YALIYOJIRI MKUTANO WA KAMATI YA MARIDHIANO, BWAWANI ZNZ 23 NOVEMBER
Yote yaliyojitokeza katika mkutano huo yapo katika uzi huu (video zitawekwa)
Waliokuwa wasemaji ni Mzee Hassan Moyo, Mzee Salim Rashid (Katibu wa kwanza wa baraza la mapinduzi), Mansour Himid, Jusa Ismail, Ali Salehe(Mjumbe wa iliyokuwa tume), Eddy Riyami na mshereheshaji Bimani.
Katika wazungumzaji wote, hakuna hata mmoja aliyesimama na kusema 'wazanzibar hawataki muungano''
Walichokuwa wanapigania ni kuwa na muungano wenye masilahi kwao.
Kuna sehemu moja Eddy Riyami alisema ''.... katiba ya Chenge ni kuendeleza ukoloni wa Watanganyika''
Nilimshangaa kama nilivyomshangaa Sheikh katika bandiko hapo juu.
Haiwezekani Wazanzibar watambue kuwa Tanganyika ni mkoloni, lakini waendelee kutafuta njia za kuishi na mkoloni huyo huyo.
Ingalikuwa vema kama wangeamua kuachana na mkoloni kuliko kubaki na duku duku mioyoni.
Mzee Salim Rashid,alifananisha ZNZ na ya Mauritius na Seychelles.
Akasema ZNZ inaweza kuwa na kipato cha mtu kikubwa kama nchi hizo mbili.
Alitaja idadi kama watu milioni 1.2.
Ninamshangaa Mzee Rashid kwasababu, hakuna sababu ya muungano na Tanganyika ikiwa znz inaweza kuendeleza watu wake.
Mzee Rashid hakueleza ukweli kuwa kati ya hao 1.2 nusu yao wamekimbilia Tanganyika wanakoishi bila tatizo.
Mzee Rashid aelewe mazingira ya Seychelles au Mauritius ni tofauti na ya znz.
Kijiografia znz inabaki kuwa katika kivuli cha Tanganyika kwa hiari au kwa lazima.
Si hiari au lazima ya mtu, bali mazingira yaliyotengenezwa na mwenyezi mungu.
Hata hivyo, badala ya kulalamika, alikuwa na wajibu wa kuhamasisha wznz wakatae muungano kabisa ili wawe kama Mauritius.
Mansour Himid, aliongelea sana kuhusu maridhiano. Alionyesha kuwa wapo watu wanaotaka znz kamili lakini hawawezi kusema kwa woga. Akasema, watu hao wakisikia jambo wanapanda ndege na kukimbia wakiacha msala kwa wenzao.
Hapa alikuwa anamsema Shemeji yake ambaye ni Karume kwa namna ya kiungwana sana.
Jusa alitumia muda mwingi kulinganisha katiba ya 1977, ya Chenge na ya ZNZ.
Alitumia taaluma yake kuonyesha jinsi katiba ya Chenge ilivyochukua nafasi ya ile ya 1977.
Na alionyesha ugumu uliopo hata pale katiba ya Chenge itakapolzimishwa. Ugumu huo unatokana na kubadili katiba ya znz ambayo ina masharti magumu.
Pamoja na umahiri wa kuelezea, Jusa aliacha ukweli na kuzungumzia mambo yasiyo na maana katika kuwapendeza wazanzibar.
Hapo ndipo tunasema, muungano upo katika matatizo makubwa.
Viongozi hawazungumzii ukweli, bali kupotosha watu wao pengine wakitaraji kupigiwa makofi.
Kwa mfano, badala ya kuongelea wingi wa viongozi wa katiba ya Chenge kwa kulinganisha na rasimu ya Warioba, Jusa aliongelea madaraka ya Rais wa znz katika katiba ya Chenge.
Tulidhani kuwa wananchi walitakiwa waelezwe, ile hoja ya gharama kubwa kwa S3 iimejibiwa vipi na rasimu ya Chenge.
Na hapa wznz walitakiwa waelewe zaidi kwani wao ndio wenye malalamiko na wao ndio hawaelewi hasa wanataka nini.
Kwanini hawawelewi!
Mansour kaonyesha picha ya wa kaskazini na kusini, waarabu na waswahili.
Kwasasa wanalaumiana, kwamba wale waliotengeneza katiba ya znz ya 2010 ndio wameenda kutengeneza katiba ya Chenge. Kwamba, kuna kusalitiana na kuisaliti znz.
Hoja hizo zimeungwa mkono na kauli za mzee Moyo, Eddy.
Lakini pamoja na kutojielewa na kutojua nafasi yao, wznz wanaficha ukweli kwa kumtuhumu Mtanganyika.
Mtanganyika wameshaelewa ni mkoloni, vipi wznz wamuunge mkono kama walivyofanya kwa Chenge?
