Kwa nini wasiitane wakajadiliana na siyo kudhalirishana?

Tamko la Mtaka, linaondoa heshima ya waziri kwa wanafunzi na wazazi, huoni kwamba kuna siku waziri anaweza kuzomewa kwa tamko la kidhalirishaji la mkuu wa mkoa?

Mkuu wa mkoa, aache dharau, angelikuwa yeye ndio waziri angependa kudhalirishwa kiasi hiko?

Kwani kulikuwa na ulazima wa yeye kutaja jina la waziri kwenye mpango na mikakati yake ya kuboresha Elimu mkoani kwakee?
 
Sasa kama mpango huo huo aliutumia mkoa wa SIMIYU, na ukaleta matokeo mazuri sana, kwanini asiutumie tena?nenda SIMIYU, ukaona mapinduzi ya elimu aliyoyaacha huko kutokana na mfumo huo.
 
Ni kweli mkuu.

Nadhani waziri alibugi kwa namna flani
 
Mkuu afunguliwe uzi huyu mfuasi wa Chatorism hawa ndo Mataga wanao vuruga....
 
Ni kweli Ndalichako ni wa hovyo sana, lakini Tony naye angetumia lugha ya kidiplomasia kidogo kwakuwa watz wa siku hizi wanaelewa kwa haraka.
Hapana mkuu. Sometimes ukitumia lugha ya kidiplomasia ujumbe haufiki.

Ukiwa kwenye administration unaelewa zaidi alilofanya Mtaka. Sometimes you have got to blast someone in front of everybody ili mambo yaende.

Believe me
 
Sasa kama mpango huo huo aliutumia mkoa wa SIMIYU, na ukaleta matokeo mazuri sana, kwanini asiutumie tena?nenda SIMIYU, ukaona mapinduzi ya elimu aliyoyaacha huko kutokana na mfumo huo.
Kwani yeye Mtaka anaugomvi na waziri?

Je, kulikuwa na ulazima wa kutaja jina waziri kwenye mikakati yake ya kuinua elimu katika mkoa wake?

Haoni kwamba, tayari amemhasimisha waziri kwa wanafunzi na kwa wazazi kwamba yeye hafai kusikilizwa, na siku ya siku anaweza kuzomewa...?

Hao wote ni wateule wa Rais, kwa nini wasinge fanya chemba kwanza?

Mtaka aache udhalirishaji
 
Mkuu afunguliwe uzi huyu mfuasi wa Chatorism hawa ndo Mataga wanao vuruga
Kwamba yeye hashindi kwenye kiyoyozi? Kwamba yeye haindeshwi kwenye gari ya kiyoyozi? Kwamba watoto wake hawasomi "international schools"??

CCM wanafiki sana sana, wacha wararuane
Baaambieee hao Mataga...
 
Haya tuma salamu kwa watu watatu.
 
Unajuaje kama hajamtafuta ili wakae na waziri akaishia kumpiga RC danadana??

RC anataka strategies sasa atamsubiri waziri mpaka lini huku waziri anampiga danadana tu??
 
Unajuaje kama hajamtafuta ili wakae na waziri akaishia kumpiga RC danadana??

RC anataka strategies sasa atamsubiri waziri mpaka lini huku waziri anampiga danadana tu??
Ukikaa vizuri ukatulia ukafikirii...! nakuhakikishia mkuu, utakubaliana kwamba, Mtaka, kafanya kosa, kamchonganisha waziri kwa watoto woote wa shule zote hadi vyuoni na kwa wazazi kwamba, hastahili kusikilizwa, kitu ambacho hakikuwa cha lazama mkuu wa mkoa kutamka vile Mbele ya kikao cha wazazi na watoto! Kafanya udhalilishaji

Mtaka mpaka hapa, hafai atimmliwe, ama amwombe radhi waziri peupe kama alivyokuwa akijinadi kwa wazazi
 
LAkini pia si kweli kuwa watoto wanabaki shule kwa sababu masaa waliyopewa tangu asubuhi hayatoshi.
Mara nyingi unakuta mtoto anakuambia wanabaki kufanya masomo ya ziada wakati tangu asubuhi mpaka saa tisa waalimu walioingia kufundisha ni wawili tu na wamefundisha masaa yasiyozidi mawili. alafu unaambiwa saa tisa watoto wabaki kwa masomo ya ziada. Matokeo yake ni kuwashindisha njaa watoto tu.
Anachotetea Mtaka kinakuwa na maana tu iwapo ni kweli waalimu wanawajibika kikamilifu katika muda wao halali wa kufundisha. Otherwise hii kitu inaitwa masomo ya ziada si ya ziada.
 

Erratum: it is "reasonableness" not "reasonability"!
 
Ntinje, mimi ni form four failure, nipo mtaani nafanya umachinga. Ila nikipata nafasi naperuzi kidogo kuhusu wanafalsafa wa kale eg. Karl Marx
 
Huyu jamaaa anakosea Sana kusema maneno kama hayo hata kama ana point, kumsema waziri anayeaminiwa na rais ni utovu wa nidhamu, haya wangetakiwa wayamalize ndani ya serikali
 
Hio ni jungu.
Kama unafahau, au unawafahamu wanaompamba Mtaka mitndanoini kwa nini usiseme wazi.
Mtaka ni kijana safi, kwa kuli na vitendo.
Hata wakati wa Mwendazake , yeye ingalau akii zilikuwa zimetulia.
Hakuwahi kumweka mtu ndani kwa kadri ya kumbukumbu zangu, kama fashioni za kina Makonda na wenziwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…