Uchaguzi 2020 Dodoma: Yaliyojiri mapokezi ya Tundu Lissu na mkutano mkubwa viwanja vya Uhuru Dodoma

Hivi mbona hamtangazi kama anakuja sehemu? Jamaa zangu wengi waliopo Dodoma hata hawajui kuwa kuna tukio hilo, mna shida gani?
 
Hebu lete hiyo ya watu wengi.
Unajua kwa nini tunaona kweli watu hamna? Kwa sababu hakuna kiongozi yoyote au mwanachadema yoyote aliyepost picha za dodoma, tofauti na ilivyokuwa arusha na mwanza kwa maana kila baada ya dakika picha za kutosha na videos zilikuwa zinamiminika huku mitandaoni
Nipo hapa Uhuru s/msingi watu ni wengi hiyo picha ni ya saa 8 ivii
 
Hata Mimi wakati tunajiandaa na sala ya kumshukuru Mungu usiku nikaanza kuyasikia mahojiano ITV na TAL ikambidi nisalishe fastafasta ili nipate kusikiliza zile nondo Mungu anisamehe sana
 
Sidhani kama uko sahihi: Ninachokiona Lissu ameamua kufanya kwanza kwa zones/kanda ambapo anapita miji mikubwa kwanza, alafu anarudi kufanya vituo vidogo vidogo kwa maana ya miji midogo, mwenge hauruki kijiji
CHADEMA hawaamini katika mfumo wa kuwa na serikali kuu inayofanya kila kitu; wao wanaamini katika serikali ndogo ndogo za majimbo hivyo hata muundo wao wa uongozi wa chama uko kimajimbo (kanda). Anachofanya Lissu kwa sasa ni kufungua rasmi kampeni kwa kila kanda; hii ndio kusema zoezi analoendelea nalo ni ufunguzi bado.
 
Jamani nyie Mwananchi digital simumwache wamtembeze sokoni kwanza au muweke picha za mwaka jana, ona hali ilivyo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…