Kuanzia leo tutakuwa na mjadala wa video za mkutano wa Bwawani kwa kila mzungumzaji.
Tutabainisha ukweli na kuonyesha upotoshaji.
Tusemezane
https://www.youtube.com/watch?v=PCwc-W8mIuA
https://www.youtube.com/watch?v=P5t_842bXCs
https://www.youtube.com/watch?v=0HfChC3Uric
https://www.youtube.com/watch?v=LQLMhaNY7x0
https://www.youtube.com/watch?v=FlECaPDYzVQ
Wanaamvi
Tuliwahidi kuweka video za mkutano wa kamati ya maridhiano Bwawani znz dec 23 2014. Video zipo katika link hizo hapo juu
Pia kuna video ya CCM na jinsi walivyojadili katiba pendekezwa ya Chama chao iliyoandikwa na Chenge
Naomb mpitie video hizo ili mjadala ukiaendelea tuwe pamoja
Ahsante, wakati ukichambua katika forum ya uchumi yutakuja kujadiliana. Nausubiri huo uzi wako kwa hamu.Nguruvi3,
Naona sasa ya Tanganyika yamekushinda na kuanza kudandia ya Znz. Hakika mambo ya Znz ni makubwa sana na yanataka mtu mwenye upeo wa juu wa uelewa na aliyeenda skuli sio kama wewe.
Labda nikudadavulie kidogo hapa. Kinachofanywa na Znz na kuilimishana na kubainishana MUUNGANO na mapungufu yake katika kuinua uchumi wa Znz.
Nitakupa kitu kidogo sana hapa kinacho wakwaza Znz hususan katika suala la UCHUMI WA NCHI hiyo. Najua inaweza kuwa darsa kubwa sana kwako kutokana na ilmu yako lakin nitaweka kiduchu kwa faida ya wasomaji wengine wenye ilmu na walioilimika.
Ikumbukwe kuwa miongoni mwa mambo ambayo yanachangia kukuza uchumi katika nchi ni UWEKEZAJI WA MOJA KWA MOJA KUTOKA NJE (yaani tunaita FOREIGN DIRECT INVESTMENT- FDI)
uwekezaji huu wa makampuni ya nje ni muhimu katika uchumi wa kileo chini ya biashara huru na utandawazi. Uwekezaji huu unachangia ukuaji wa uchumi wa nchi husika.
Ukitazama kwa huko Tanzania SUALA LA UCHUMI SIO SUALA LA MUUNGANO lakin kwa sababu za mfumo wa Muungano uliopo suala hilo linatekelezwa kama suala la muungano.
Ikumbukwe kuwa Znz haimiliki sera za KIUCHUMI na hivyo inakuwa vigumu sana kuwashawishi wawekezaji wakubwa wa FDI kuwekeza maana wawekezaji wenye miradi mikubwa wanahitaji kwanza uhakika wa miradi yao kulindwa, mazingira mazuri ya kuwavutia, sera za fedhwa na kodi ambazo zote HAZIMO KATIKA MAMLAKA YA ZNZ.
mazingira ya Sasa yaliyopo ZNZ chini ya mfumo wenu wa Muungano yanampa ugumu muwekezaji kuvutika na kuwekeza Znz hasa akitazama utitiri wa kodi, kuna TRA, ZRB. Je ni mwekezaji gani atakwenda kuwekeza katika utitiri wa kodi namna hiyo.
Kumbuka kuwa FDI ina aina mbili za uwekezaji ambazo ni ULE WA FIXED ASSET na ule WA PORTFOLIO INVESTMENT ambazo zote zinachangia kukuza uchumi wa nchi husika.
( Darsa hili nitalichambua kwa kina katika forum ya uchumi).
Nisikuache hivi hivi nikupe kiduchu tena faida za FDI. ni kuongeza fursa za ajira, mapato kuongezaka, na kubadilishana technologies,utaalamu na kuongeza fedhwa za kigeni katika nchi.
Nguruvi.
najua ni darsa kubwa kwako lakin kiduuuchu nimekufumbua mambo uone KWANINI ZNZ WANATAKA UHURU KAMILI WA UCHUMI. Na darsa kama hizo za akina Jussa na wenzake ni kuwaandaa wananchi wajitambua na kuchukua hatua stahiki wakti unapotimu
POLE SANA.
Ahsante, wakati ukichambua katika forum ya uchumi yutakuja kujadiliana. Nausubiri huo uzi wako kwa hamu.
Mara nyingi napata taabu sana kujadiliana nawe. Mada iliyopo mbele ni video za wazungumzaji wa kongamano.
Hakuna aliyesema kongamano ni haramu, na hakuna anayesema maoni yao yana makosa.
Kinachozungumzwa hapa ni jinsi gani walivyogawanyika katika suala zima la muungano.
