Dunia imechelewa mno kuishtukia Marekani kuhusu utawala wa pesa yake DOLA katika uchumi wa dunia. Angalau sasa wameishtukia

Dunia imechelewa mno kuishtukia Marekani kuhusu utawala wa pesa yake DOLA katika uchumi wa dunia. Angalau sasa wameishtukia

No
Huu mchezo wa kuchapa pesa ndio mchezo wao.
Marekani inaweza kuchapa pesa na kuzitia kwenye mfuko kisha kuja direct Tanzania kununua dhahabu , rubi n.k
Ila wewe huwezi kuchapa pesa zako za Kitanzania na kuzibeba kama zilivyo kwenda kununua kitu US.
Kwa Nini Wao Wanaweza Kufanya Hivyo Na Sisi Hatuwezi?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
huyu hajui, unazichapa nyingi kununua rubby tanzania halafu Tz inazirudisha kwako kukunu Boeing! does it make sense kweli?
unahis wamenunua mara ngap ? je tungekuwa na boeng ngap ?
 
sandali usitoe weak reasoning to that level! f that is the case, then tanzania tutanunua Boeing kama IST toka marekani, maana tutakuwa na madola kibao ya madini yetu!
umewai kumjibu chief
 
Marekani iliipiga changa ya macho dunia kwa muda mrefu. Ikalazimisha dola iwe ndio pesa rasmi katika biashara za kimataifa na uchumi wa dunia. Wanachofanya ni kuchapisha noti tu za dola na kuipa thamani kwa kauli tu.

Dunia nayo ikawa imejikuta inakubaliana na changa hilo la macho. Lakini Urusi imeiamsha dunia na marekani imepaniki. Urusi imesema kila nchi inaweza kutumia pesa yake ya ndani kwenye miamala ya kimataifa.

Uamuzi huo ghafla ukairudishia thamani pesa yake ya ruble iliyokuwa imeshuka sana thamani kwa zaidi ya asilimia 90.

Kwa sasa mataifa kama india, China, Brazili tayari yamejifunza kitu na yataanza kutumia pesa za mataifa yao kwenye biashara baina yao na mataifa mengine yatakayokubali.

Urusi imeandaa mfumo wake kama ule wa SWIFT kwa ajili ya miamala ya kimataifa na nchi zimeshajiunga tayari na kwa kuanzia mataifa hayo (ukiacha mataifa ambayo hayaogopi kitu kama India na China) hayataainishwa ili kuyakinga na vitisho na vikwazo vya marekani.

Ndio maana Marekani inahaha kuongeza vikwazo kila siku na kupeleka silaha ukraine, si kwa kuwa inaipenda sana ukraine lakini inataka kuangusha kabisa uchumi wa urusi na kuipunguza nguvu kijeshi.

Japo mpaka sasa marekani inaonekana haijafanikiwa kwa hilo ila mambo yanaigeukia yenyewe kuwa mabaya!
Kaka hii dunia mwenye nguvu ni yule anayeweza change narration. Anayeweza sema hiki ni cheupe ingawa ni cheusi, na wote tukakubali kuwa ni cheupe. Watu kama hawa hata ukiwa na bonge la dhahabu mkononi, wakisema ulichoshika ni blood diamond, thamani yake inashuka hadi sifuri. Wanaweza set bei ya unachouza, na wao wakiwa wanunuzi wakuu.

Kwamba taifa lingine litakuja kuwa na nguvu zaidi ya US iwe kwa pesa au kitu chochote kile hakitaondoa umaskini wetu.

China na Russia kuanzisha SWIFT si kwa manufaa ya Watanzania. Hata tukichekelea sana hatuna share huko. Kote tutakakoingia tutakuwa digidigi. Ni manufaa yao. Ni walewale. Hakuna Taifa lina interest ya Taifa lingine, iwe Uchina, Urusi, US n.k.

Tuna vya kujifunza kwa nguvu aliyonayo US na mataifa mengine kwa sasa.

Tusife tukishababia minyukano ya US vs China, Ukraine, US, NATO vs Russia. Sisi ni Watanzania. Tuamke.
 
Viwanda vya china /urusi haviwezi kushindana na vya USA kwa ubora, ndiyo maana huoni Ihone maduka ya mitaani. By the way, viwanda vya maana vingi uchina ni patent za USA, Am I right?
Ukiwaambia kuwa uchumi wa china unabebwa na US na Ulaya hawatakuelewa, pia US na Ulaya bidhaa zao ni jiwe haswa, tofauti na china.
 
Kuna Nchi Zina Uwezo Kiuchumi Kwa Sababu Wanatecnologia Ya Kutengeneza Vitu Je Sisi Tutaweza Kuipata Wapi Hiyo Tecnologia AU Tukachukue Huko Kwao Kama Kuunda Magali Kutengeneza,Ndege,Simu?
Naomba Majibu.

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Thamani ya fedha inategemea na utegemezi wa bidhaa na mahitaji ya nchi yako.

USA thamani ya fedha yake ni kubwa kwa sababu anazalisha bidhaa nyingi zinazotegemewa na watumiaji wengi duniani

Sasa wewe ulazimishe itumike fedha katika mauzo ya bidhaa ipi?
Dola ya marekani inaongezewa thamani na nchi za kiarab maana waliingia mkataba wa manunuzi yote ya mafuta lazima yatumie dola
 
Si kweli, thamani ya pesa inatokana na what you produce to the world. Kila kitu kinapatikana USA, kila nchi inahitaji kitu from USA, fedha yao itaabudiwa tu!
Hamna ukwlei, ....pesa ya Kenya ina thamani zaidi ya pesa ya Japan[emoji51][emoji51]
 
Utakuwa nyumbani au milembe hospital[emoji23][emoji23][emoji23][emoji845][emoji3480]
sisi wacommunist tunauwezo mdogo kudili na Mambo makubwa Ukraine chambo tu na dollar nihabari ya dunia kizazi and generation .......rubble angalia tu neno lenyewe lapesa
 
Kila kitu kitu gani..acha fix. Inaonekana ubongo wako umejaa propaganda mpaka huwezi kupumua
Cha kujiuliza ni hapo kwako na kwangu na kwa mwingine,ofisini, barabarani unatumia vitu vingapi vya mmarekani ndio tutapata jibu la uhitaji wa dola.
Mimi simu mchina, computer (used) marekani, pikipiki china,redio japani, computer desktop Japan, assets bongo land , nguo China/ ulaya, Madawa ya shambani China nk.
Internet na software marekani.
Kwa kiasi gani namtegemea marekani? Labda 20%.
Bila USA maisha yanawezekana ila mazoea tu ndio yanatuponza.
Sasa internet kuna 5G ya mchina akizingua USA nchi inafunga mitambo ya mchina, sina hakika kama Russia wana internet yao.
 
the world is not static anything can happen,its matter of time
Si kweli, thamani ya pesa inatokana na what you produce to the world. Kila kitu kinapatikana USA, kila nchi inahitaji kitu from USA, fedha yao itaabudiwa tu!
 
Back
Top Bottom