Dodoma: RC Antony Mtaka amchana Waziri wa Elimu kuhusu mwisho wa Watoto kusoma kuwa ni saa tisa
Mwamba katuangusha sana kwa utovu wake wa nidhamu, Sheria na sera za elimu zipo wazi nchini na wizara ina wajibu wa kutoa matamko ya kukumbusha pindi zinapoonekana kutofuatwa! Waziri wa elimu ndiyo mwenye mamlaka ya kutoa muongozo na kauli lakini why MKUU wa mkoa amekuwa mkaidi? Watanzania tuwapinge wote hawa otherwise nchi yetu itakuwa haina mkuu wala kiongozi mwenye mamlaka.
 
Akazumgumze nae nini sasa, iwapo Watoto wa huyo Waziri hawakai kwenye hayo makambi kama wale watoto wa Watanzania maskini?

Binafsi namuunga mkono huyo Mkuu wa Mkoa kwa 100%
 
Huyo Mtaka kama hajapewa maelekezo apunguze mihemko, iko siku watendaji wa hii serikali watatukanana hadharani wakitafuta sifa kwa wananchi.
 
Kwani yeye sio mwanasiasa?
Ni mwanasiasa asiye mwoga, mbona kaeleweka vzr tu, kwamba tumuulize waziri na wewe mtoto wako yuko kwenye hizi shule zetu ambazo hazina mwl wa chemistry?
 
Mkuu wa mkoa ulipaswa kwenda kuzungumza na waziri faragha sio public kama hivyo. Hapo umekosea mkuu.

Mkuu wa mkoa anapata nguvu wapi ya kupinga maagizo ya Waziri jamani.

Tena maagizo ya waziri wa elimu jamani tena mbele ya wanafunzi kweli.

Waziri hawezi kuwa chanzo cha mkoa wako kuwa wa mwisho. Kwani Mikoa yote ni ya Waziri, na katika hiyo mikoa lazima mmojawapo uwe wa mwisho na mwingine uwe wa, kwanza hata kama yote ikifaulu vizuri.

Mkoa ukiwa wa mwisho wa kuulizwa ni wahusika wa mkoa huo.
Unajichanganya
Anaulizwa mkuu wa mkoa ila kuja na mbinu zake hutaki

wote tunakubali Mh RC kama alipanic kauli ila ujumbe wake ni sahihi
 
Kwani yeye Mtaka anaugomvi na waziri?

Je, kulikuwa na ulazima wa kutaja jina waziri kwenye mikakati yake ya kuinua elimu katika mkoa wake?

Haoni kwamba, tayari amemhasimisha waziri kwa wanafunzi na kwa wazazi kwamba yeye hafai kusikilizwa, na siku ya siku anaweza kuzomewa...?

Hao wote ni wateule wa Rais, kwa nini wasinge fanya chemba kwanza?

Mtaka aache udhalirisha
Mpaka lini mtaona haya kumtaja mvurugaji? Ndalichako ni hovyo!
 
Mtaka ni wa hovyo, jiulize ni shule gani hiyo ya serikali ambayo kuanzia asubuhi hadi saa 9 walimu walifundisha muda wote? Shule za serikali kuanzia asubuhi hadi saa 9 unaweza kuta wameingia walimu wasiozidi watatu tu.
Umesikiliza clip yote? Ina dakika 14. Unayoyazungumza ameshayafidia na ametoa njia ya nini kifanyike.
 
..Augustino Mrema naye alijiona ana nguvu sana akatofautiana na msimamo wa serikali, Rais Mwinyi wala hakupoteza muda kumuondoa.

..Huyu asipochukuliwa hatua itajenga mfano mbaya na nidhamu inaweza kutoweka ktk wateule wa Raisi.
Umenena vyema sana.

After all,msimamizi wa utekelezaji wa sera na miongizo ya elimu ni waziri. Alichokisema waziri ndio mwongozo uliopo.

Kama wananchi wa DODOMA wanataka kufanya utaratibu ambao ni kinyume na miongizo,kama kuna masilahi,siyo jambo baya. Lakini kumshambulia hadharani waziri kwa kutekeleza majukumu yake,siyo jambo sahihi. Mtaka amekosea sana. Amejivunjia heshima mno!
 
Mkuu wa mkoa ulipaswa kwenda kuzungumza na waziri faragha sio public kama hivyo. Hapo umekosea mkuu.

Mkuu wa mkoa anapata nguvu wapi ya kupinga maagizo ya Waziri jamani.

Tena maagizo ya waziri wa elimu jamani tena mbele ya wanafunzi kweli.

Waziri hawezi kuwa chanzo cha mkoa wako kuwa wa mwisho. Kwani Mikoa yote ni ya Waziri, na katika hiyo mikoa lazima mmojawapo uwe wa mwisho na mwingine uwe wa, kwanza hata kama yote ikifaulu vizuri.

Mkoa ukiwa wa mwisho wa kuulizwa ni wahusika wa mkoa huo.
Faragha ni kwa wanaoweza kusikilizana, vinginevyo ni jambo lusilowezekana
 
Swala la Elimu yetu kufanywa kama mpira wa danadana na kila mmoja kuwa anachezea, ni makosa makubwa sana, mwongozo wa pamoja uko wapi?

Napingana na huyo mkuu wa mkoa wenu pendwa, Inakuweje awe na mpango wa kivyake vyake?

Mkuu wa mkoa wa Songea naye awe na matakwa yake, na wa mikoa mingine, tutakuwa taifa la aina gani?
Mkuu wa mkoa hana facts ni siasa tu watoto wanahitaji kupumzika bhana.Mbona Tabora girls na tabora boys zimeshika namba 3&4 kitaifa bila makambi.Aaacha kuja mikakati isiyo na takwimu za ukweli
 
asante, wanaume amkeni...kama mbwai na iwe mbwai
 
Back
Top Bottom