Kwa mfano, ukiangalia video, Bimani, Jusa na Ali Swalehe wanahimiza wananchi wajiandikishe ili kuweza kupiga kura ya hapana katika mchakato.
Kwa upande mwingine Mansour anaongelea kutoijadili kabisa katiba na kuiacha kama ilivyo.
Hapa kuna two school of thought.
Ya kwanza ni ya akina Bimani wanaotaka kura ya hapana. Kama umemsikiliza, Bomani amerudia mara nyingi ''haikubaliki, haipiti''
Ya pili, ni kuhusu Mansour anayetaka katiba ya Chenge isijadiliwe kabisa.
Hapa ndipo watu wanaotumia vichwa vyao wanapaswa kuvishgulisha ili kuleta maana kwa wasomaji na watu wengine.
Hakuna sababu za kuanza kuongelea mambo ya nje ya mada. Utaratibu wako wa kuvuruga mada unbakera kwa kweli.
Ningekushauri uanzishe uzi wako kuhusu yale unayodhani yanapaswa kujadiliwa.
Midhali unaingia katika nyuzi za wengine, nadhani kiustarabu na weledi unapaswa kuelewa na kuheshimu mawazo ya wengine.
Lakini pia ukumbuke kuwa kwavile unasoma na unachangia, basi darsa ni kubwa. Vinginevyo ungekuwa na darsa lako lenye akili zaidi na kuacha hili la wengine wajadiliane. Kinyume chake, kama unasoma na unachangia basi unakubali darsa
Narudia tena, vipi kama utaanzisha uzi wako na kusema unayotaka? Hili ni jukwaa huru.
Wanajamvi, tutaendelea kuziangalia video zote za kongamano na mkutano wa CCM
Nawataka radhi kwa usumbufu unaowapata. Hii ni jamii na tupo watu wa kila aina na mitazamo tofauti.
Barubaru ahsante sana kwa michango yako, tunaomba nafasi tujadili mada bila usumbufu usio wa lazima.
Mgongano wa mawazo within the paremeter and in sensible and logical way.Nguruvi3.
Ndio maana kila wakti nakuhimiza ahali yangu kuwa skuli ni muhimu sana katika kupambanua mambo.
Unajuwa wewe umejikita kwa KUAMINI KUWA MAWAZO YAKO NI SAHIHI NA WENGINE HAWANA MAANA. Kumbuka kuwa katika majadiliano yoyoye laazima kuwe NA MGONGANO WA MAWAZO AU FIKRA na hicho ndio kinaitwa majadiliano. Kila Upande uinapata nafasi ya kutoa mawazo, fikra na mtazamo wao na kuwaachia wananchi wapime.
Kumbuka hata katika hiyo KATIBA PENDEKEZWA ya Chenga/ Sitaa wananchi watatakiwa KUIKUBALI AU KUIKATAA. Na sio wananchi kulazimishwa kuikubali au kulazimishwa wote waikatae hiyo ndio demokrasia.
Nimebainisha toka mwanzo kuwa SIASA ZA ZNZ zinataka mtu awe na uelewa wa hali ya juu sana na nikabainisha ZINATAKA UENDE SKULI na kuilimika bila hivyo utakwenda halijojo au mchomo kama ulivyokwenda wewe.
Makundi yote katika katika VIDEO hizo yana mitazamo yao na kila mtu anajaribu kushawishi lakin mwisho wa siku watafikia muafaka wa nini cha kufanya. Ikumbukwe kuwa waZnz ni waelewa na wamekwenda skuli sio wa kusukumwa kikondoo kama walivyo wengi katika majirani zao.
Kwa hiyo katika hiyo KATIBA pendekezwa laazima kutakuwa na makundi
1. wanaosema mkaipigie kura ya SIO na watakupa reasons zao.
2. Wanaosema mkaipigie kura ya NDIO na watakupa reasons zao.
3. Watakaosema msiende kabisa kupiga KURA na watakupa sababu zao.
Hiyo ndio inayoitwa demokrasio.
Na hata huko Tanganyika mkianza kampeni laazima yatajitokeza makundi kama hayo na ndio maana kunatolewa kipindi maalum cha kuilimishana kabla ya kufanya maamuzi.
Lakin kikubwa kinachonishangaza kwa sasa ni namna ulivyobadili upepo kwa kasi saaaana na kuacha yale manung'uniko yako
1. Wa TGK wanaibeba Znz kwa kuwalipia umeme, mishahara kwa wizara zote za muungano n.k
2. Wa TGK wanaipa pesa SUK Znz kulipa mishahara wafanyakazi wake na kuchangia bajeti ya Znz
3. Znz haichangii muungano na hivyo muungano kuchangiwa na Bara.
Na sasa umehamia kwa kulalamika.
KWANINI ZNZ HAWASEMI hatuutaki muungano?
