Dunia hii vilaza ndo wanafanikiwa, wenye akili wanaishia kufa kwa stress

Umesema wanaosoma sayansi ndio watu wenye akili. Nimekuuliza unamfahamu Lee Kuan Yew unaruka ruka kama umepigwa shoti jibu swali nakusubiri
 
Nimekumbuka, Kuna jamaa tulisoma shule moja hakuw serious Kabisa na shule alikua msela msela tu. Jamaa aliendaga jeshi wakamsomesha huko nchi za nje sahivi ni Major JWTZ.

Mimi mwenyewe nina jamaa yangu. Enzi za chuo mzumbe darasani alikuwa haji kabisa kila siku ana sap .. kamaliza na gpa ndogoo.

Tulivyomaliza chuo tu. Akaingia polisi... enzi zile ajira zilikuwa nyingi hivyo graduates hawataki upolisi.

Jamaa polisi kule na degree yake kapewa nyota.. mara nyota mbili.. mara kapelekwa ulaya kusomea mambo ya upelelezi.. sasa hivi ana cheo kikubwa na ana maisha ya juu sana .

Kila siku safari za nje ya nchi tu akiwakilisha polisi
 
Tupo tunatengeneza Sumu za HKL mkauane vizuri siasani.
Tulichofaulu zaidi ni kugeuza kila chakula kuwa pombe... Mtakufa njaa mbwa nyie ila walevi wataenjoi Hadi kufa.
 
Mkuu ndio uwezo wako wa kufikilia umeishia hapo, yaani unapima uwezo wa akili kwa kiwango cha pesa
 
Pia kuna wanaolia kwa kusoma hkl au kwa kutokusoma
 
Tuulaumu mfumo wetu wa elimu tu sio watu wenyewe
 
Sasa we unasemaje kwan
 
Mbona JPM ni mwanasayansi lakini alikuwa MWONGO kuanzia Thesis ya PhD aliyofoji hadi kutuambia anajenga miundombinu kwa fedha za ndani. Prof Sospeter Muhongo ni mwanasayansi lakini naye alitudanganya kuwa gesi ya Mtwara ndiyo suluhisho la umeme na umaskini wa Tanzania.

Acha kuhaIaIlisha uwongo wako na Physics!! Kupata A+ Physics siyo kipimo cha IQ kubwa hata kidogo
 
Ila na wewe umezingua kutudharau tuliosoma masomo ya sanaa. Kisa tu umejaliwa akili ya kukariri Archimedes Principle na Law of floatation, basi ndiyo unajiona una akili!!

Kwa taarifa yako watu wenye akili halali ni wale wanaoweza kupambana na maisha mtaani. Na siyo kwa kukariri masomo na kupata divisheni 1.


Na kinachotokea Tanzania hakijasababishwa na watu wa masomo ya sanaa!! Isipokuwa kinatokana na sera mbovu za CCM na mfumo wake wa kupeana kazi/vyeo kwa kujuana! Badala ya kuangalia uwezo wa mtu.

Maana Magufuli alisomea masomo ya Sayansi, lakini mpaka muda huu ndiyo anaongoza kwa kuitawala nchi hovyo.
 
Kwenye maisha hata kama ulisomea mambo ya nyuki hakikisha una nidhamu hasa kwa waliokuzidi umri. Vijana wanaopata ulaji wengi wao wana nidhamu kuanzia nyumbani, shuleni, kanisani au msikitini na kwenye jamii yote kiujumla. Wakati wewe bila aibu unawadharau kina Msigwa, Kabudi na Rioba kuna vijana wenzako wanapata connection za uhakika kupitia wao. Unaweza ukawa umesoma PCM na kufaulu vizuri ila kama huna nidhamu utaishia kulalamika tu mitandaoni.
 
Waliosoma sayansi wapo wa kutosha kwenye uongozi, ni maamuzi binafsi.

Festo pale TAMISEMI ni MD, Gwaji (KE) MD, Hussein Mwinyi MD, JK, JPM, Dr. Gharib Bilali, Dr. Sheni...
 
Una mawazo ya kitoto sana.
 
Kilaza Ni baba yako.
Pumbavu Sana wewe.
 
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…