Uchaguzi 2020 Dodoma: Yaliyojiri mapokezi ya Tundu Lissu na mkutano mkubwa viwanja vya Uhuru Dodoma

Uchaguzi 2020 Dodoma: Yaliyojiri mapokezi ya Tundu Lissu na mkutano mkubwa viwanja vya Uhuru Dodoma

WanaJF

Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu leo anatarajiwa kuzindua kampeni katika Kanda ya Kati mkoani Dodoma.

Rais huyo mtarajiwa wa Tanzania ataambatana na mgombea Mwenza Salum Mwalimu, Katibu Mkuu John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu

Tayari Kuna pilikapilika kubwa hapa jijini Dodoma kuhusu ujio wake na maandamano makubwa ya kumpokea na Mkutano wake katika Uwanja wa Uhuru unatarajiwa kuvunja Rekodi kwa wingi wa watu

Lissu ambaye Watanzania wamembatiza jina la 'Charismatic Leader' amekuwa akilakiwa na Maelfu kwa Malaki ya watu popote anakopita ikiashiria kuzoa wingi wa kura katika uchaguzi mkuu wa October 28

Tutaendelea kuwapa taarifa kwa kila kitakachoendelea
Hivi mbona hamtangazi kama anakuja sehemu? Jamaa zangu wengi waliopo Dodoma hata hawajui kuwa kuna tukio hilo, mna shida gani?
 
Dodoma mbona hakuna watu mkutano wa lissu?? Nini kimetokea??
tapatalk_1599226773981.jpg
 
Hebu lete hiyo ya watu wengi.
Unajua kwa nini tunaona kweli watu hamna? Kwa sababu hakuna kiongozi yoyote au mwanachadema yoyote aliyepost picha za dodoma, tofauti na ilivyokuwa arusha na mwanza kwa maana kila baada ya dakika picha za kutosha na videos zilikuwa zinamiminika huku mitandaoni
Nipo hapa Uhuru s/msingi watu ni wengi hiyo picha ni ya saa 8 ivii
 
wenzako wako TCRA wanapanga namna ya kuikomesha ITV wewe unakenua tu meno ! zile DK 45 zimeharibu ccm kwa 96% , si mchezo .

Nilikuwa pub fulani hivi muda ule , kuna mtu kanywa bia 7 kwa nusu saa tu bila kujielewa kutokana na nondo za Lissu , uzuri ni kwamba alipoletewa bili hakubisha
Hata Mimi wakati tunajiandaa na sala ya kumshukuru Mungu usiku nikaanza kuyasikia mahojiano ITV na TAL ikambidi nisalishe fastafasta ili nipate kusikiliza zile nondo Mungu anisamehe sana
 
Sidhani kama uko sahihi: Ninachokiona Lissu ameamua kufanya kwanza kwa zones/kanda ambapo anapita miji mikubwa kwanza, alafu anarudi kufanya vituo vidogo vidogo kwa maana ya miji midogo, mwenge hauruki kijiji
CHADEMA hawaamini katika mfumo wa kuwa na serikali kuu inayofanya kila kitu; wao wanaamini katika serikali ndogo ndogo za majimbo hivyo hata muundo wao wa uongozi wa chama uko kimajimbo (kanda). Anachofanya Lissu kwa sasa ni kufungua rasmi kampeni kwa kila kanda; hii ndio kusema zoezi analoendelea nalo ni ufunguzi bado.
 
Jamani nyie Mwananchi digital simumwache wamtembeze sokoni kwanza au muweke picha za mwaka jana, ona hali ilivyo.

 
Back
Top Bottom