Suala la kujiuliza manung'uniko hayo yamekwisha mpaka umegeuka hivyo? au ndio sarakasi za mjini ikijumlishwa na darsa tulizokupa zimekuingia na kuona ukweli kwanini pamoja na kufadhwiliwa kote Znz na bara (kwa jinsi ulivyokuwa unaamini) lakin baada waZnz wanadai uhuru zaidi wa kiuchumi?
Pole sana kwa sarakasi zako. Lakin ukisikia waZnz wanavyosasambua mambo bila shaka utajifunza mengi sana na utarudi katika mstari.
Tutajaribu kuzipitia video hizi ili kubaini nakutafakari hali ya kisiasa Zanzibarhttps://www.youtube.com/watch?v=PCwc-W8mIuA
https://www.youtube.com/watch?v=P5t_842bXCs
https://www.youtube.com/watch?v=0HfChC3Uric
https://www.youtube.com/watch?v=LQLMhaNY7x0
https://www.youtube.com/watch?v=FlECaPDYzVQ
Wanaamvi
Tuliwahidi kuweka video za mkutano wa kamati ya maridhiano Bwawani znz dec 23 2014. Video zipo katika link hizo hapo juu
Pia kuna video ya CCM na jinsi walivyojadili katiba pendekezwa ya Chama chao iliyoandikwa na Chenge
Naomb mpitie video hizo ili mjadala ukiaendelea tuwe pamoja
Sijui kama umedhamiria kusema hayo kwa ushahidi au ni kwa hisia.Tafadhalisana pitia rekodi zangu ili ujiridhishe na msimamo wangu kuhusu suala lamuungano.Nguruvi3 swali kwako.
Mara kadhaa umekuwa ukiwakandamiza sana Wazanzibar kwamba wanabebwa na TGK sie wengine tulikuambia kwamba hawa wapeni nchi yao tuone kama watalalamika. Kwanini wewe usitumie nguvu hii ikubwa unayotumia katika kuwabeza badala yake ukawaelimisha wenyewe pamoja na TGK wajitoe katika muungano ambao wao wanaona wanadhulumiwa na ni kweli! Wakati wewe ukisema twawabeba? Yaani why wewe unatumia nguvu kubwa kuungana na CCM kuulinda muungano kwa kuwatisha na maneno kuwa nyie twawasaidia kwahyo mkiondoka katika muungano mtakuwa mmeumia?
Sijui kama umedhamiria kusema hayo kwa ushahidi au ni kwa hisia.Tafadhalisana pitia rekodi zangu ili ujiridhishe na msimamo wangu kuhusu suala lamuungano.
Nadhani nivema ungeonyesha wapi nimewebeza katika video walizotengeneza wenyewe.
Nitawebezavipi ikiwa sijaanza hata kuzijadili hizo video.
Usiongozwe na prejudice,ongozwa na ukweli. Nimeweka video tu, unasema nimewebeza, ni wapi
Nyuz izipo wazi , chukua muda uzipitie.
Hatahivyo, kuna hoja moja kubwa wengi hawaielewi. Wenye malalamiko ya muda mrefu niwznz kuhusiana na muungano.
Watanganyikawachache waliokuwa na ufahamu kuhusu namna gano muungano ni mzigo kwao.
Ninazungumziasuala la muungano kwa pande zote sawia.
Kwabahati mbaya au nzuri, wznz wamejitokeza sana katika suala hili kama historiainavyoeleza.
Wakatiwote wa malalamiko hakuna kiongozi wa znz aliyesimama kuonyesha msimamo Zaidi yamsimamo wa pamoja wa znz huru yenye mamlaka kamili.
Leounasikia video kama ya Sheikh akilaani muungano halafu anadai haki ya muungano.Hapo hakuna la kujadili kweli.
Ukiziangaliavideo hizo, utaona hoja zinazokinzana. Kamati ya maridhiano ikisema hili, CCMznz wakisema lile. Hakuna la kujadili kweli.
Tatizola wengi hawataki kujadili mada, wanataka kusikia wanachotaka kusikia. Sisitunasema, hapana!
Kama ipo video ya Tanganyika iletwe, na tumeshaweka nyingi tu
Sasa kuonyesha udhaifu wa wznz katika kutafuta nchi yao, jambo ninaloliunga mkono kwa dhati kabisa, imekuwa dhambi kweli!
Nimalizie kwa kusema, rekodi zipo. Msimamo wangu ni ZNZ huru, Tanganyika huru.
Kama,narudia kama ipo haja ya kuisadia znz basi uwepo muungano. Nasema hivyokwasababu sijawahi kuonyeshwa kwa mantiki na hesabu, Tanganyika inanufaika vipina uwepo wa znz.
Nguruvi3 swali kwako.
