Mwamba katuangusha sana kwa utovu wake wa nidhamu, Sheria na sera za elimu zipo wazi nchini na wizara ina wajibu wa kutoa matamko ya kukumbusha pindi zinapoonekana kutofuatwa! Waziri wa elimu ndiyo mwenye mamlaka ya kutoa muongozo na kauli lakini why MKUU wa mkoa amekuwa mkaidi? Watanzania tuwapinge wote hawa otherwise nchi yetu itakuwa haina mkuu wala kiongozi mwenye mamlaka.
 
Akazumgumze nae nini sasa, iwapo Watoto wa huyo Waziri hawakai kwenye hayo makambi kama wale watoto wa Watanzania maskini?

Binafsi namuunga mkono huyo Mkuu wa Mkoa kwa 100%
 
Huyo Mtaka kama hajapewa maelekezo apunguze mihemko, iko siku watendaji wa hii serikali watatukanana hadharani wakitafuta sifa kwa wananchi.
 
Kwani yeye sio mwanasiasa?
Ni mwanasiasa asiye mwoga, mbona kaeleweka vzr tu, kwamba tumuulize waziri na wewe mtoto wako yuko kwenye hizi shule zetu ambazo hazina mwl wa chemistry?
 
Unajichanganya
Anaulizwa mkuu wa mkoa ila kuja na mbinu zake hutaki

wote tunakubali Mh RC kama alipanic kauli ila ujumbe wake ni sahihi
 
Mpaka lini mtaona haya kumtaja mvurugaji? Ndalichako ni hovyo!
 
Mtaka ni wa hovyo, jiulize ni shule gani hiyo ya serikali ambayo kuanzia asubuhi hadi saa 9 walimu walifundisha muda wote? Shule za serikali kuanzia asubuhi hadi saa 9 unaweza kuta wameingia walimu wasiozidi watatu tu.
Umesikiliza clip yote? Ina dakika 14. Unayoyazungumza ameshayafidia na ametoa njia ya nini kifanyike.
 
..Augustino Mrema naye alijiona ana nguvu sana akatofautiana na msimamo wa serikali, Rais Mwinyi wala hakupoteza muda kumuondoa.

..Huyu asipochukuliwa hatua itajenga mfano mbaya na nidhamu inaweza kutoweka ktk wateule wa Raisi.
Umenena vyema sana.

After all,msimamizi wa utekelezaji wa sera na miongizo ya elimu ni waziri. Alichokisema waziri ndio mwongozo uliopo.

Kama wananchi wa DODOMA wanataka kufanya utaratibu ambao ni kinyume na miongizo,kama kuna masilahi,siyo jambo baya. Lakini kumshambulia hadharani waziri kwa kutekeleza majukumu yake,siyo jambo sahihi. Mtaka amekosea sana. Amejivunjia heshima mno!
 
Faragha ni kwa wanaoweza kusikilizana, vinginevyo ni jambo lusilowezekana
 
Mkuu wa mkoa hana facts ni siasa tu watoto wanahitaji kupumzika bhana.Mbona Tabora girls na tabora boys zimeshika namba 3&4 kitaifa bila makambi.Aaacha kuja mikakati isiyo na takwimu za ukweli
 
asante, wanaume amkeni...kama mbwai na iwe mbwai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…