DP World kuanza kuendesha bandari ya Dar es Salaam tarehe 01 Novemba 2023

DP World kuanza kuendesha bandari ya Dar es Salaam tarehe 01 Novemba 2023

Huenda hii mada ikapata wachangiaji wengi uone vile wabongo walivyo
 
Mimi kama mtanzania;
Mimi kama mtanganyika;
Mimi kama mkatoliki;
Mimi kama mtu mwenye utimamu wa akili;
Naisubiri ccm uchaguzi mkuu wa 2025; kama kweli dp world watatia mguu Tanzania kwa mkataba ule.
Ccm inashinda kwa kishindo 2025. Na DP World anaenda kuleta mapinduzi makubwa katika ufanisi na mapato bandarini
 
Kura yako na ndugu zako hazitabadili chochote mkuu.

Dp world wapo pale pale wala kelele za mafisadi haziwezi kusikilizwa kamwe.
Duh!
Hivi bado unayo matumaini na mpango uliokwisha zimwa. Utakuwa upo dunia yako ya kipekee kabisa.
Lakini ni kawaida ya watu walevi kama wewe kuwa na hali ya namna hiyo, kwa hiyo haishangazi.

Samia, yaani ashinde uchaguzi wa aina yoyote ile, hata wa wizi wa kura. Utakuwa unatania.
 
IGA hiyo hiyo inaanza kazi Novemba mosi, jiandae kisaikolojia. IGA hiyo hiyo haina matatizo yoyote ndio maana tenda zinatangazwa na TPA za kuendesha magati namba nane mpaka kumi na moja hapo hapo bandarini Dar.

Ndio maana tenda ya kuendesha bandari ya Mbegani inatangazwa pia.

Kutakuwa na tenda ya kuendesha bandari ya Tanga itatangazwa muda wowote kuelekea mwishoni mwa mwaka huu.
Bado upo mkuu 'Ntamusana' na matumaini yaleyale ya ufisadi? IGA ilishakufa siku nyingi.

Haya unayozungumzia sasa ni mambo tofauti kabisa na hiyo IGA yenu; lakini inaeleweka, jishikizeni hapo hivyo hivyo kuziba macho ya wasioweza kuona sawasawa.
 
Kelele za Watanganyika kulilia dhidi ya mkataba mbovu wa bandari, hazijasikilizwa na DP WORLD wanaingia rasmi ofisini tarehe 01 November.

Watu walikuwa wanadhani watendaji wa DP WORLD ni Waarabu, hapana, kuna Wazungu, Wahindi, Wafilipino na watu weusi.
Kwani nani alikuambia waliyokua hawatakiwi ni waarabu. Hiklo shirikawanaojua wanajua hao ni wamatekani na waingeteza. Ni ubeberu mtupu na hatari kwa usaama wa nchi yetu
 
Tatizo lako ni uelewa tu. IGA ndio imezaa mikataba ya kibiashara, ambayo inazaa uwekezaji pale bandarini.
 
Tatizo lako ni uelewa tu. IGA ndio imezaa mikataba ya kibiashara, ambayo inazaa uwekezaji pale bandarini.
Mkuu, tusirudi huko tena.
Sahau habari ya IGA, hiyo ni habari iliyokwishapita muda kitambo, na hakwenda popote.
Haya unayotaka kupotosha watu juu yake ni mipango nje ya IGA hiyo mbovu. IGA haipo mahali popote tena.
 
Kwani nani alikuambia waliyokua hawatakiwi ni waarabu. Hiklo shirikawanaojua wanajua hao ni wamatekani na waingeteza. Ni ubeberu mtupu na hatari kwa usaama wa nchi yetu
Hakuna hatari yoyote. Kwa taarifa yako usalama wa uwanja wa ndege na wa bandari muda wote upo kazini.

Pale airport kuna swissport yupo miaka na miaka na hakuna hujuma iliyofanyika. Itatusaidia sana iwapo tutaachana na hizi dhana kwamba bandari ni taasisi nyeti kwa usalama wetu, hayo ni mawazo ya mwaka 1967 enzi za Tanzania ya Mwalimu Nyerere.
 