Mara kadhaa umekuwa ukiwakandamiza sana Wazanzibar kwamba wanabebwa na TGK sie wengine tulikuambia kwamba hawa wapeni nchi yao tuone kama watalalamika. Kwanini wewe usitumie nguvu hii ikubwa unayotumia katika kuwabeza badala yake ukawaelimisha wenyewe pamoja na TGK wajitoe katika muungano ambao wao wanaona wanadhulumiwa na ni kweli! Wakati wewe ukisema twawabeba? Yaani why wewe unatumia nguvu kubwa kuungana na CCM kuulinda muungano kwa kuwatisha na maneno kuwa nyie twawasaidia kwahyo mkiondoka katika muungano mtakuwa mmeumia?
HOJA KINZANI
Barubaru, umesema unaanzisha uzi, tafadhali kaanzishe tutakuja. Lau kana unajadili nyuzi za watu wengine basi ziwe katika viwango. Napata taabu baadhi ya watu wanaposema nikupuuze at the same time unaingia na kuharibu mjadala.
Please ahsante kwa mchango wako, tunasubiri uzi wako wa uchumi.
Hapa tumeshatosehaka na hoja zako dhaifu. Jasusi aliwahi kukuambia, hakuna mjadala unaochangia la maana zaidi ya kuharibu.
Hivi kwanini hujitambui hata unapopuuzwa! unaonekana kituko katika jamvi.
lengo lako ni kuharibu uzi ili tUsIjadili gizo video. Kama huwezi kuwa katika mada, basi usituondoe wengine kwa kuingiza hoja zisizo na maana. Please anzisha uzi kama ulivyosema, kama utabaki hapa uwe na adabu ya darsa. Too low PhD
HOJA KINZANI
Kwa muda mrefu wzn wa pande zote wamekuwa mtsari wa Mbele kudai znz huru yenye mamlaka kamili.Hapa ungeweka wazi ni pande gani hizo. maana CCM wanataka muundo huo huo wa muungano uboreshwe na Upinzani wanataka Znz yenye mamlaka kamili . sasa kuna misimamo ya CCM na CUF. tufafanulie hiyo pande zote unazodai weye?
Aliyekuwa waziri kiongozi Shamsa Vuai(CCM) aliwahi kukaririwa na TV star akieleza jinsi muungano usivyoitendea haki znz
Katibu mkuu wa zamani wa CUF na makamu mwenyekit Hamad Rashid aliwahi kuwa kiongozi wa serikali 3 zenye mamlaka kamili. Chama cha CUF kimegwanyika, Seif Hamada akitaka mkataba wakati Lipumba akitaka S3. hizo zote ni tofauti ya mitazamo na ndio inayoitwa demokrasia lakin mwisho wa siku wanakuja na wazo moja tu ambalo ni S3
Tume ya Warioba imekuja na pendekezo la S3 zilizoungwa mkono na wznz wengi kuliko 1 au 2 kwa kuangalia mkataba pia.
Wazanzibar waliungana kutengeneza katiba yao ya 2010 bila kujali vyama.
Lengo ni kuhakikisha znz inakuwa na mamlaka kamili.Hilo lilifanyika bila SMZ kukemea ukiukwaji wa katiba ya JMT.Hapa nafikiri Bunge la JMTz walitakiwa wafanye kama walivyofanya kuhusu issue ya Znz kujiunga na OIC. kwanini walishindwa kukemea hilo na kuufyata. Jeulize Bunge la JMTz lilipata kigugumizi gani kukemea uvunjwaji huo wa sharia?
Hivyo ni haki kusema msimamo wa znz ni kutaka S3 na wala si kuvunja muungano.huu ni msimamo wa upinzani mara bada ya kujadiliana kwa kina kuhusu aina ya muungano. Na msimamo huu hata TGK wanao pia CHADEMA, NCCR na CUF na vyama vingine vya upinzani. HAKUNA UPINZANI AU CHAMA TAWALA KINACHOTAKA KUVUNJA MUUNGANO SIOTU KUTOKA ZNZ BALI HATA TANGANYIKA. NIELEZE KAMA KUNA MSIMAMO HUO KUTOKA BARA?
Hakuna mahali ambapo kiongozi yoyote wa siasa wa znz amewahi kutamka vunja muungano.
Wakati wanaelekea Dodoma, mwanasheria mkuu wa znz aliwauliza wenzake kuhusu msimamo wao. JE UNAWEZA KUTUELEZA MSIMAMO WA TANGANYIKA ULIKUWA NINI?
tuliona akina Kificho wakijiondoa taratibu na kusahau walikuwa na makubaliano katika BLW hata kama hayakuwa ya maandishi.
