..Augustino Mrema naye alijiona ana nguvu sana akatofautiana na msimamo wa serikali, Rais Mwinyi wala hakupoteza muda kumuondoa.

..Huyu asipochukuliwa hatua itajenga mfano mbaya na nidhamu inaweza kutoweka ktk wateule wa Raisi.
 
Mkoa fulani ukifeli analaumiwa Waziri au Mkuu wa Mkoa?.
 
We pingana naye sisi tunaenda naye
 
Umeiweka vizuri
Ujumbe ulikuwa mzuri
Maneno sio
 
Ndio hujawa Samia!
 
Safi Sana Mh MTAKA ,mawaziri wanajikuta Sana ,na kwenye elim wametuvuluga Sana
Mawaziri mara nyingi ni kama hujiamulia baadhi ya mambo, sitasahau JJ Mungai akiwa Waziri wa Elimu walivyoruhusu Physics na Chemistry kuwa somo moja eti wakaliita Phys-Chem.

Sijui walikuwa wanafikiria nini??

Ifikie wakati Elimu isifanyiwe mzaha na Wanasiasa.
 
Mkuu 'MTAZAMO', leo umetoka vizuri sana na kueleweka vyema, at least na mimi kuhusu hayo uliyoandika hapo juu.

Pamoja na kukubaliana na wewe, nakataa hiyo dhana unayoitetea kutokana na mazoea mabaya ambayo tumekwishayashuhudia hapa nchini.

Unalotetea hapa ni kulinda uozo uleule unaoendelea wa kuabudu viongozi hata kama wanafanya mambo ya kipuuzi. Tumefika hatua sasa ya kukataa, hata kama ni hadharani kama alivyofanya Mtaka. Mambo ya kufunikafunika unayoyatetea ndiyo yaliyotufikisha hapa. Unafiki ndio umekuwa sifa ya kuonekana kuwa kiongozi mzuri!.

Ni wakati sasa, kiongozi anayejuwa anakerwa na jambo, aliseme waziwazi, tuondokane na hii tabia mbovu ya kulalamikia pembeni.

Namuunga Mtaka mkono, na kama Samia anachembe yoyote ya uongozi ndani yake, angeanzia hapa kukataa unafiki kwa kumuunga mkono Mkuu wa mkoa wake.
 
[emoji106][emoji106]. Mkoa wa Njombe wana mkakati huo wa kambi toka miaka mingi unaitwa "UWANJO". Msingi wa kambi hizi ni kuwa Wanafunzi ambao ni senior pamoja na walimu wa shule husika husaidiana kuwaanda wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya Form IV.
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na walimu wa shule husika husaidiana kuwaanda wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya Form VI.
Hivyo RC Mtaka yuko sahihi kabisa. Anaanzisha kitu ambacho mikoa mingine kilishaanza miaka mingi iliyopita.
 

..shule ya msingi phys-chem-bio yamechanganywa na kuitwa SAYANSI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…