PreGE2025 Dudubaya: Katiba imeruhusu kuwa na wabunge wajinga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ufafanuzi
Kwa wakati huo na mahitaji ya uhuru na post uhuru katiba ilikuwa relevant. Alichofeli ni kuamini aatakao waachia, watabadili katiba ili kuendana na mahitaji ya vizazi vijavyo. He was so so wrong
Katiba iliyopo inategemea busara ya kiongoz , si miongozo iliyopo.

Na ndio tatizo lililopo
 
Alizingatia kuweka fursa sawa kwa wote....wasomi na wasio wa wasomi wote ni wetu.
 
Nyerere habebi lawama kwa hili kwani kwa wakati huo tulikuwa tunapambania kujua kusoma na kuandika tu. Diploma na degree za kumwaga ni mambo ya 2010, hivyo lawama ni kwa Kikwete, Magufuli na Samia walioshindwa kuleta katiba inayoendana na nyakati hizi.
 
Hadi 1977 wasomi walikuwa wachache?
Na hadi 1985 alipoondoka madarakani je?
Tena alisema katiba inampa raisi nguvu kubwa ya kuweza kuwa dikteta.
 
Mbunge anapongeza uvunjaji wa Sheria anazozitunga yeye na katiba aliyoapa kulinda huo ni uzezeta wahali ya juu.
Unapongeza utekwaji na mauaji ya wananchi wanaokulipa mshahara tenalingine ni libunge mwanamke mwenye ushungi kabisa! Anamwacha Mungu anatetea uovu na kujidai mkali... Jinga kabisa!!
 
Ulikuwa Wakati Huo
Ila Hakuandika Masahafu au Biblia
Kwamba Wakati Wenu Msibadilishe
 
Ulikuwa Wakati Huo
Ila Hakuandika Masahafu au Biblia
Kwamba Wakati Wenu Msibadilishe
 
Mkuu kwa kipindi kile watu wengi walikuwa kama hawa hadzabe…angefanya nini? Muhadzabe leo hii unampelekea pepsi anaitingisha then wanaifungua…ikianza kurusha mapovu wanaitupa na kuanza kutimua mbio…
 
Hakuna cha rushwa wala nini.
Wananchi wenyewe ni wajinga ndiyo mana wanawachagua wajinga.

Watanzania wengi hawajui wanataka nini ndiyo mana wanachezewa na wajinga.

Hata mashairi yao ni ya kijinga jinga tu.
Hakuna mwananchi anachagua mbunge.
Wabunge wanapitishwa kwa nguvu ya pesa ama amri kutoka kwa mwenyekiti wa CCM.

Kwenye bunge lenye wabunge 264, wabunge waliochaguliwa na wananchi hawazidi 40, wengine waliwekwa kwa utashi wa Jiwe.

Hizi kelele zote za "mama hivi, mama vile", kusifu kuliko hata Mungu anavyosifiwa, ni katika zile harakati za kuonekana ili kwenye mchakato wa uchaguzi waonwe na kusaidiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…