Kificho alisimamia katiba ya 2010 iliyodharau katiba ya JMT. Hivyo msimamo wake na wenzake ni znz yenye mamlaka. Fair enough . KUMBUKA PIA HATA AFISI YA WAZIRI MKUU PINDA AMBAYO NAYO ILITAKA S3 ILIIKANA HABARI HIYO ACHILIA MBALI BUNGE LA MUUNGANO?
Watanganyika ambao wengi hawakujali muungano taratibu walifuatilia malalamiko ya znz. HATA WAzNZ NAO WALIFUATILIA MALALAMIKO YA JIRANI ZAO TGK YALIYOBAINISHWA NA AKINA MH KESSY, TUNDU LISU NA WENGINE
Kubwa lililojitokeza, muungano ni wa Tanganyika katika kuendesha na wa Tanzania pale panapohitaji mafao kwa wazanzibar.
Hoja za wznz zilikuwa kurudi katika mambo 11 ya mkataba wa muungano wa 1964. JE UNAWEZA KUTUDADAVULIA HOJA YA TANGANYIKA ILITAKA MRUDI KATIKA MAMBO MANGAPI YA MUUNGANO?
Hoja hiyo iliungwa mkono na Watanganyika baada ya kubaini kuwa mambo 22 hayakuwa na mafao kwao bali mzigo wa huduma.JE INAINGIA AKILINI ANAEBEBWA AOMBE YAPUNGUZWE LAKIN ANAYEBEBA ASIWE NA MAWAZO. HUO SI UZUZU KWELI AU NDIO UZEZETA?
Hivyo walipendekeza kupitia tume ya Warioba yabakizwe machache.
Katika hali ya kawaida ilitegemewa wznz wakubali mambo kupunguzwa hadi 11. JE WATANGANYIKA WALITAKA YAONGEZWE AU KUPUNGUZWA MPAKA MANGAPI?
Tume ya Warioba ikapunguza hadi mambo 7 ikitoa unafuu kwa kila upande kubeba mzigo wake.
Hilo likawashtua wznz ambao kiuchumi wanategemea JMT. SASA KAMA LILIWASHTUA WA ZNZ, KWANINI ILE KURA YA MAAMUZI YA KATIBA YA SITTA/CHENGE ILIPATA WAKTI MGUMU ZNZ NA SIO TGK?NAFIKIRI MAJIBU YA ILE KURA ILITAKIWA KUWA DARSA KUBWA KWAKO IMA WA TGK VIGEUGEU KIMSIMAMO KAMA ALIVYO MB KESSY AU ...
Ukisiliza video zote za CCM na kamati ya maridhiano, hakuna anayeongelea jinsi ya kuendesha muungano.
Hakuna anyeongelea muungano kwa faida ya pande zote.Hakuna anyeongelea gharama za muungano bali wote wanaongelea vyeo. SKULI MUHIMU SANA. SI TU BUNGE LA KATIBA YOTE HAYO YALISASAMBULIWA NA MH JUSSA NA HATA TUNDU LISSU ALIBAINISHA NA MH JUMA DUNI. NAOMBA PITIA ANSARD ZA BUNGE HILO USIKILIZE VIZURI BADALA YA KUZUA MAMBO HAPO BARZANI
Kinyume chake, wznz wamegeuka na kuwa waumini wa mfumo ule ule wa kikoloni walioulaani miaka mingi. MFUMO GANI HUO?
Wamegeuka na kukiri Nyerere waliyemwita laanatullah ni makosa. Mawazo yake ni muhimu kwao kuliko wakati mwingine. HILO LIPO WAZI ZNZ NA MAWAZO YAKE YALIPINGWA KILA KONA. Pitia kadhia ya Mzee Jumbe.
Pengine tuangalie hoja moja baada ya nyingine.
Katika video ya CCM, waziri wa SMZ amekiri wznz wanapata nafasi za elimu ya juu nyingi kuliko SMZ inavyotoa, na hilo kalisema kama neema. WACHUMI TUNASEMA HAKUNA NEEMA NI UDHALILI TU NA NDIO WANADAI UHURU KAMILI WA KIUCHUMI NA HUO NDIO MSIMAMO WA UPINZANI WOTE HUKO TANZANIA (TGK na ZNZ) NDIO MAANA WANATAKA S3
Hakueleza Watanganyika wanafadika na nini katika utaratibu wa S2 anaouelezakutoka znz. Ikumbukwe hizi ni nchi sawa na hivyo zinapaswa kuhudumiana na si moja kuwa mgongoni kwa nyakati za dhiki na kudai usawa wakati wa faraja.
