Uchaguzi 2020 Dodoma: Yaliyojiri mapokezi ya Tundu Lissu na mkutano mkubwa viwanja vya Uhuru Dodoma

Uchaguzi 2020 Dodoma: Yaliyojiri mapokezi ya Tundu Lissu na mkutano mkubwa viwanja vya Uhuru Dodoma

Na haya ndio yanapelekea ITV kuwa supa brand huku tiibiisii ikiendelea kutafuna ruzuku za wananchi pasipo manufaa wala kujiendesha!!! Mpaka leo wana vichaneli viwili aibu kabisa yani wanazidiwa hata na Azam wenye chanel nyingi
Ni sawa na Chadema tu, wachilia mbali ruzuku wanazopata kuna pesa za wabunge pia wanawakata lakini bado wamezidiwa na Diamond, dogo ata chuoni hajaenda anamiliki WASAFI TV, Michadema imebaki kulialia na kudhani ati kuwafukuza TBC ndio watapa kura 💩.
 
Huyu jamaa kampeni zake anafanyia mijini pekee

Sidhani kama uko sahihi: Ninachokiona Lissu ameamua kufanya kwanza kwa zones/kanda ambapo anapita miji mikubwa kwanza, alafu anarudi kufanya vituo vidogo vidogo kwa maana ya miji midogo, mwenge hauruki kijiji
 
saa 15:49 imetangazwa muda wowote LISU atawasili
IMG_20200904_154512_269.jpg
 
Nyie Molemo nyie nina hasira na nyie? Inakuwaje kitengo chenu cha habari kinapwaya namna hii mpaka tunachekwa na mataahira ya Lumumba? Mnashindwa hata kumtengenezea visibility mgombea wetu? Sijaona banner hata moja ya mh. Lissu nini maana yake? Natoa tena ushauri wa bure, tengenezeni picha nyingi za Lissu zisambazwe kwa wagombea ubunge na udiwani kila mmoja awe nayo anapokuwa anahutubia mkutano wa kampeni ameibebele kabisa na anawaelewesha wananchi nini cha kufanya siku ya kupiga kura. Vijijini raia hawamjui Lissu kwa sura. Kuhusu live stream nini kimewashinda? Mnashindwa hata kutumia vijana waliomaliza IT ambao wako mitaani hawana kazi mkawaajiri kwa miezi hii miwili wakawa busy kwenye youtube na kadhalika? Mwambieni mwenyekiti asibanie hiyo hela aliyokuwa anawakata wabunge wetu kwa miaka yote mitano! Uchaguzi ni gharama lazima tukubali kuingia gharama! Safari hii tukishindwa kumtoa mkoloni mweusi bora mimi nirudi tu nikajiunge nayo!
Ukishindwa kupambana,unaungana nao. Pole sana mkuu kwa uchungu ulio nao.

Hawaoni CCM wanavyofanya..ilibidi kila alipo mgombea wa CCM na wa CDM awepo.
 
Ni sawa na Chadema tu, wachilia mbali ruzuku wanazopata kuna pesa za wabunge pia wanawakata lakini bado wamezidiwa na Diamond, dogo ata chuoni hajaenda anamiliki WASAFI TV, Michadema imebaki kulialia na kudhani ati kuwafukuza TBC ndio watapa kura 💩.
Tv na redio zinasajiliwa wapi?
au bado unawaza kwa akili 💩 (nimekunukuu!!)
 
wenzako wako TCRA wanapanga namna ya kuikomesha ITV wewe unakenua tu meno ! zile DK 45 zimeharibu ccm kwa 96% , si mchezo .

Nilikuwa pub fulani hivi muda ule , kuna mtu kanywa bia 7 kwa nusu saa tu bila kujielewa kutokana na nondo za Lissu , uzuri ni kwamba alipoletewa bili hakubisha
Hahahahaha!
Dah, weekedn hii huyo mtu tunaweza kumpata akapate idadi sawa kwa bill yangu??
 
WanaJF

Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu leo anatarajiwa kuzindua kampeni katika Kanda ya Kati mkoani Dodoma.

Rais huyo mtarajiwa wa Tanzania ataambatana na mgombea Mwenza Salum Mwalimu, Katibu Mkuu John Mnyika na Mwenyekiti wa Kanda ya Kati Lazaro Nyalandu

Tayari Kuna pilikapilika kubwa hapa jijini Dodoma kuhusu ujio wake na maandamano makubwa ya kumpokea na Mkutano wake katika Uwanja wa Uhuru unatarajiwa kuvunja Rekodi kwa wingi wa watu

Lissu ambaye Watanzania wamembatiza jina la 'Charismatic Leader' amekuwa akilakiwa na Maelfu kwa Malaki ya watu popote anakopita ikiashiria kuzoa wingi wa kura katika uchaguzi mkuu wa October 28

Tutaendelea kuwapa taarifa kwa kila kitakachoendelea
Hizo sifa unazompa hazina uhalisia wowote, wewe utakuwa ulibemendwa
 
Chadema ndo chama pekee Tanzania chenye Sera ambazo zimelenga kuivusha Tanzania na mtu pekee mwenye uwezo kuongoza Tanzania mpya ni Lissu pekee yake kuna mwingine anajigamba anapambana na ufisadi wakati yeye amejenga uwanja wa ndege wa Kimataifa nyumbani kwake mpaka mbuga ya wanyama amehamishia nyumbani yake ni ulevi wa madaraka #NIYEYE
Lakini angevileta kwenye mkoa unakotoka wewe ungefurahi................. Sisi wote ni Watanzania tusigombanie vito.
 
Dodoma ipi hiyo? Maana mimi nipo hapa mjini kati sijaona, Labda kama bado maana naona kila kitu cha kawaida? SIJUI LABDA BAADAYE, ngoja niendelee kuvuta SUBIRA.
Wanadai viwanja vya Uhuru,,, ndio vipi hapo Dodoma vipo mtaa gani?
 
Back
Top Bottom