Dodoma: Watu wasiojulikana wavunja na kuingia nyumbani kwa Humphrey Polepole na kuiba

Dodoma: Watu wasiojulikana wavunja na kuingia nyumbani kwa Humphrey Polepole na kuiba

Wahuni wamepita na TV🐒

20211213_000658.jpg
 
Haya ndo madhara ya kuingiza machangudoa ndani ya nyumba...polepole aache tabia ya kununua machangudoa na kupeleka nyumbani
 
Hapa ni hakuna kulala mpaka kieleweke. Hakuna kurudi nyuma.
Hatuwezi kukubali Tanzania iangukie mikononi mwa WAHUNI. JPM alipoifikisha Nchi hii hatutakiwi tena kuwaachia WAHUNI wairudishe shimoni.
Ushauri wangu kwa Mh. POLEPOLE ni kama ifuatavyo:-
(1) Awe na ulinzi uliojitosheleza (Mungu akiwa mbele)
(2)Atoe Namba ya simu ili tuweze kumchangia katika harakati hizi.
(3) Kama ni issue ya wazalendo, tupo wengi sana huku mtaani.
Naomba akiweza atembelee Nchi mzima na kuanzisha vikosi vya kizalendo.
KWA NYONGEZA:-
(1) Naviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua kali dhidi ya WAHUNI.
Lakini pia, anapojitokeza mtu mmoja au wachache kati ya Watanzania takribani milioni 60 kutetea maslahi ya Nchi tuchukue jukumu la kuwalinda.
Tusipowalinda wazalendo wa Nchi, tutamlinda nani?
(2) Kuna WAHUNI wengine tunaishi nao mitaani huku. Tuchukue jukumu la kuwakanya waache UHUNI.
Wasipotusikiliza tuchukue hatua stahiki dhidi yao.
(3) Watanzania tuache woga na ubinafsi.Woga wetu ndo umaskini wetu. Miaka 60 ya Uhuru izae matunda ya ukombozi wa fikra zetu.
Kama Mwl. Nyerere alipigania Uhuru wa Tanganyika katikati ya Ukoloni bila kuogopa, sisi tunaogopa nini?
Ahsante, nawasilisha.
 
Ni muhimu hili tukio tukalichambua kwa kina, kwa mfano....

1. Mpaka Sasa Pole Pole anaweza kusema ameibiwa vitu gani mbali na Tv?

2. Ni vitu gani haswa vimeharibiwa?

3. Wahusika walikuwa na msukumo gani? (eg. Kuiba, kuharibu, kudhuru, kuua, kutisha)

4. Mazingira anayoishi Pole Pole yako salama kiasi gani? (Kwa mfano, Uzio, walinzi, Kamera, majirani, milango)

5. Uharibifu huo utakuwa umefanyika muda gani?

6. Pole Pole yeye anaweza kuhisi nini kuhusu hili tukio (unaweza kulihusianisha na mambo yapi?)
 
Pole pole wa nyakati za tume ya Warioba,
Polepole wa nyakati za Rais Magufuli,
Polepole wa Baada ya Rais Magufuli.

Hawa ni watu watatu tofauti hawafanani kiumbo, kinasaba, wadhifa, kiakili, kimawazo, kihoja, kimsimamo wala ki UTU na uzalendo. Hawa watu watatu wanafanana jina na sura tu.

Kwa mtazamo wangu, yule Polepole wa tume ya Warioba wakati wa mchakato wa kupigania Katiba Mpya alikua bora kuliko hawa Polepole wengne.

Polepole wa nyakati za Jaji Warioba yule alikuwa kijana mbichi, mwanazuoni, mwenye misimamo nyoofu kwa maslahi mapana ya taifa.

Polepole wa nyakati za Tume ya Jaji Warioba na Polepole wa nyakati za Rais Magufuli kisha Polepole huyu wa sasa wa nyakati za Rais Samia Suluhu ni maadui ambao wakikutana kuna Polepole ambaye anaweza kuuawa na Polepole mwingine. Mungu aepushie mbali wasikutanishwe kabla ya kupatanishwa.

Anyway wacha Mvua iendelee kunyesha sehemu zote zinazovuja ndani ya serikali, chama na Katiba yetu zifahamike.

NOTE: Nimkumbushe tu Polepole kuwa uhuni ule ule aliokuwa akiupigia debe na kuuchekelea wakati wa utawala wa mwendazake ndio unaomshughulikia yeye leo. Katiba ile aliyosema ni nzuri inatosha hakuna umuhimu wa Katiba Mpya leo ndio inamshughulikia.

Muhimu sana Polepole akumbuke kuwa Serikali na chama chochote cha siasa havina adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu ila vina maslahi ya kudumu. Serikali ile ile iliyokuwa rafiki yake leo ni mwiba kwake.

Ukiua kwa mkuki nawe uta uwawa kwa mkuki. Mungu wetu ni kijana sana ana kulipa uliyo yatenda kwa wapinzani. Ukingali hai. Ulifurahi na kusherehekea madhila waliyo piyia wapinzani, sasa ni samu yako.
Biblia ina tuambia Tajiri akiwa motoni akamuona Lazaro yuko mahali pema, akamuomba achovye vidole vyake kwenye maji ili ampe apooze ulimi wake maana ana teketea. Sasa hilo ni igizo la kwanza, mengi yana kuja. Stay tuned.
 
Ngoja 2025 Ifike, Tutaona Mengi na Sura Zao Halisi. Ngoja Miradi aliyo Anzisha JPM iishe kufunguliwa [emoji28], Tuanze kumpima Amefanya nini? Mwaka mmoja unatimia Mwakani, Tutaangalia.

Hadi Sasa Kikubwa ni TOZO, Tanzania Tungekuwa na Upinzani IMARA, 2025 ulikuwa muda Sahihi wa wao kuchukua Nchi, SEMA JPM aliyajua Yote haya akawafanyia kile alichowafanyia. Hicho Chama Kinapaswa sana Kumshukuru JPM kwa Aliyo yafanya na sio kumfanyia legacy yake Kama Wanavyo mfanyia sasa, wachache wanao mpambania maono yake ndani Ya Chama, Wanafanyiwa UHUNI. Lakini Kiuhalisia na Za Ndani kabisaaaa, Bila JPM, 2025 walikuwa wanaenda kupoteza Madaraka.
 
Back
Top Bottom