Duru za Uchaguzi Afrika Kusini. Umokhonto We Sizwe

Mtambachuo

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
1,907
Reaction score
3,560
Wakuu habari,

Chama cha Umokhonto We Sizwe (MK) chini ya kiongozi wake na aliye kuwa raisi wa zamani Jacob Zuma wamejizolea asilimia 13 ya wabunge wote mpaka sasa wamesha hesabu 80% ya wilaya zote, na MK imeshika nafasi ya 3. Hata hivyo ina tegemewa kuongezeka kufika mpaka asilimia 17 zoezi la kuhesabu litakapo kamilika.

ANC ndio ina ongoza kwa 41% lakini ikiwa Imepoteza idadi kubwa ya wabunge, ikifuatiwa na Democratic Alliance 22% huku EFF chini ya mwanasiasa machachari Julius Malema ikipata 9% na kushika nafasi ya 4. Hivyo kwa sasa Cyril Ramaphosa tumbo lipo joto kwa sababu itambidi azungumze na chama kingine baadae ili aongeze idadi ya wabunge.

Kilicho ni furahisha mimi ni muda mfupi wa hiki chama cha MK lakini kimeweza kuitikisa ANC. Jimbo la Kwa Zulu Natal ndio ngome kuu ya chama hiki na pia ndio asili ya Jacob Zuma.

Mimi naona wazi kuwa raisi Cyril Ramaphosa na chama chake cha ANC lazima watamtafuta Jacob Zuma kiongozi huyu mashuhuri mpigania uhuru wa Afrika kusini wamuombe kujiunga nae kufanya alliance ili waweze kupata wabunge wengi wa kufanya yeye na serikali yake kuwa na ushawishi.

Pia nime furahishwa kwa raisi mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta kuwa muangalizi wa uchaguzi. Nadhani Afrika ya Mashariki tume wakilishwa vema.

Nawasilisha.
FB_IMG_1717306859725.jpg
 
AnC wameharibu sana Ile nchi yani SA ni inaporomoka imagine SA ni ya kukosa umeme na maji safi !?
Nimeishi SA umeme kukatika kwanza haikuwepo ,hapakuwa na kutibu maji kabla ya kunywa ni unakinga unakunywa ,bidhaa bei rafiki kabisa Randi 10 unakula kabisa bila shida Sasa unahitaji Randi 50 ndio ule sio poa
 
Dah kweli na ina uma sana mkuu, SA ilikuwa mbali sana. Na mambo uliyo yasema ndio watu wame yaangazia na yanawapa hasira.

Ukosefu wa maji na umeme wa uhakika, ukosefu wa usalama, gharama za maisha kuwa juu na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira hasa kwa vijana.
 
Wamewaweka voters kwenye wakati mgumu sana maana wakirudi kwa DA ni kama kujitukana lakini ukiangalia sera za DA western cape zinafanya vizuri sana

Hii ndio sababu imempa Zuma umaarufu na huenda MK kikawa chama mbadala japo binafsi ningependa wa SA wafunike kombe wairudishe DA faster madarakani (hii ni ndoto)
 
Mkuu Mtambachuo, Democratic Alliance ni chama cha wazungu na hakiongozwi na Julius Malema. Chama cha Malema ni Economic Freedom Fighters ( EFF).
Ndio @ Mselewa asante sana kwa weka sawa nilidhani labda ni Alliance ya EFF ya Malema na vyama vingine, kumbe sio.

Kwa hiyo ina maana kwamba Julius Malema na EFF hawaja fua dafu kwenye uchaguzi huu.
 
Wamewaweka voters kwenye wakati mgumu sana maana wakirudi kwa DA ni kama kujitukana lakini ukiangalia sera za DA western cape zinafanya vizuri sana
Hii ndio sababu imempa Zuma umaarufu na huenda MK kikawa chama mbadala japo binafsi ningependa wa SA wafunike kombe wairudishe DA faster madarakani (hii ni ndoto)
Yes changamoto yao ni ubaguzi wa rangi ndio uliharibu mambo, ila kwa ujumla kipindi chao ndio Afrika Kusini iliendelea sana.
 
Ndio @ Mselewa asante sana kwa weka sawa nilidani labda ni Alliance ya EFF ya Malema na vyama vingine, kumbe sio.

Kwa hiyo ina maana kwamba Julius Malema na EFF hawajafua dafu kwenye uchaguzi huu.
Hata mimi nilijua Mapema na Chama chake ndio anaongoza kwa update ya Jana kumbe mambo yamebadirika...
 
AnC wameharibu sana Ile nchi yani SA ni inaporomoka imagine SA ni ya kukosa umeme na maji safi !?
Nimeishi SA umeme kukatika kwanza haikuwepo ,hapakuwa na kutibu maji kabla ya kunywa ni unakinga unakunywa ,bidhaa bei rafiki kabisa Randi 10 unakula kabisa bila shida Sasa unahitaji Randi 50 ndio ule sio poa
Sasa wale wabongo waliozamia huko kama umeme unakatika katika na maji hakuna warudi tu bongo ....... sisi mgao umeisha
 
Dah kweli na ina uma sana mkuu, SA ilikuwa mbali sana. Na mambo uliyo yasema ndio watu wame yaangazia na yanawapa hasira.

Ukosefu wa maji na umeme wa uhakika, ukosefu wa usalama, gharama za maisha kuwa juu na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira hasa kwa vijana.
Nikilinganisha na nyumbani hapa kila kitu kipo sawa kama ukosefu wa maji na umeme wa uwakika, garama za maisha kuwa juu kasoro amani ya uoga tu lakini vilivyobaki vyote tumeishi navyo kwa muda mrefu mpaka watanzania wamezoea😆😆
 
Mengine yanafanana kabisa
 
Back
Top Bottom