Vile vita vya niwadini yetu kwa huyu Mama Prof tangu akiwa Taasisi ya Tume ya Elimu pale Kijitonyama bado mnaviendeleza. Safari hii mnatumia pandikizi lenu hili.
 
Mtaka yupo sahihi kuhusu Kambi zake. Lakini approach ya kumjibu waziri, yaani mteule wa rais hivi kuna mushkeli kidogo. Labda yupo undercover ili kumexpose waziri kurahisisha uamuzi wa mamlaka
Mkuu huo ndio mgongano wa mamlaka na majukumu ya kazi. Haya ndiyo matatizo ya viongozi kutojua kuwa wanawajibika kwa nani. Wote ni wanasiasa wa Chama kimoja ambao wajibu wao ni kusimamia sera kwenye Serikali ya JAMUHURI YA MUUNGANO WATANZANIA. Aidha SJMT ina Serikali mbili katika mipango yake ya maendeleo, kuna Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, hapa ndipo kuna mwingiliano katika utendaji, inaonekana Serikali Kuu imeimeza Serikali za Mitaa na hadi kupelekea vyazo vyake vya mapato kuchukuliwa na Serikali Kuu, na kupelekea kutotimiza vyema shughuli zake za maendeleo kwenye eneo lake la kimamlaka.

Leo inaonekana Mawaziri na Wakuu wa Mikoa ndio watendaji badala ya kusimamia sera, wanaingilia hata zile shughuli za kiutendaji ambazo zipo chini ya Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala ambao sasa wapo kama watazamaji na baadhi yao kushawishika/kuwaza kuingia katika siasa.

Wizara ya Serikali za Mitaa ndio mwenye jukumu la hizi shule na idara zingine mikoani lakini wapo kimia, hawaonyeshi umakini katika kusimamia shughuli na majukumu ya Serikali za Mitaa.

Baada ya kuzika Azimio la Arusha Wakuu wengi huwapeleka watoto wao kusoma aidha nje ya nchi ama shule za watu binafsi na kuacha kabisa kuwapeleka kwenye shule za Serikali kwa kuwa elimu inayotolewa katika shule hizo wanaamini ni za kiwango cha chini. Ni wakati sasa wa Viongozi Wakuu wa Serikali kuonyesha mfano na UZALENDO WA KWELI KWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE ZA SERIKALI, kwa kufanya hivyo kutaidia sana kuboresha elimu kwenye shule za Serikali maana Wakuu hao watakuwa makini sana katika kujadili maboresho ya elimu wakati wa vikao/mikutano/bungeni maana watakuwa wanajadili sera bora, kwa ubora zaidi ambazo zinazowagusa watoto wa kitanzania na WATOTO WAO.
 
..shule ya msingi phys-chem-bio yamechanganywa na kuitwa SAYANSI.
Afadhali huko Shule za Msingi inaweza kuleta maana, maana huko ni mwendo wa kusoma Kani mbinuo, Lensi, Barehe .

Upande wa Sekondari inakuwa vigumu kwanza kumpata Mwl aliyesoma Physics, Chemistry kama masomo ya kufundishia. Mara nyingi utakuta Mwl anafundisha Physics na Mathematics (Hasa aliyesoma PCM advance) au Chemistry na Biology ( Aliyesoma PCB)

Pia mtu akisoma Phys-Chem atasomaje michepuo ya CBG n.k

Zile zilikuwa Siasa mbaya sana
 
Sio privatezote ni shule za bweni, au unamaanisha hadi shule za kutwa(day) nazo wanasoma hadi usiku?
 
Sasa kuna shida ipi watoto kujibidisha muda zaidi ili wajisomee baada ya masaa ya kawaida ya masomo?.

..Elimu yetu ina MATATIZO makubwa.

..Na SERIKALI ipo njia panda ktk suala hili.

..Je, waziri akiruhusu utaratibu huo ina maana watoto watakuwa hawaendi likizo na hawana ratiba za kujifunza kulingana na muongozo wa kitaalamu?

..Utaratibu wa makambi na jinsi ulivyo maarufu unaonyesha kwamba kuna tatizo ktk UFUNDISHAJI.

..Wanafunzi wangekuwa wanafundishwa inavyopaswa kusingekuwa na ulazima wa kuwa na makambi mengi kiasi hiki nchi nzima.

..Kwenye mataifa ambayo wanatoa elimu ya uhakika wanafunzi wachache ndio huhitaji msaada wa ziada. Lakini kwa hapa kwetu ni kinyume na hivyo.

..Makambi ya kujiaandaa na mitihani ni hatua ya kizimamoto. Tunatakiwa tuka-solve mzizi wa tatizo hili ili wanafunzi wote wapate ELIMU YENYE VIWANGO.
 
Na hiki ndio mimi pia nilitaka kusema. Najua hata huyo mtaka watoto wake pia wanasoma shule nzuri
 
Kiongozi lazima tuanze na maisha yako binafsi, huwezi ukawa unalewa unajikojolea tukakuacha eti sababu unatekeleza majukumu yako vizuri.
Ebu tuambie kwanza kwa Sheria ipi mtu akienda salon au kufanya mapenzi na mtu uliomzidi umri imekuwa kosa? ili Ndalichako awe amefanya kosa
 
Huu uongo mmeutoa wapi? Hiyo nguvu ya umma mtaka kaipata lini? Mbona Kama huyu mtu mnamuabudu sana?
 
Mimi sikubaliani na mkuu wa mkoa kwenda kinyume na Waziri. Huyu mkuu mkoa atolewe hafai. Hayo anayozungumzia ilitakiwa ayazungumze wakikutana na wenzake huko lakini sio kumkosanisha waziri na watoto. Anajenga picha mbaya kwa watoto.
 
Wote wangekuwa na akili kama yako ingekua raha Sana, hata huyo mkuu wa mkoa hii akili hana
Hii kitu inaitwa makambi ni ujinga uliopitiliza. Watoto wanapaswa kufundishwa vizuri kuanzia siku ya kwanza anaingia form 1 hadi siku ya mwisho anamaliza form 4
Haya makambi ni kuzima moto tu, na ndio tunarudi palepale kuwa wanafunzi hawasomi kuelewa bali wanasoma kujibu mitihani
 
ila huyu jamaa SMART sana
 
Na hiki ndio mimi pia nilitaka kusema. Najua hata huyo mtaka watoto wake pia wanasoma shule nzuri

..Nakubaliana na wewe.

..Naamini na wewe utakubaliana na mimi kwamba " makambi ya kukariri mitihani " ni matokeo ya elimu hafifu / duni inayotolewa ktk shule nyingi hapa nchini.

..Kwenye nchi za wenzetu wanafunzi hawapigi kambi kukariri mitihani, bali hupiga kambi kwa ajili ya klabu za debate, sayansi, mashindano ya hesabu, michezo, etc etc.

Cc Chige, Augustine Moshi , Nguruvi3
 
Kunywa soda popote ulipo
Makambi ni ujinga uliopitiliza, Kama tatizo ni watoto hawafundishwi vizuri basi waangalie namna nzuri ya kuwafanyia wafundishwe vizuri kuanzia wanapoingia form 1 hadi wanapomaliza form 4. Na sio haya makambi ambayo yanalenga tu mwanafunzi kufaulu, anafaulu alafu baada ya mwezi kasahau kila kitu.
Tatizo ni ufundishaji hafifu, hapo ndio inabidi waangalie wanafanyaje. Huu ujinga nchi zilizoendelea hakuna.
 
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…