Nyani Ngabu na
Kiranga
Kimsingi nakubaliana na mitazamo yenu.
Lakini katika academic rankings za kwenye academic institutions za Tanzania, mtu kuwa 'Professor' ni ishara ya kupanda kitaaluma.
Ngoja niwape mchanganuo:
1. Tutorial Assistant (B.Sc. or B.A) ,
2. Assistant Lecturer (M.Sc. or M.A),
3. Lecturer (PhD),
4. Associate Professor (PhD and other requirements), na
5. Professsor (PhD and other requirements)
Hata kama neno 'Professor' lina maana ya mwalimu kwa kifaransa, katika academic rankings linamaana kubwa sana. Professor (nazungumzia aliye na PhD na vigezo vingine vinavyohitajiwa) anakuwa ni nguli katika eneo lake la kitaalamu.
Tatizo kwa upande wa Tanzania linakuja katika namna ya vigezo vingine (zaidi ya kuwa na PhD) vinavyopatikana na kuwa assessed. Kwa mfano, moja ya vigezo ni kuwa na published articles katika 'international journals'. Kwa Tanzania, vyuo vikuu havina utaratibu wa kurank hizi international journals. Mwishowe, watu wanakuwa promoted to 'Professorship' katika journals ambazo hata published articles zao haziwe kusomwa wala kuinfluence policy, knowledge, theories n.k.
Katika publishing world kuna namna journals zinakuwa ranked kwa namna articles zinazochapishwa katika journals hizo zinavyokuwa cited na kuinfluence the state of knowledge. Hapa ndipo unasikia journal inakuwa na 'impact factor'. Kwa sasa, journals zenye high impact factor katika ulimwengu wa sayansi ni journals za 'Nature', 'Cell', 'PLoS', na Science'. Pia kuna journals zingine zinakuwa na high impact factor katika eneo husika la kitaaluma kama fizikia, kemia, uchumi, elimu, biashara, siasa, tiba, mazingira, sheria n.k.
Kwa vyuo vikuu vya nje, promotion based on published works inakuwa scrutinised kwelikweli kwa assessors kuangalia aina za journals ambazo mtu anaye seek promotion amepublish. Kwa Tanzania, nimeambiwa hilo suala halifuatiliwi kabisa, ilimradi iitwe international journal, basi mtu atasubmit hizo published articles kwa promotion.
Nitafurahi kuona journals ambazo Kitila Mkumbo kapublish maandiko yake aliyoyatumia kuseek promotion to associate professorship.
Ni hayo tu.