DR Congo imewanyonga Majambazi 102, Tanzania tunacheka na Panya Road, Wadudu na Magenge Mengine ya Wahalifu

DR Congo imewanyonga Majambazi 102, Tanzania tunacheka na Panya Road, Wadudu na Magenge Mengine ya Wahalifu

Serikali ya Congo imewaua wanaume wapatao 102 kwa njia ya kunyongwa wiki iliyopita, na wengine 70 wanatarajiwa kuuawa. Waziri wa sheria wa nchi hiyo alisema Jumapili katika taarifa kwa Shirika la Habari la Associated Press.

Waziri alisema wanaume hao, wenye umri wa miaka 18 hadi 35, walikuwa majambazi wenye silaha na "wahuni wa mijini," wanaojulikana kama Kulunas, waliouawa katika gereza la Angenga, kaskazini-magharibi mwa DrCongo.

Amesema 45 waliuawa mwishoni mwa Desemba, na wengine 57 waliuawa ndani ya saa 48 zilizopita.

Waziri wa Sheria Constant Mutamba, ambaye anasimamia mauaji hayo, alisema Jumapili jioni kuwa "kundi la tatu litanyongwa, kwa hivyo makundi mawili ya kwanza tayari yameshapewa adhabu ya kifo.
Na wale wanaotuma M23 na kuua Raia wa Congo, wizi wa mali za congo na kujimilikisha mali za congo za umma na wao wamenyongwa?
Maskini mna Roho Mbaya sana, hupenda kufurahia madhira yanayomkuta Maskini Mwenzako.

Mnalaana nyie
 
Na sale wanaotuma M23 na kuua Raia wa Congo, wizi wa mali za congo na kujimilikisha mali za congo za umma na wao wamenyongwa?
Maskini mna Roho Mbaya sana, hupenda kufurahia madhira yanayomkuta Maskini Mwenzako.

Mnalaana nyie
Endelea na wizi wako na kuua raia ukiingia kwenye 18 ni kifo tu mjinga wewe
 
Waziri wa Sheria Constant Mutamba,
1737021230106.jpeg

Waziri wa sheria Constant Mutamba wa DR Congo agonga vichwa vya habari katika media za kieletroniki na magazeti kwa mrengo wake mkali wengine wakihoji mafisadi, wala rushwa, wezi serikalini, bungeni, ofisi za umma, mawaziri kwanini wasikifiwe na sheria ...


View: https://m.youtube.com/shorts/ooeIxA5Dq9Y

Waziri Constant Mutamba amekuwa akishangiliwa kila apitapo na makundi ya watu huku wengi wekisema ni rais wa siku zijazo wa DR Congo


View: https://m.youtube.com/watch?v=3f2CTbLHZ-8
Fuatilia kwa undani operesheni ya kustaajabisha iliyofanywa Kinshasa kurejesha utulivu na usalama. Mamlaka inalenga kutokomeza uhalifu wa mijini na kutoa mazingira ya amani kwa wakazi. ⚡ Muhtasari wa video: Maendeleo ya operesheni ya "Zero Kuluna" Ushuhuda kutoka kwa vyombo vya sheria na wakaazi Uchambuzi wa athari kwa usalama Kinshasa...


Comment wa watu wa Kinshasa:

1. Asante Waziri, tunahitaji mtu kama wewe na vitendo kama hivyo huko Haiti, umefanya vizuri.

2. Kama Mkongo, Waziri wetu wa Sheria lazima pia azuie KULUNAS katika TIES na wabadhirifu wa kukataa hadharani, miongoni mwa wengine, mawaziri, Wakurugenzi wakuu wa makampuni, nk.

3. Hapana, hiyo sio suluhisho. Unda viwanda na mitambo ya usindikaji ifanye kazi, na kufanya uhalifu wa vijana kutoweka


4. Kwamba haya yote yawe fundisho kwa wakuluna na hasa kwa viongozi wetu. Lazima watawala wa serikali kutengeneza sera za ajira kwa vijana ili kuwaepusha watu hawa na hali ya uhalifu

5. Inasikitisha kufika hapa...wazee walioko madarakani na vijana machinjioni...sikufikiri ningeiona hii picha ya Kongo yangu kwa bahati mbaya siwezi kufurahia hilo...ndugu waziri. katika hili la kutafuta haki tuwe makini maana mara nyingi haki inaweza kutukuta na wasio na hatia wanaweza kupita


Soma zaidi comment 113 YouTube
 
Magufuli alituonesha njia nzuri ya kuwafanya hawa wahalifu,adhabu ya kifo si njia sahihi sana, kwanza kwenye maandiko ni dhambi,na ktk sheria ni kuvunja haki ya binadamu (haki ya kuishi) hawa wahalifu, wanatakiwa wasinyongwe, badala yake wafungwe maisha gerezani, wakiwa gerezani wafanyishwe shughuli za uzalishaji mali hasa kilimo manake watakuwa wanaliingizia taifa mapato huku wakijutia kutokana na uhalifu wao. Kazi zipo nyingi zitakazowafanya wafe haraka,kupasua miamba,migodini,kulima kwa muda mwingi nk.
 
Back
Top Bottom