kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Kula samaki Tanzania ni anasa, samaki hawapo na wakiwepo ni ghali hata kama tuna mwambao mrefu sana wa bahari, maziwa na mito. Tunaonekana wote kama vile hatuna akili timamu kwenye kuweka vipaumbe vya taifa na hasa kwa vijana.
Bahari, maziwa na mito ni rasilimali kubwa tayari inayohitaji akili ndogo tu kuweza kuivuna na kusaidia uchumi, afya za watu na ajira kwa vijana. Ukiachana na bandari pia kuna mazao mengi sana ya majini ambayo yanaweza kuwa chanzo ya ajira kwa vijana wengi sana nchini.
Wizara ya uvuvi tengeneza mnyororo mrefu sana na mpana sana utakaowazoa vijana wengi kama sio wote ili waachane na kazi hatarishi za bodaboda na umachinga.
1. Jenga bandari nyingi za uvuvi Dar es salaam,, Tanga, Lindi, Pwani, Mtwara, Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera, Nyasa.
2. Kisha jenga sehemu kubwa za kuhifadhia samaki kuanzia bandarini na kila wilaya nchini
3. Nununua meli kubwa nyingi za uvuvi wa maji ya kina kifupi na kina kirefu
4. Nunua magari mengi ya kusambazia samaki hadi kwenye vituo vilivyoko kila wilaya
5. Nunua boti za kulinda usalama majini kulinda wavuvi na meli/boti za uvuvi na samaki/mazao ya baharini.
6. Wafanyabiashara na wananchi watanunua samaki kutoka wilayani kwenda kwa walaji popote walipo kwenye tarafa, kata, vijiji, vitongoji na kaya.
7. Uza samaki kwa wingi nje ya nchi zenye uhitaji wa samaki (nchi zisizokuwa na bahari, maziwa na mito kama sisi).
8. Wezesha vijana kufuga samaki, kulima mwani na kuvua.
9. Jenga viwanda vya kuchakata samaki
Kama ukiyatimiza hayo Mungu na Umma utakutukuza. Utawafagia vijana wooote mitaani na kuwaingiza kwenye mnyororo wa mrefu na mpana wa samaki na mazao ya majini. Bahari, maziwa na mito vitageuka mfadhili wetu mkuu. Samaki wataliwa nchi nzima kwa bei nafuu na watu/vijana kujiongezea kipato na afya zao zitaboreka.
Kwanini hamfanyi hivyo miaka 65 ya uhuru?. Mna bahati sana tz kuna vyama vya siasa vinavyokosoa tyuuuuu bila kuonyesha ufumbuzi wa matatizo ya wananchi mliyoshindwa kuyatatua.
Ni aibu nchi hii kuwa na vijana wengi wanaokatwa miguu yao kila siku kwasababu ya ajali za bodaboda, eti hakuna ajira.