Kelele za Watanganyika kulilia dhidi ya mkataba mbovu wa bandari, hazijasikilizwa na DP WORLD wanaingia rasmi ofisini tarehe 01 November.

Watu walikuwa wanadhani watendaji wa DP WORLD ni Waarabu, hapana, kuna Wazungu, Wahindi, Wafilipino na watu weusi.
Ikiwa waendeshaji ni hao basi hakuna neno.Tatizo la TEC ni kuhofu DP world ni waarabu watupu.
 
Mimi kama mtanzania;
Mimi kama mtanganyika;
Mimi kama mkatoliki;
Mimi kama mtu mwenye utimamu wa akili;
Naisubiri ccm uchaguzi mkuu wa 2025; kama kweli dp world watatia mguu Tanzania kwa mkataba ule.
Watatia miguu na mikono na hutafanya lolote, wacha 2025 hata 2030 na 2035 hamtafanya chochote na ccm itatawala maisha
 
Mkuu, tusirudi huko tena.
Sahau habari ya IGA, hiyo ni habari iliyokwishapita muda kitambo, na hakwenda popote.
Haya unayotaka kupotosha watu juu yake ni mipango nje ya IGA hiyo mbovu. IGA haipo mahali popote tena.
Kukuelimisha sitochoka kwa sababu naelimisha umma wa watanzania kupitia kwako. IGA iliyopita bungeni ndio hii imezaa Project Contracts ambazo masuala ya ukomo na mengine yenye kuwapa watu dukuduku yamo humo.

Ukubwa wa uwekezaji uliulazimu mkataba mzima upitie kwanza bungeni kupata baraka za kisheria na ndio masuala mengine yaweze kuendelea.

Nchi imesomesha wasomi wengi tatizo letu ni kila mtu kujiona anao uwezo wa kujadili na kuongelea masuala nyeti ya mikataba.
 
HABARI NJEMA HIZII..hapa niko na wazalendo wenzangu tunapongezana hakika bandari inakwenda kuwa injini ya uchumi nchini
 
Kukuelimisha sitochoka kwa sababu naelimisha umma wa watanzania kupitia kwako. IGA iliyopita bungeni ndio hii imezaa Project Contracts ambazo masuala ya ukomo na mengine yenye kuwapa watu dukuduku yamo humo.

Ukubwa wa uwekezaji uliulazimu mkataba mzima upitie kwanza bungeni kupata baraka za kisheria na ndio masuala mengine yaweze kuendelea.

Nchi imesomesha wasomi wengi tatizo letu ni kila mtu kujiona anao uwezo wa kujadili na kuongelea masuala nyeti ya mikataba.
Hiyo elimu yako siitaki na wala huna uwezo wa kufanya hivyo.
La muhimu fahamu tu kuwa ule ujinga wenu na hao waarabu wenu ulikufa kifo cha mende.

Sasa dandieni tu kwenye hii miradi ya kawaida, ili mfiche aibu zenu, mafidadi wakubwa nyinyi.
IGA ilishakufa, isahau moja kwa moja. Usilete upotoshaji hapa.
 
Nchi imesomesha wasomi wengi tatizo letu ni kila mtu kujiona anao uwezo wa kujadili na kuongelea masuala nyeti ya mikataba.
Hilo "Genge" lenu unaloliita la wasomi ni hasara kubwa sana kwa nchi yetu kuwa na watu wa aina ile. Ni aibu kubwa.
Kajitambulisha Hamza pekee yake wengine wote mnajificha kwenye majina ya bandia kama wewe. Ufisadi mliotaka kulifanyia taifa hili na kulidhalilisha aibu yake itawaandama maisha yenu yote.

Kwa kweli inabidi nikushangae wewe, kama nawe unajihesabu kuwa wasomi wa kutegemewa na nchi hii. Ndiyo maana tunaonekana kama vichekesho mbele za mataifa mengine siku hizi, kwa sabau ya "wasomi" wa aina yako na genge lote.
 
Back
Top Bottom