Lakini waziri alikuwa na hoja muhimu sana. Kwamba, katika muungano huu znz ni tegemezi na kilichopatikana ni neema kwa maana ya mgongo wa Mtanganyika utagharamia. Waziri ameonyesha kuwa znz inanufaika na muungano na wala si Tanganyika kwa hoja yake moja tu rahisi sana. NILIWAHI KUULIZA HUKO AWALI KUWA KWANINI SERIKALI YA JMTz INAPATA KIGUGUMIZI KUTEKELEZA SHARIA YA BUNGE LA JMTz YA KUUNDWA ACCOUNT YA PAMOJA YA UCHUMI NA FEDHWA (JOINT FINANCE COMMISSION) WACHUMI TUNAJIULIZA KUNA SIRI GANI HUKO TGK
Waziri wa muungano, Samia suluhu amesema, upo utaratibu na formula imepatikana kupata ajira za BoT na TPDC. SIO TU BOT NA TPDC KINACHOTAKIWA NI KUWA NA FORMULA KATIKA WIZARA NA IDARA ZOOOOTE ZA MUUNGANO. KWANI MUUNGANO SIO TU TGK NA ZNZ WAMO. NJE YA ZNZ HAKUNA TZ.
Wakati huo huo Rais na waziri wa nishati na ardhi wa znz wanasema, mafuta na gesi si ya muungano kwa mujibu wa katiba ya Chenge wanayoipigia debe.
Hapa kuna maswali ya kujiuliza. Hivi kama mafuta na gesi si ya muungano, wapi wznz wanapata mtima na nguvu za kudai ajira TPDC ambayo haina masilahi na wala haiwahusu?Hoja hii inaeleza tatizo walilo nalo wznz la umimi. NDIO MAANA NIKASEMA USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA KIZA. TPDC SIO CHOMBO CHA MUUNGANO , NI VIPI WAINGIE MKATA WA KWENDA KUTAFUTA MAFUTA KWENYE ENEO LA NCHI YA ZNZ? MAMBO HAYA PIA YALIKUWA YANAFANYWA NA BODI YA WAHANDISI (ERB), BODI YA MAKANDARASI (CRB) BODI YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA MAHISABU etc. kuweza ku operate mpaka Znz wakti wao sio vyombo vya muungano
Ndiyo hoja aliyozungumza sheikh katika video nyingine.
Sheikh kaita muungano Dubwana baya sana. Halafu kaomba uwepo unafuu wa makontena ya znz kuingia katika Tanganyika kwa sababu ni muungano. Hapa inakuwaje, kwamba anaomba fadhila kutoka kwa dubwana baya sana. Je, alielewa anaongelea nini. NAFIKIRI HILI NILILIFAFANUA KIDOGO HUKO JUU NA NIKABAINISHA NITASASAMBU KWA KINA KUHUSU MFUMO WA MUUNGANO WA SASA UNAVYOIGANDAMIZA NA KUINYONYA ZNZ KATIKA MADA MAKHSUS
Sheikh kasema elimu ya juu si suala la muungano na halipaswi kuwa hivyo kwasababu linadumaza znz kielimu.
Waziri wa SMZ anasema wznz wananufaika sana na nafasi za elimu ya juu kuliko SMZ inazotoa.
Hapa wanajamvi mnaelewa nini ! HIYO NI MITAZAMO TOFAUTI TU NA KILA MTU AMEBAINISHA HOJA ZAKE ALIZOSIMAMIA
Ndivyo waziri Samia, Sheina na waziri Abdallah wanavyojichanganya.
Kama mafuta na gesi si ya muungano, wapi wanaingia katika maeneo kama TPDC?
Wakati huo huo, kamati ya maridhiano inasema suala hilo bado halijapata ufumbuzi.
Rais wa Tanzania ndiye mwenye ardhi na mafuta yapo ardhini. Hivyo kuna utegemezi wa Rais wa JMT katika kutafuta mafuta. UKISOMA KATIBA PENDEKEZWA NA ILE RASIMU YA PILI YA WARIOBA UTAPATA DARSA KUBWA SANA HAPA. KWANI WARIOBA AMEDADAVUA VIZURI SANA NA UTAONA UCHAKACHUWAJI ULIOFANYWA NA BUNGE LA KATIBA LA CHENGE/SITTA. YAPO MENGI LAKIN HILO NDIO TUNASEMA NI MUSWIBA MKUBWA SANA KWA TGK
Hoja kama hizi zinachanganya na kujiuliza endapo wznz wanaelewa hasa nini wanataka.
Mgaongano wa mawazo si jambo baya, lakini lazima uwe katika mantiki.NI MANTIKI GANI HIYO UNAYOITAKA WEWE. MBONA MGONGANO HUO HATA TGK UPO BAINA YA UPINZANI NA TAWALA. UPINZANI UNATAKA SERIKALI ZA MAJIMBO WAKTI TAWALA WANATAKA MFUMO WA MIKOA? AU UKITOKEA ZNZ BASI IMEKUWA NONGWA?
