DP World kuanza kuendesha bandari ya Dar es Salaam tarehe 01 Novemba 2023

Hata kama ni hao hao; hawaji chini ya masharti ya IGA.
Wewe huoni tofauti yake?
IGA imeandikwa kitaalam sana kama ukiwa unaisoma kwa kuchagua kifungu kipi ukijadili na kipi ukiache hautakuja uelewe mkataba ule kwa kina unaongelea kitu gani.

Mkataba unachambuliwa kwa ukamilifu wake sio kwa kuchagua mahali tunapodhani panatupendelea na kuacha vifungu tusivyovipenda.
 
Maprofesa kuhoji ukomo kwenye mkataba wa IGA wakati ukomo unaandikwa baada ya kujua mtaji halisi wa mwendeshaji unakuwa ni kiasi gani. Huko ndiko kuumbuliwa kwa wasomi wetu wanaoongea kingereza kingi mbele ya kamera za TBC na ITV saa mbili usiku.

Mkataba kupita bungeni ni kuuwekea kinga ya kisheria, sio biashara ya mtaji mdogo inayotegemewa kufanyika, ni biashara ya mabilioni ya pesa.

Fitina zako zooote kwisha kudadadekiii.
 
Sasa hata kama hujui taratibu za IGA utajitangazaje wewe kuwa msomi wa uelewa wowote? Hujui baada ya najisi hiyo iliyofanyika Bungeni ni mambo gani yalitakiwa kufanywa kukamilisha matakwa ya IGA?
Mbona hiki ni kiwango cha ujinga wa hali ya juu sana kwa upande wako!
IGA haiwezi kufanya kazi bila kukamilika kwa ngazi zote zilizotakiwa kukamilishwa. Sasa hivi kamuulize Samia kaiweka kabati lipi huko Ikulu.
 
"IGA imeandikwa kitaalam sana...."; haya pekee ndiyo unayoweza kushinda kutwa ukiyaimba kama kasuku, lakini huwezi kuieleza utaalam huo ni upi. Hili ndilo linalokuonyesha kuwa mtu usiyekuwa na elimu ya kutosha kueleza chochote, unabaki kushangilia tu!
 
Unayeongea nae muda huu anazo taarifa zote za hiyo biashara. Novemba Mosi biashara inaanza pale bandarini.

Baada ya kupitishwa bungeni ndio michakato ya kuandaa hizo project contracts ikaanza na ilishamalizika tangu mwezi wa nane.
 
IGA hii imeupa uwezo serikali wa kutaifisha hiyo biashara nzima, kifungu namba 14 B nenda kakisome ukielewe.

Imesema kwamba biashara itafanyika hapo bandarini Dar, nyinyi wapenda fitina na chuki mnadai kwamba DPW kapewa uwezo kisheria wa kuchukua bandari zote kwa maana kwamba amepewa sauti juu ya kila kitu kuhusu mamlaka nzima ya TPA.

Ukweli ni kwamba kapewa magati namba tatu mpaka namba saba pekee.
 
Usichukulie hiyo najisi iliyofanyika bungeni kuwa ndiyo ilikuwa hatua ya mwisho kuufanya ujambazi wenu kuwa halali.
 
Unayeongea nae muda huu anazo taarifa zote za hiyo biashara. Novemba Mosi biashara inaanza pale bandarini.

Baada ya kupitishwa bungeni ndio michakato ya kuandaa hizo project contracts ikaanza na ilishamalizika tangu mwezi wa nane.
Huo ni ujinga wake huyo mtu, wakati akijua miradi yote inayofanyika sasa hivi kuhusu bandari zetu inafanyika nje ya IGA.
 
Yale yale ya "Kifungu", na tulishamaliza hilo kwa wewe kushindwa hata kukiweka hapa kifungu hicho. Leo hii unarudi kulekule, kuonysha upumbavu ulionao.
 
Usichukulie hiyo najisi iliyofanyika bungeni kuwa ndiyo ilikuwa hatua ya mwisho kuufanya ujambazi wenu kuwa halali.
Uelewa wako ni tatizo pia roho mbaya ya asili uliyozaliwa nayo ni tatizo jingine linaloisumbua nafsi yako.

Huo mkataba ni wa kwanza na wa mwisho kupita bungeni? Unajua kuna mikataba mingapi inayaandikwa na kusainiwa ikiwa imepitishwa bungeni?.

Kosa la kuufanya mkataba uka-leak kwenye jamii halitafanyika tena, serikali imejifunza kupitia huu ujinga wa IGA ya DP World.
 
Huo ni ujinga wake huyo mtu, wakati akijua miradi yote inayofanyika sasa hivi kuhusu bandari zetu inafanyika nje ya IGA.
Tafuta wataalam wakupe ufafanuzi. Hujui ulichoandika na kibaya zaidi unaendelea kuamini katika kutokujua kwako.
 
Kuonyesha ufinyu wa akili yako hapa, unasahau kwamba IGA ni kati ya Tanzania na Dubai. Uwekezaji unaotafutwa sasa hivi haulazimishi ushiriki wa DP World kuhusika katika maswala hayo.
 
Iwe roho mbaya hilo siyo swala lako.
Swala hapa ni ujambazi mliotaka kuwafanyia waTanzania kwa mipango yenu miovu kwa taifa lao.

Hili swala la IGA limewaumiza kweli kweli, kama inavyoonyesha katika maandishi yenu.

Huyo aliyeutoa nje ni mzalendo anayestahili kuenziwa na taifa hili, na kuna siku atafahamika tu ili apewe heshima yake stahili.

Sasa unazungumzia "serikali imejifunza...", funzo ambalo limekuja kwa gharama kubwa sana ambalo serkali hiyo hiyo unayoizungumzia maisha yake yakiwa ukingoni.
Watanzania hawataweka serikali nyingine ya kipuuzi kama hii iliyotaka kutunadi wananchi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…