Droo ya Play-off, Yanga yapangwa na Club Africain ya Tunisia

Droo itakayofata kwa Yanga ni Azam Sports Federation🤣🤣
 
Fact ya kwanza ya kuzingatia kabla hujaangalia rekodi unatakiwa ujue timu ambayo ni mbovu ndio huanzia nyumbani
Kwahiyo wale Waarabu waliowatowa Azzam ni wabovu?

Kaizer Chief wakati wanawakalisha 4 bila kwao ni wabovu?

Kwa watu wenye Mipango kuanzia nyumbani ni faida mechi unaimaliza mapema kabisa.
 
Kwahiyo wale Waarabu waliowatowa Azzam ni wabovu?

Kaizer Chief wakati wanawakalisha 4 bila kwao ni wabovu?

Kwa watu wenye Mipango kuanzia nyumbani ni faida mechi unaimaliza mapema kabisa.
Sio kila mzungu ni doctor

Sio kila muarabu ana kiwango

Ni kama Al Hilal tu sema ndio hivyo alikutana na mpinzani ambaye kamzidi nafuu
 
Yanga wamepangiwa hatua ya mtoano dhidi ya Club Africain ya waarabu. Hawa ndio wale waliowapiga Kipanga FC 7-0 huko shirikisho.

Club Africain ni timu Kongwe na walishatwaa ubingwa wa Klabu bingwa Afika mwaka 1991. Hawa jamaa wanamiliki uwanja wao unaobeba watazamaji 60,000/= kama kwa mkapa tu. Wapinzani wao wakubwa na wanaocheza nao derby ni ES Tunis na pia wana upinzani wa jadi na Etoel du sahel na MC Alger ya Algeria.

Club Africain ni timu inayocheza kwa mbinu za hali ya juu wakiwa ugenini huwa wanacheza kwa tahadhari ya kutopoteza mchezo na wakiwa nyumbani huwa wanaachia majini yao yote na ndio kilichomkuta kipanga.

Yanga wasichukulie kuwa hawa ni wepesi kwa kuwa kwenye ligi yao walimaliza nafasi ya 4. Tunajua wenzetu uwekezaji wao ulivyo hata timu za chini zina uwezo mkubwa.

Tarehe 2 November itakuwa kipimo kingine kwa Yanga ambao kwa hapa ndio underdog na wataanzia tena nyumbani kama kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…