Haiwezekani mtawaliwa akashangilia zawadi kutoka kwa mkoloni(CCM), na anayepinga ukoloni akataka kuwepo na muungano na mkoloni yule yule asiyemtaka(KAMATI YA MARIDHIANO)
Kuna mgongano wa mawazo, kinachoonekana kwa wenzetu ni zaidi ya hapo.LABDA UTUWEKE WAZI NI KIPI HICHO? BARZANI HAPA WE FUNGUKA TU NA KAMA ITAKUPURUCHUKA TUTAKUWEKA SAWA.
Hoja zaidi za wasemaji zinachambuliwa kutoka katika video zao wenyewe
Tutaendelea
MHESHIMIWA JUSA AONGELEA UMAKAMU WA RAIS
Katika video za maridhiano six, mh Jusa ameongelea umakamu wa pili wa Rais kwa umakini, lakini pia kwa kupotosha
Mtakumbuka Jumbe alikuwa makamu wa kwanza wa Rais. Yaliyomkuta tunayajua.
Kuondolewa kwake ni kutokana na nafasi yake kama makamu wa Rais na wala si Rais wa Zanzibar
Jumbe aliitwa Dodoma na yaliyoendelea ni hadithi
Kabla ya BMK kuvugika, tulizungumzia hili. Warioba/tume walifanya busara kutenga muungano, Tanganyika na Zanzibar
Kutenga nafasi hizo kulilenga kutoa mamlaka kamili ya nchi hsuika bila kuingiliwa.
Kwa mujibu wa video, WanaCCM wa znz wanashangilia Rais wa znz kuwa makamu wa Rais
Jusa anasema, umakamu wa Rais kwa mujibu wa katiba ya Chenge inayopigiwa upatu na CCM znz, Rais wa znz atakuwa makamu daima. Hili linahakikisha kuwa hakuna siku znz itakuwa na Rais wa JMT. Hoja ya Jusa ni ya kweli
Pili, Jusa amesema, kwa itifiki Rais wa znz ambaye ni makamu hatashika wadhifa wa Urais ikitokea Rais hayupo.
Atakayekaimu nafasi hiyo ni makamu wa pili wa Rais ambaye ni waziri mkuu wa Tanganyika.
Jusa kasema, hilo ni kumuondolea Rais wa znz hadhi, kwani kikao cha baraza la mawaziri, waziri mkuu wa Tanganyika ndiye atakuwa mwenyekiti na Rais wa znz mjumbe.
Jusa anaendelea, Rais wa znz anachaguliwa, hivyo anapokuwa chini ya waziri mkuu wa Tanganyika wa kuteuliwa ni kumdhalilisha. Hilo lina ukweli.
Hata hivyo anapotosha kwa kutoangalia kwa umakini na mantiki.
Kwanza, Rais wa znz anachaguliwa na watu chini ya laki 5. Mbunge wa Tanganyika anachaguliwa na watu zaidi ya milioni.
Mfano, Jimbo la ubungo wapiga kura tu ni zaidi ya milioni moja. Hivyo, mbunge wa Tanganyika anapochaguliwa kuwa waziri mkuu, bado ana uhalali wa kidemokrasia kluliko Rais wa znz kwa mambo mengi.
- Kachaguliwa na watu wengi kuliko Rais wa znz
- Ana wajibu mkubwa kwa watu milioni 41 na uchumi unaonedesha muungano. Hivyo, hadhi yake katika msingi wa demokrasia, ulinzi na usalama pamoja na uchumi ni kubwa kuliko Rais wa znz
- Rais wa znza anachaguliwa na wznz,anpo kuja kutawala Tanganyika ni kama kuazima kiongozi.
- Makamu wa Rais ambaye ni mgombe mwenza ana uhalali zaidi ya Rais wa znz ambaye Watanganyika hawajui kapatikana kwa njia zipi. Hapa ndipo Watanganyika wanatakiwa wajiulize, hivi imefika mahali kiongozi wa taifa anaweza kupatikana kutoka popote tu bila kujali kapatikana vipi.
Ukimsikiliza Jusa kwa makini, ana hoja za msingi ambazo sijui kama wzn wanaweza kuzitazama kwa jicho mujarabu.
Rais wa znz anapokuwa makamu, tayari hadhi yake inapungua.
Rais huyo atakuwa ni makamu wa Rais wa JMT na hivyo uwezekano wa kwenda kinyume na matakwa ya JMT haupo.
Hatakuwa na nguvu za katiba ya znz bali atawajibika kwa katiba ya JMT aliyoapa kuitetea. Katiba ya znz itakuwa ni muongozo tu kama Standard operatig procedure kwake, sheria atakayosimama nayo ni ile ya JMT
Na endapo atajaribu kinyume na katiba ya JMT, historia ya Jumbe itajirudia. Ataitwa na kukabidhi funguo za ofisi.
Je hayo ndiyo mamlaka wanayozungumzia? Je, Warioba aliwaonea au aliwasadia?
Tusemezane