Dodoma: Spika Ndugai awapa mbinu CHADEMA ili awafukuze akina Halima Mdee

Tulilia na nduli wa chato MUNGU akatuondelea mtu yyle dhalimu Kati Taifa letu adhimu

Nafikiri na huyu mjivuni wa kongwa hatustahili anaisigina Sheria wazi wazi anakojolea KATIBA yetu

Amekalia kitu Cha mamlaka huku akitenda kwa ubatili

Najua hatuwezi shika bunduki ,Wala hatuna ubavu wa kupanda na mtu yule basi kwakua Bwana ndio mtoaji wa vyeo na mamlaka hapa dunia je ,si kusema anamuona mtu dhalimu akiwa mfano mbaya kwa ustawi wa nchi.

Bwana afanye lililo jema macho pake(Wala hatuna uwezo kwa kumshurutisha).

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Kwani sheria imeelekeza waambatanishe katiba?
kama mnaona mnaonewa nendeni mahakamani watumnaona mmeshawafukuza bado mnawafuata wa nini? nyie pelekeni watu wengine wakikataliwa nendeni mahakamani basi
 
Anatumika kuficha hoja ya wafanyakazi juzi hakuna kitu hapo na mama anaweza mgeuka kulingana na upepo ulivyo sasa.
Kikao cha mama na spika kabla ya kuhutubia bunge unafikiri kilikuwa cha kunywa kahawa?

[emoji23][emoji23][emoji23]Bavicsha hili suala lirudisheni kwa Mbowe mwenyewe.
 
Mara waseme hatujapata barua, mara siyo barua ni kipeperushi. Ipi ni ipi sasa hapo mbona Jobuu unatucanganya Sana?
 
kama mnaona mnaonewa nendeni mahakamani watumnaona mmeshawafukuza bado mnawafuata wa nini? nyie pelekeni watu wengine wakikataliwa nendeni mahakamani basi
Hujajibu hoja hapo mkuu!
 
Maswali:
1. Mbona haombi nakala ya Katiba ya nchi?
2. Ina maana Spika ana wabunge wanaotoka vyama mbalimbali halafu hana Katiba zao?
3. Ina maana CCM ni ya daraja la juu na hupewa kipaumbele zaidi ya vyama vingine? Maana naona anasema "hata kama barua hiyo inatoka CCM lazima nitawaambia "top" kwanza taratibu".
4. Anapata nini kwa kuwalinda hao wabunge feki?
5. Anajua jinai haifi? Kesho haijulikani, aweza kuja kujibu mbele ya sheria siku moja kwa uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya madaraka. Nani alijua JIWE leo atakuwa historia?
 
Ndugai anaishi kwenye ulimwengu wa mwendazake
 
chama kinapomfukuza mtu uanachama kwa sababu binafsi za chama kinapashwa tu kutoa taarifa kwenye jamii ikiwa na official stamp + signature juu ya maamuzi...

CHADEMA wakifungua kesi, basi Mahakama itatoa court injuction kama ilivyokuwa kwa Zitto. Mzigo utatoka kwa Spika utaenda kwa Mahakama. Inawezekana hicho ndicho CHADEMA hawakitaki maana hawana imani na Mahakama zetu.

Amandla...
 
Reactions: BAK
JIONGEZE acha KUKURUPUKA. Sheria za nchi si za kuchezewa chezewa.
 
Kwani sheria imeelekeza waambatanishe katiba?
Ofisi ya Bunge inatakiwa kuwa na nakala za Katiba za vyama vyote vilivyo ndani ya Bunge. Kudai aambatishiwe Katiba ni kuonyesha kiburi tu.

Amandla...
 
siku zote kufanya maamuzi kwa kusikiliza pressure za watu, mwisho wake, ni mbaya, kwani kuna ubaya gani utaratibu ukafuatwa, tatizo ni kila mtu anataka kufanya maamuzi ya kibabe, ili ionekane tu, yeye yupo imara. Mimi nadhani Ndugai yupo sahihi.
 
La Sophia hulijui weweeeeee! Ungelikuwa unalijua ungelijua kuwa aliitwa kwenye vikao HALALI vya CCM na kujieleza kabla hajachukuliwa hatua.
Mbonà kwa Sofia Simba hakutaka hayo, huyu ni mtu hatari inabidi Mungu ampumzishe Kama alivyompumzisha wa Executive.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…