni member pia ambaye yeye pamoja na watoto wake hawajawai kukanyaga hizo shule za kata...RC kawasengenya wengi Sana Kwa kujifanya anamsema waziri mmoja AME attack almost the entire government....he has to go..you can't have collectiveness by senior officials attacking others on matter of personal issues in public.
wajuzi watujuze kwanza watoto wa RC mtaka wao wanasoma wapi shule gani anuai....? au kiongozi yeyote cabinet minister , RC au mtunga sera yeyote mwenye kutembelea kiyoyozi au bendera yeye watoto wake wao wanasomea wapi shule gani za kata au serikali msingi na sekondar?
 
Wengine wameajiriwa na serikali lakini sisi raia tunaambiwa tujiajiri mana serikali haina nafasi.

Nasikia Mhe. Joyce Ndalichako ana mtoto mmoja na alifeli chuo, wajuzi ni kweli hayo.?
Mkuu huyo akifeli chuo hafeli maisha maana connections zipo nyingi tu kama JESCA
 
Mtu mwenye Phd ukimsikiliza ata masters tu provided kweli kaisotea na transcript zake zimejaza B’s kwenda juu kuanzia sekondari anapoongea kuna reasonability ya intelligence unaiona.

Siku zote nimekuwa nasema Ndalichako doesn’t add up kama Phd; she is just too shallow ukimsikiliza mara nyingi.
Ndalichako alikua best student enz zake huko sekondari...yaan Tanzania one...shaur yako.
 
Syllabus ipo, Work plan ipo, huhitaji kukaa hadi saa 10.

Sheria inataka mwalimu asilazimishwe kukaa overtime na hata akikubali alipwe overtime.

Sasa umlipe overtime wakati mshahara tu mbinde.


Nchi moja mazingira ya shule yanatofautiana halafu unataka wote wafanye kama yellow buses. Mwisho wa mchezo watoto wetu wanaondoka na mayai viza. Nooooo. Big up RC
 
Wajinga hawa. Mwanafunzi anatakiwa kuelewa kwa muda wa darasani.

Ukiwazoesha waelewe kwa muda wa ziada basi chuo kikuu wataukosa na kazini wanaukosa.

Solution ni kulipa vizuri walimu wawe na moyo wa kufundisha muda wa darasani.


Mnachosha watoto kuwasomesha masaa mengi hivo
 
Achilia mbali overtime, hata salary yenyewe mbinde hadi mwalimu anakosa hela ya kiatu.


Huyo Mtaka anavyotaka watoto waendelee kusoma baada ya muda wa kazi ametetenga fungu la kuwalipa walimu extra time? Tatizo kubwa linaletwa pia na NECTA la rate ufahulu kimkoa hadi wilaya kana kwamba elimu ni madhindano au ligi na kufanya kila kiongozi mteuliwa kutaka ashike nafasi za juu kwa kuwakaririsha manotes wanafunzi au kuiba mitihani.
 
H
Swala la Elimu yetu kufanywa kama mpira wa danadana na kila mmoja kuwa anachezea, ni makosa makubwa sana, mwongozo wa pamoja uko wapi?

Napingana na huyo mkuu wa mkoa wenu pendwa, Inakuweje awe na mpango wa kivyake vyake?

Mkuu wa mkoa wa Songea naye awe na matakwa yake, na wa mikoa mingine, tutakuwa taifa la aina gani?
Hiyo mipango yake ndiyo iliyoipaisha simiyu. Siku wakifeli mtamlalamikia Mkuu wa Mkoa. He's right and he's my support. Go Anthony.
 
Mtaka yupo sahihi kuhusu Kambi zake. Lakini approach ya kumjibu waziri, yaani mteule wa rais hivi kuna mushkeli kidogo. Labda yupo undercover ili kumexpose waziri kurahisisha uamuzi wa mamlaka
Nchi hii inayumba sana kwa sababu ya kuoneana aibu. Anthony has made it. Development is integrated with difference in opinions. Na hakuna kuambiana huko ofisini. Tell it in broad day light. Joyce amemkera sana Anthony I hope. Hata mimi ningemjibu hivyo hivyo zaidi ya Anthony. Watoto wakifeli RC ndiye anasakamwa. Remember, waziri ni policy tu lakini utendaji uko TAMISEMI kwa akina Anthony. Niliwahi kusema kuwa wakuu wa mikoa watakaofanikiwa ni Anthony, Kafulila, and Queen.
 
Ndalichako ni "status quo" na mtaka ni "mlevi wa madaraka" wote wana mazuri yao na mabaya yao, nchi bdo sana hii, tuvumiliane.
 
Back
Top Bottom