Dodoma: RC Antony Mtaka amchana Waziri wa Elimu kuhusu mwisho wa Watoto kusoma kuwa ni saa tisa
..Augustino Mrema naye alijiona ana nguvu sana akatofautiana na msimamo wa serikali, Rais Mwinyi wala hakupoteza muda kumuondoa.

..Huyu asipochukuliwa hatua itajenga mfano mbaya na nidhamu inaweza kutoweka ktk wateule wa Raisi.
Mhe. Jokakuu hata mimi nimetangulia kusema kwamba huyo RC kakosea. Mamlaka za uteuzi ndo zenye kauli ya mwisho. Ila tukubaliane kuwa Mtaka anakubalika sana.
 
..Augustino Mrema naye alijiona ana nguvu sana akatofautiana na msimamo wa serikali, Rais Mwinyi wala hakupoteza muda kumuondoa.

..Huyu asipochukuliwa hatua itajenga mfano mbaya na nidhamu inaweza kutoweka ktk wateule wa Raisi.
Tumsamehe. Nafikiri lipo jambo lilimtokea maana kwa jinsi alivyo ni ajabu kutoa lugha zisizo za kiungwana kiasi kile kama vile ana ugomvi binafsi.
 
Huu uongo mmeutoa wapi? Hiyo nguvu ya umma mtaka kaipata lini? Mbona Kama huyu mtu mnamuabudu sana?
Sio hiyo nguvu ya umma ya CHADEMA. Hizi za Mtaka ni zile halisi sio hizo nguvu za KVANT za chadema
 
Mtaka ana hoja, tatizo kuu ni yale mashambulizi kwa boss wake tena very personal. Mtaka si mtu wa mambo hayo, nafikiri lipo jambo.
 
Waziri yupo sahihi,

Muda wa kazi wa Serikali ni saa tisa na nusu.

Waziri kafuata sheria ya kazi ilivyo.

Kinyume na hapo ni fujo.

RC amemkosea heshima Waziri.

Hakupaswa ajibu.Angepiga kimya na akaendelea na mipango yake kimya kimya tu.
Ubinafsi wenu ndio unaowafelisha watoto wa masikini,na agenda zenu ni kutaka watoto wenu tu ndio wawe wasomi, selfish katika ubora wenu
 
Hapa nimekukubali mkongwe. BTW ameomba radhi kiungwana. Tusahau tusonge mbele. Ni mtu mwema na mchapakazi.

..kama ameomba radhi basi naunga mkono RC Mtaka asamehewe.

..wahenga walisema, " we learn from our mistakes. "
 
Mtaka tumemsifia sana sasa kalewa sifa! Anajiona very exceptional
Mtaka ni mjita,anatokea kabila moja na
Kuna ulazima gani wa kumshambulia waziri na familia yake? Kuwa realistic hakuondoi utu brother. Vipi kama wewe ni kiwete nikikuita wewe kiwete njoo hapa? Si realistic? Kwanza kiuongozi huwezi kumzodoa boss wako hadharani namna ile.

Zipo channel za kuchallenge mambo ya utawala! Huu ujasiri si wa bure, Ndalichako ndiye waziri mwenye dhamana ya elimu na aliyemteua ndiye mwenye responsibility ya kumuwajibisha na si huu uhuni.

Kwahili hastahili hata kuomba radhi bila kujivua ukuu wa mkoa maana ameongea kwa msisitizo na kurudia mara nyingi akijua anachofanya.

Wewe unajua, mwambie mtu hapo Chadema amkosoe Mbowe hadharani uone kama atabakia salama! Kuna miiko ya uongozi na Mtaka hajakosea tu bali amekoroga sifa yake njema tuliyomsifia muda mrefu.
Mtaka kakosea sana
 
Tofauti inayoonekana kwa vijana wengi, na ndiyo maana hata ajira zimekuwa ngumu sana, inaonyesha mnaenda shule si kwa ajiri ya kuondoa ujinga

Jenga hoja, na usipende matusi kwani kutoa matusi bila kujenga hoja ni sehemu mojawapo ya kujiani jinsi ulivyo mweupe kichwani

Unadhani hayo anayosimamia mkuu wa mkoa ndio mwongozo kitaifa, na unadhani anachokifanya mkuu wa mkoa hamkivunjii heshima mwingine? Lakini je, kulikuwa na ulazima mkuu wa mkoa kumtaja waziri kwenye kikao hiko?
Nijenge hoja kwa mtu mpumbavu?
 
