Kisiasa huyo Mkuu wa mkoa kakosea sana. Alichofanya ni utovu wa nidhamu kwa serikali na Chama Cha Mapinduzi. Sema huyo RC ana nguvu kubwa sana ya umma nyuma yake... kumtumbua kizembe inaweza leta mtikisiko. Waziri angetulia zake na kufanya mambo yanayomhusu. Hii kuingilia hadi watoto wasomeje ni upumbavu kwa hadhi ya waziri.... waziri adili na mambo ya madawati, mitaala, maslahi ya walimu na mambo mengine ngazi ya kitaifa. Kambi za wanafunzi ni jambo dogo mno. Tusubiri uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM (Rais wa JMT) katika hili.
..Augustino Mrema naye alijiona ana nguvu sana akatofautiana na msimamo wa serikali, Rais Mwinyi wala hakupoteza muda kumuondoa.
..Huyu asipochukuliwa hatua itajenga mfano mbaya na nidhamu inaweza kutoweka ktk wateule wa Raisi.