DP World kuanza kuendesha bandari ya Dar es Salaam tarehe 01 Novemba 2023

Wamemkataa shetani na mawakala zake wote.
Wamechemka vibaya sana, DP World wanakuja hapo bandarini. Kukataa uendeshaji ni kujaribu kuikwaza serikali pia ni kuitisha serikali kwamba ikienda kinyume na matakwa ya kanisa basi wao viongozi wa kiroho hawahusiki!!.

Hapo hapo inaibuka hoja ya kuutazama huo usafi wa kimaadili wa baadhi ya maaskofu wanaoitisha serikali.
 
Mimi kama mtanzania;
Mimi kama mtanganyika;
Mimi kama mkatoliki;
Mimi kama mtu mwenye utimamu wa akili;
Naisubiri ccm uchaguzi mkuu wa 2025; kama kweli dp world watatia mguu Tanzania kwa mkataba ule.
Ukatoliki wako una kazi gani juu ya mambo mtambuka ya taifa?!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]

Ninyi kweli ni machizi na hizo imani zetu za mapokeo.....

Taifa letu ni la kijamaa...kaeni na hayo madini yenu mifukoni mwenu....
 
[emoji1787][emoji1787][emoji109][emoji2956][emoji106]
 
Unamaanisha hawana akili kama viongozi wa Uingereza siyo? SAu huelewi kuwa kuna banadari mbili za Uingereza wanaendesha DP World?

Tena kubwa sana mara 100 ya kipande kidogo wanachoendesha kwetu.
Ujuha ndio huu.
Kwa kuwa Uingereza wamefanya ndiyo iwe sababu ya sisi kufanya kama wao? Uingereza wanazo bandari ngapi, na unajua makubaliano waliyofanya na hao DP World ndiyo kama haya ya kipuuzi kama tunayofanya sisi chini ya IGA?

DP World kuendesha siyo hoja, hoja muhimu ni masharti yanayoendana na uendeshaji huo. Hili ndilo hampendi kabisa kulisikia kwa sababu zenu za kijinga tu.
 
Ni kweli kuna ma supervisor wahabeshi tupo nao huku duh! kwisha habari yetu pole pole tutajua wapi pakusimama, maana Suma JKT tayari wamepigwa chini.
 
Utajifanya uonekane mjinga, kumbe ni mjinga kwelikweli.
Kabla ya DP World TICTS walikuwepo hapo, na wengine wengi.
Leo hii kwa ujinga huo huo, unataka watu waamini kwamba ni kwa sababu ya DP World, ndiyo maana tenda zinatolewa Bandarini?
Halafu kwa ujinga wote huu, unang'ang'ana na "usomi na wasomi", sijui wewe unaelewa kitu gani kuhusu usomi unaouzungumzia hapa.

Hata siku moja hujaeleza chochote cha maana kuhusu usomi unaohusu mkataba wa DP World na IGA yake, ambao wasomi wengine wote ila wewe na akina Hamza pekee ndio wenye usomi wa kuyaelewa hayo!
Unauza maneno matupu hapa, kumbe huna lolote.
 
IGA ndio hii hii ya DP World ndio hii hii iliyopita bungeni, ndio maana nimesema hili suala limetutoa jasho mpaka kwenye meno!.
Usidhani watu ni wajinga kutoelewa upotoshaji.

IGA ilishakufa, na kamwe haitatokea tena uwepo wa ujinga kama huo Tanzania.

Sasa subiri tu matokeo ya ujinga wenu yatakavyo watokea puani.
 
Usidhani watu ni wajinga kutoelewa upotoshaji.

IGA ilishakufa, na kamwe haitatokea tena uwepo wa ujinga kama huo Tanzania.

Sasa subiri tu matokeo ya ujinga wenu yatakavyo watokea puani.
Hakuna ujinga ndio ukweli wenyewe kwamba ilipitishwa IGA bungeni baadae zimeandaliwa hizo HGAs na sasa shughuli inaanza.

IGA haziwezi kufa kwani ndio mkataba mama unaotambulika bungeni, tatizo letu ni kujazana ujinga humu mitandaoni mahali ambapo kila mtu anadhani anajua kila kitu hata kile ambacho hana kabisa utaalam nacho.

Hakuna matokeo ya ujinga, ni matokeo ya uwekezaji wa kisasa sana kati ya Tanzania na Dubai.

Huwezi kujenga reli ya SGR kwa matrilioni ya pesa halafu ikae tu kama mapambo wakati Dubai wameshanunua mzigo wa kutosha kule Rwanda na DRC.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…