Dotto Abdallah Ketto (Doto Magari) atafuna nyama ya kitimoto hadharani

Dotto Abdallah Ketto (Doto Magari) atafuna nyama ya kitimoto hadharani

Yupo sahihi kabisa. Kiasili Watanzania hatuna makatazo ya Nguruwe. Paka, nyoka ndio Watanzania ila mbwa, panya Kuna baadhi ya makabila wanaokula vizuri.
Huwezi Kuacha kula kitoweo Fulani kisa eti wayahudi au waarabu hawali. Suala la nyama ni la kikabila Kuna baadhi ya makabila Yana makatazo ya asili ya kutokula nyama Fulani au sehemu Fulani ya nyama lakini unakuta jamii nyingine zinakula na zipo powa tuu. Hata hivyo vizazi vya Sasa vimeona hata hayo makatazo ya kijadi yslikuwa ni magumashi tuu na Wala hayana madhara yoyote na wanabugia tuu
 
Raha ya kitimoto usiile ushuani. Inatakiwa sehemu kama Mianzini ambapo usafi wa eneo ni wa mashaka huku mpishi mwenyewe haeleweki kama amelewa au yuko sawa. Na wakati wa kula ni mwendo wa kufukuza nzi... halafu eneo liwe limebana hadi nyie wateja kupishana ni kwa shida. Kitimoto ya maeneo hayo inakuwaga tamu balaa.
Nitakuja hilo chimbo mkuu
Haiwezekani sijafika na stori nilishazipata
 
Back
Top Bottom