Pole pole wa nyakati za tume ya Warioba,
Polepole wa nyakati za Rais Magufuli,
Polepole wa Baada ya Rais Magufuli.
Hawa ni watu watatu tofauti hawafanani kiumbo, kinasaba, wadhifa, kiakili, kimawazo, kihoja, kimsimamo wala ki UTU na uzalendo. Hawa watu watatu wanafanana jina na sura tu.
Kwa mtazamo wangu, yule Polepole wa tume ya Warioba wakati wa mchakato wa kupigania Katiba Mpya alikua bora kuliko hawa Polepole wengne.
Polepole wa nyakati za Jaji Warioba yule alikuwa kijana mbichi, mwanazuoni, mwenye misimamo nyoofu kwa maslahi mapana ya taifa.
Polepole wa nyakati za Tume ya Jaji Warioba na Polepole wa nyakati za Rais Magufuli kisha Polepole huyu wa sasa wa nyakati za Rais Samia Suluhu ni maadui ambao wakikutana kuna Polepole ambaye anaweza kuuawa na Polepole mwingine. Mungu aepushie mbali wasikutanishwe kabla ya kupatanishwa.
Anyway wacha Mvua iendelee kunyesha sehemu zote zinazovuja ndani ya serikali, chama na Katiba yetu zifahamike.
NOTE: Nimkumbushe tu Polepole kuwa uhuni ule ule aliokuwa akiupigia debe na kuuchekelea wakati wa utawala wa mwendazake ndio unaomshughulikia yeye leo. Katiba ile aliyosema ni nzuri inatosha hakuna umuhimu wa Katiba Mpya leo ndio inamshughulikia.
Muhimu sana Polepole akumbuke kuwa Serikali na chama chochote cha siasa havina adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu ila vina maslahi ya kudumu. Serikali ile ile iliyokuwa rafiki yake leo ni mwiba kwake.
Ukiua kwa mkuki nawe uta uwawa kwa mkuki. Mungu wetu ni kijana sana ana kulipa uliyo yatenda kwa wapinzani. Ukingali hai. Ulifurahi na kusherehekea madhila waliyo piyia wapinzani, sasa ni samu yako.
Biblia ina tuambia Tajiri akiwa motoni akamuona Lazaro yuko mahali pema, akamuomba achovye vidole vyake kwenye maji ili ampe apooze ulimi wake maana ana teketea. Sasa hilo ni igizo la kwanza, mengi yana kuja. Stay tuned.