Mhe. Jokakuu hata mimi nimetangulia kusema kwamba huyo RC kakosea. Mamlaka za uteuzi ndo zenye kauli ya mwisho. Ila tukubaliane kuwa Mtaka anakubalika sana.

..wamesema ameomba RADHI.

..hilo ni jambo la kiungwana.

..litamsaidia yeye Mtaka kuwa makini zaidi.

..pia atakuwa ameonyesha mfano mzuri kwa walioko chini yake, na wananchi kwa ujumla.

..binafsi ningefurahi kama RC Mtaka angekwenda kuomba msamaha mbele ya wale wanafunzi aliwaambia wampuuze Waziri wa Elimu.
 
Kisiasa huyo Mkuu wa mkoa kakosea sana. Alichofanya ni utovu wa nidhamu kwa serikali na Chama Cha Mapinduzi. Sema huyo RC ana nguvu kubwa sana ya umma nyuma yake... kumtumbua kizembe inaweza leta mtikisiko. Waziri angetulia zake na kufanya mambo yanayomhusu. Hii kuingilia hadi watoto wasomeje ni upumbavu kwa hadhi ya waziri.... waziri adili na mambo ya madawati, mitaala, maslahi ya walimu na mambo mengine ngazi ya kitaifa. Kambi za wanafunzi ni jambo dogo mno. Tusubiri uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM (Rais wa JMT) katika hili.
Yaani Mtaka alete impact gani acheni masihara
 
Mataka awaasa wananchi wampuuze Waziri wa Elimu kuhusu mambo ya elimu Kwenye mkoa wa Dodoma.

Mataka amesema wampuuze Waziri ambaye watoto wake wanasoma international school.

Sikiliza audio hapo.
Mama Ndali umezoea kuwaonea wakuu wa taasisi za elimu halafu system inakuangalia tu.

View attachment 1851200


Ndalichako ni Waziri wa kawaida sana. Tokea aingie Wizarani ni kufitinisha tu wenzake.

Wakuu wa taasisi wanamkoma huyu Mama. Wakuu wa idara Wizarani wanaipata habari yake.

Ndalichako badilika Mama Samia yupo tofauti na mwendazake.

Hakuna thamani uliyoongeza hapo Wizarani zaidi ya kufitinisha wakurugenzi na mamlaka za uteuzi.

Tabia ya kuwafitinisha wenzako waondolewe kwenye uteuzi acha mara 1.

Ndalichako alishindwa Baraza la Mitihani kwa ubishi wake ilikuwaje apewe Wizara.

Mama Samia tuondolee huyu Ndali
View attachment 1851425

Badala ya kujadili swala la msingi tunataka kujadili nani mkubwa zaidi. Yaani hapa yunatakiwa tuangalie maslahi ya watoto kwanza. Nakumbuka wakati nikiwa Ilboru pale wote tuliwekwa sawa bila kijali wewe ni mtoto wa nani lakini siku hizi shule ni kwa matabaka na viongozi wengi watoto wao hawako shule za kata. Wakati wetu watoto wa wakulima, mawaziri, mabalozi, viongozi wa mikoa tulikuwa kitu kimoja. Hii imesababisha watoto kujiamini mtaona watoto wa wakulima pale Ilboru kama Lissu na Nyalandu wametoka kama sio washamba kwasababu ya kuwachanganya .
 
Mkuu wa mkoa ulipaswa kwenda kuzungumza na waziri faragha sio public kama hivyo. Hapo umekosea mkuu.

Mkuu wa mkoa anapata nguvu wapi ya kupinga maagizo ya Waziri jamani.

Tena maagizo ya waziri wa elimu jamani tena mbele ya wanafunzi kweli.

Waziri hawezi kuwa chanzo cha mkoa wako kuwa wa mwisho. Kwani Mikoa yote ni ya Waziri, na katika hiyo mikoa lazima mmojawapo uwe wa mwisho na mwingine uwe wa, kwanza hata kama yote ikifaulu vizuri.

Mkoa ukiwa wa mwisho wa kuulizwa ni wahusika wa mkoa huo.
 
Back
Top Bottom